Zimbabwe: Wakamatwa kwa kuuza tiketi za kwenda mbinguni

image3.jpg

Tito and Amanda Watts mtu na mkewe, walikamatwa mwishoni mwa wiki kwa kuuza ''ticket za dhahabu za kwenda mbinguni'' kwa mamia ya watu. Wanandani hawa, waliokuwa wanauza tiketi hizo kwa dola za kimarekani 99.99 kwa kila tiketi, huku wakiwaambia wanunuaji kuwa zilikuwa zimetengenezwa kwa dhahabu halisi na kila tiketi ilikuwa na uwezo wa kumpeleka mtu mbinguni-- mara ukionyesha hii tiketi kwenye lango la mbinguni unakuwa umefika, walidai.

Polisi wazungumza:
''Hatukatazi watu kuuza tiketi za kwenda mbinguni'' msemaji wa polisi wa eneo la Jacksonville alisema

''lakini hawa ndugu walifanya ulaghai '' Tiketi zilikuwa ni miti iliyopuliziwa rangi inayofanana na dhahabu huku zikiwa zimeandikwa ''Tiketi ya kwenda mbinguni- jinyakulie moja''. Huwezi kuuza kitu unachosema ni dhahabu kumbe sio. Hapa ndipo hawa wanandani walipovuka mpaka''

Tito kwenye maelezo yake kwa polisi aliandika:

"Sibabaishwi na wanachokisema polisi. Hizi tiketi ni dhahabu halisi na sio kweli kuwa nimepulizia rangi. Ni Yesu mwenyewe aliyenipa pale nyuma ya mgahawa wa KFC huku akiniambia nikauze ili nipate fedha za kwenda anga za juu.

"Kwanza nilikutana na kiumbe wa sayari nyingine anayeitwa Stevie ambaye aliniambia kuwa kama nikiwa na fedha ataninyakuwa mimi na mke wangu kwenye ungo wake unaopaa mpaka kwenye sayari yake ambayo imeumbwa kwa cocaine tupu. Nitaweza kuvuta unga wa cocaine kadiri nipendavyo... tena bila malipo.

Jaribuni kumpeleka mtu asiye na hatia jela ndio mtakiona cha mtema kuni. Kama ni kukamata basi akamatwe Yesu kwasababu ndio yeye aliyenipatia hizi tiketi na kuniambia nikauze. Niko tayari kumrikodi kwa kificho ili ukweli ujulikane"

Mke naye alijitetea:

"Nia yetu ni kuondokana na dunia hii tuende zetu anga za juu tukavute unga wa cocaine.

Sijafanya chochote. Mume wangu ndio alikuwa anauza hizo tiketi za dhahabu za kwenda mbinguni. Mimi nilikuwa mwangaliaji."

Polisi wanasema waliwakamata na zaidi ya dola za kimarekani 10,000 taslimu, mabomba matano ya kuvutia unga na mamba mdogo.

Couple Arrested for Selling "Tickets to Heaven" | CelebTriCity
Mwamposa hajaanzisha hii huduma, na yeye atakuja na mpya.

Wajinga ndiyo waliwao.
 
Muislamu akifanya nje ya Qur'an mnaanza kumkataa na kusema sio muislamu
Wewe muislamu unampima kwa kutumia nini? Shida yenu ukiona mwarabu kavaa kanzu unajua muislamu wakati kanzu ni kawaida kule kuvaa. Hata Tanzania kuna makabila uvaa kanzu kwenye sherehe zao wakati sio waislamu.
 
image3.jpg

Tito and Amanda Watts mtu na mkewe, walikamatwa mwishoni mwa wiki kwa kuuza ''ticket za dhahabu za kwenda mbinguni'' kwa mamia ya watu. Wanandani hawa, waliokuwa wanauza tiketi hizo kwa dola za kimarekani 99.99 kwa kila tiketi, huku wakiwaambia wanunuaji kuwa zilikuwa zimetengenezwa kwa dhahabu halisi na kila tiketi ilikuwa na uwezo wa kumpeleka mtu mbinguni-- mara ukionyesha hii tiketi kwenye lango la mbinguni unakuwa umefika, walidai.

