Zimbabwe nako kama Malawi? Kiongozi wa Upinzani Zimbabwe Tendai Biti "atembelewa" na wasiojulikana. Haieleweki yuko wapi hadi sasa

Zimbabwe nako kama Malawi? Kiongozi wa Upinzani Zimbabwe Tendai Biti "atembelewa" na wasiojulikana. Haieleweki yuko wapi hadi sasa

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Wakuu,

Naona huko Zimbabwe napo wameanza kujifunza mbinu za Malawi. Yaani kuna huyu kiongozi wa upinzani hajulikani hadi sahivi.

Kiongozi wa Jukwaa la Watetezi wa Katiba (CDF), Tendai Biti huko Zimbabwe nae inaonekana amekutana na wale watu wasiojulikana

Kwa mujibu wa taarifa ya CDF, mapema leo kundi la wanaume waliokuwa wakitumia magari yasiyo na namba za usajili aina ya Toyota Fortuner GD6 na Ford Ranger walifika katika ofisi ya Biti na kuizingira wakiwa na silaha aina ya AK-47.

Dereva wa Biti pamoja na wanawake waliokuwa naye ofisini hapo walishambuliwa na kupigwa kwa marungu, na dereva huyo amejeruhiwa

CDF watu hao walimtisha sana Biti ambapo walisikika wakisema jkuwa ukwaa lao la CDF halitaruhusiwa kuzinduliwa nchini Zimbabwe. Pia walidai kuwa wanafahamu shughuli za CDF na kusema kuwa watafanya zaidi ya kile kilichowahi kufanywa kwa Lovemore Madhuku.

Baada ya kundi hilo, Biti naye aliondoka ofisini kwake akiwa ameambatana na viongozi wengine wa CDF. Hata hivyo muda mfupi baadaye magari matatu yalidaiwa kuanza kumfuatilia tena gari.

biti.png


Kwa sasa CDF imesema imepoteza mawasiliano na Biti na wenzake na haiwezi kuthibitisha walipo au hali yao ya usalama.

Aidha, imeelezwa kuwa magari mengine yasiyo na alama pamoja na magari ya polisi na maafisa waliovaa sare na wengine waliovaa kiraia yameonekana kuzingira eneo la ofisi ya Biti, na pia watu wanaojaribu kupiga picha au kurekodi matukio yanayoendelea nao wanazuiwa.

tendai.png
 
Ni stage tu, itafika hatua tutavuka na kua kama Scandinavia countries
 
Uwezekano wa kuvuka ni mdogo sana, tunaweza kukwamia hapa. Scandinavia countries hawakuwahi kupitia udikteta kama huu wa KiAfrica.
Ni zama tu mkuu, sio lazima tufanane.
Dunia inabadilika, vizazi vinabadilika pia.
 
Back
Top Bottom