ZIMBABWE vs KENYA

ZIMBABWE vs KENYA

Sheghwede

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2013
Posts
277
Reaction score
123
Miaka kadhaa iliyopita, Zimbabwe waliingia kwenye machafuka ya wenyewe kwa wenyewe mara baada ya uchaguzi mkuu uliomrudisha Robert Mugabe Madarakani. Suluhisho likawa ni kutengeneza serikali ya mseto, Tsvangilai akawa Waziri Mkuu.
Kenya nao waliingia katika dimbi hilohilo 2007/08, wakapigana na kuuana. Mwisho wa siku suluhisho ikawa ni serikali ya mseto, Raila Odinga akawa Waziri Mkuu.

Katika vurugu hizo Zimbabwe ilipita pagumu, yafuatayo yakatokea.
1. Watu wengi walijeruhiwa ama kufa, na wengine kuihama nchi
2. Uchumi ulidorora, wali maharage ukauzwa ZWD 70,000,000,000/= na soda ikauzwa ZWD 60,000,000,000. Baada ya serikali mseto ikabidi kufuta sarafu, mpaka leo wanatumia USD
3. Wameishia kuwa na vikwazo vya kimataifa

kwa upande wa Kenya,
1. Watu wengi walijeruhiwa, kufa na kuikimbia nchi kwa muda mfupi
2. Uchumi uliguswa kwa mbali sana, na hiyo haikugusa kabisa mfumo wao wa fedha.
3. Hawakukutana na vikwazo vya kimataifa

Tafakari ni hii, kama wote Zimbwabwe na Kenya walipitia njia inayofanana ingawa katika mazingira tofauti ya kikatiba, kwa nini Zimbabwe mambo yawaendee kombo kiasi hicho wakati Kenya ni kama waliinama tu halafu wakainuka?

Hili ni jambo la kujifunza sana kutoka kwa wakenya, kwani nchi nyingi za kiafrika zilipoingia katika vita ya wenyewe ndio imekuwa kaburi lao. Kenya ndio imepinga hilo, imeingia katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, na bado wameinuka na wanasonga mbele. Mimi nasema tuwaige, wamepita pagumu na wamevuka, huo ni ukomavu mkubwa.
Kila nchi ya Afrika ni prospective victimu, mhanga mtarajiwa, wa yale yaliyotokea Kenya na Zimbabwe. Ivory Coast wamepita njia hiyo, na nchi nyingi za Afrika ya Magharibi, na zinasuasua baada ya bonde hilo.
Narudia tena, tujifunze kwa Kenya, they proved that they can go against the rally
 
Mazingira yanatofautiana baina ya nchi moja na nyingine...Ghana, Zambia, Malawi, ni baadhi za nchi zilizofanikiwa kuwa na mageuzi ya kidemokrasia... besides, kwanini utupe mifano ya Zimbabwe na Kenya? well zote zinafanya vizuri kiuchumi kwa sasa ukilinganisha na sisi wenye kila kitu! Zimbabwe recently wameongeza uzalishaji wa industrial Diamond, Kenya wamepata soko jipya south Sudan na hivi punde watakamilisha deal la kusafirisha mafuta hadi mombasa...Rwanda inapeta kwa kwenda mbele...kung'oa kucha na meno haviwasaidii mkuu...
 
Nadhani analysis na ulinganisho wako si sahihi hata kidogo! Kuporomoka kwa uchumi wa Zimbabwe hakukusababishwa na michafuko ya kisiasa pekee, kuna sababu nyingi na pia Kenya kuendelea kuwa na uchumi mzuri hata baada ya machafuko yaliyotokea 2007/2008 ni tofauti kabisa huwezi kuhusisha na machafuko yake! Nakubaliana na wewe kuwa kuna vitu vya kujifuna tofauti kabisa na ulivyolinganisha uchumi na machafuko!
 
Ulinganifu huu haukuzingatia matukio kabla ya uchaguzi na historia ya utawala. Mugabe amekuwepo madarakani tangu uhuru miaka ya 80 na hakukubali mabadiliko kiuraisi huku kundi la wapigania uhuru wakiwa na sauti kubwa kwenye utawala bila utayari wa mabadiliko. Hii nitofauti na kenya ambao wao walikwisha shuhudia kukoma kwa utawala wa chama kikongwe cha KANU. Zimbabwe ilitazamwa kama nchi isiyokuwa ya kidemokrasia. Lakini pia kumbuka matukio mabaya dhidi ya wapinzani huko Zimbabwe ni tofauti na Kenya. Mgogoro baina ya Mugabe na nchi za magharibu ulianza miaka kadhaa nyuma na kupelekea nchi kuwekewa vikwazo. Kenya hawakukumbwa na kadhia hii. Sera ya ardhi ilizaa changamoto kubwa na kuzorotesha uzalishaji mashambani na viwandani. Wazungu walinyang'anywa ardhi na kupewa wazawa wasiyo na mitaji ili kukidhi sera za ZANU PF na wapigania uhuru. Yote haya ni tofauti na ilivyokuwa Kenya. Mwisho mgogoro wa Zimbabwe ulidumu kwa muda mrefu hata baada ya serikali ya mseto kuundwa tofauti na kenya. Kuyumba kidogo kwa uchumi wa Kenya haukutokana na siasa bali usalama kitu kilichopelekea kenya kuingia vitani na kundi la al shabab. Kwa maelezo haya sikubaliani na mtoa hoja kuwa tunahitaji kujifunza toka kenya. Tusiruhusu migogoro maana hathari zake hazipimwi kiuchumi tu bali kisiasa, kijamii na kiutamaduni pia. Uchaguzi wa kenya 2013 umedhibitisha uwepo wa hathari za 2007/2008
 
Back
Top Bottom