Polisi wazungumza:
''Hatukatazi watu kuuza tiketi za kwenda mbinguni'' msemaji wa polisi wa eneo la Jacksonville alisema

''lakini hawa ndugu walifanya ulaghai '' Tiketi zilikuwa ni miti iliyopuliziwa rangi inayofanana na dhahabu huku zikiwa zimeandikwa ''Tiketi ya kwenda mbinguni- jinyakulie moja''. Huwezi kuuza kitu unachosema ni dhahabu kumbe sio. Hapa ndipo hawa wanandani walipovuka mpaka''

Tito kwenye maelezo yake kwa polisi aliandika:

"Sibabaishwi na wanachokisema polisi. Hizi tiketi ni dhahabu halisi na sio kweli kuwa nimepulizia rangi. Ni Yesu mwenyewe aliyenipa pale nyuma ya mgahawa wa KFC huku akiniambia nikauze ili nipate fedha za kwenda anga za juu.

"Kwanza nilikutana na kiumbe wa sayari nyingine anayeitwa Stevie ambaye aliniambia kuwa kama nikiwa na fedha ataninyakuwa mimi na mke wangu kwenye ungo wake unaopaa mpaka kwenye sayari yake ambayo imeumbwa kwa cocaine tupu. Nitaweza kuvuta unga wa cocaine kadiri nipendavyo... tena bila malipo.

Jaribuni kumpeleka mtu asiye na hatia jela ndio mtakiona cha mtema kuni. Kama ni kukamata basi akamatwe Yesu kwasababu ndio yeye aliyenipatia hizi tiketi na kuniambia nikauze. Niko tayari kumrikodi kwa kificho ili ukweli ujulikane"

Mke naye alijitetea:

"Nia yetu ni kuondokana na dunia hii tuende zetu anga za juu tukavute unga wa cocaine.

Sijafanya chochote. Mume wangu ndio alikuwa anauza hizo tiketi za dhahabu za kwenda mbinguni. Mimi nilikuwa mwangaliaji."

Polisi wanasema waliwakamata na zaidi ya dola za kimarekani 10,000 taslimu, mabomba matano ya kuvutia unga na mamba mdogo.

Couple Arrested for Selling "Tickets to Heaven" | CelebTriCity
Itoshe kusema wakristo wengi ni wajinga.
 
Muhimu ni kukumbushana na kuonyeshana njia sahihi.

Ukimuita mtu mjinga hali ya kuwa yeye Ana imani kuwa akifanyacho ni sahihi atakuona wewe adui

Wengi hawajui kuwa wanatapeliwa Otherwise wasingekwenda makanisani.

Imani kitu hatari sana
Wako wengine Uganda waliambiwa wachomwe wataingia mbinguni WAKAFA WATU ZAIDI YA 40.
 
Walevi wa cocaine na mbinguni wapi na wapi?piga viboko hao mbwa
 
Muhimu ni kukumbushana na kuonyeshana njia sahihi.

Ukimuita mtu mjinga hali ya kuwa yeye Ana imani kuwa akifanyacho ni sahihi atakuona wewe adui

Wengi hawajui kuwa wanatapeliwa Otherwise wasingekwenda makanisani.

Imani kitu hatari sana
Wako wengine Uganda waliambiwa wachomwe wataingia mbinguni WAKAFA WATU ZAIDI YA 40.
Sikatai wao kwenda kanisani Wala wao kuabudu ndio maana sikutumia neno "Wote" bali nilitumia neno "Wengi".

Kwa ujinga unaofanyika mara kwa mara ambao asilimia kubwa wanatapelika kirahisi ndipo hapo ninapowaita wajinga.
 
jamaa kweli ni mtata,....hebu mwachen amrekodi huyo Yesu kwa kificho ili angalau tumsikie hata sauti yake tu
Nilivyoanza kusoma hii habari nikajua wahanga ni wakristo, baada ya kusoma zaidi nikakuta neno YESU nikajua tayari kondoo washapigwa
 
Kila nikizitafakali akili za hao waliokuwa wakinunua tiketi hizo nashindwa kuelewa kuwa walikuwa wanatumia kiungo gani cha mwili kufikiria hadi kufanya maamuzi ya kununua tiketi....
KWELI DUNIA MSONGAMANO...
Itakuwa ni fellow drug addicts [emoji1] [emoji1787] [emoji23]
 
Nilivyoanza kusoma hii habari nikajua wahanga ni wakristo, baada ya kusoma zaidi nikakuta neno YESU nikajua tayari kondoo washapigwa
Mkuu hapa imebidi nicheke sana.
Yaani kondoo kupigwa ni kazi ndogo kama kumskuma mlevi.
We vaa kofia kubwa na joho.
Kamata speaker na mic kisha anza na kwaya kidogo kisha waambie watu umepewa unabii jana usiku .
Unauza kashata za upako.kisha hizo kashata chora msalaba.

Mpk jioni utauza Lori zima la kashata za karanga. Na kondoo wengine watakosa kashata wakichelewa.
 
Back
Top Bottom