Kingdom Finder
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 1,119
- 1,391
Kulikuwa na agreement ya mgawanyo wa ardhi uliokuwa umekubalika na waingereza (Lancaster House Agreement) na ndio wangetoa pesa kuwalipa wenye ardhi. kwa mf. kama una heka 3000 ungetoa heka 1000 kwa seriakali na kugawiwa wananchi na mwenyewe utalipwa na Serikali ya Uingereza. Kilichotokea hayo makubaliano hayakufanyika kwa wakati. Sasa baada ya kutokea chama cha upinzani chenye nguvu (MDC) hawa wazungu wakawa wana support hiki chama, na kama mjuavyo, chuki za siasa za Afrika, Mugabe akafanya kama kuwa adhibu na akaona atumie force kuwanyanganya mashamba yao na kuwagawia rafiki zake na watu wa kabila lake. Kilikuwa ni kilio kwa wazungu na ukisema waliacha laana inaweza kuwa kweli kwa sababu from there, uchumi wa Zimbabwe ulinza kwenda chini na mpaka sasa hivi hali ni mbaya sana usiombe.