GE2025 Zimeenda wapi hamasa za wadau, mijadala, warsha kipindi cha uchaguzi? Mbona kuna kimya kuelekea Oktoba?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
Tunapoelekea katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025, kuna hoja nzito ya kutafakari kuhusu hali ya elimu kwa mpiga kura, mijadala ya uraia, na nafasi ya taasisi mbalimbali katika kusaidia wananchi kufanya maamuzi sahihi ya kidemokrasia.

Miaka ya nyuma, hasa katika nyakati za uchaguzi, tuliweza kushuhudia harakati nyingi na zenye nguvu kutoka kwa wadau mbalimbali wa kijamii:

Asasi za kiraia zilijitokeza kwa wingi kutoa elimu ya uraia kupitia warsha, semina, mikutano ya hadhara na makongamano.

Vyombo vya habari vilikuwa majukwaa ya wazi ambapo wataalamu, wanaharakati, wanazuoni na wanasiasa waliweza kujadili masuala ya msingi kuhusu uongozi, sera, na haki ya kuchagua kwa uwazi na kwa usawa wa kiwango kikubwa.

Kwa kiwango kikubwa, mijadala ya wazi ilihamasisha fikra pevu miongoni mwa wapiga kura, ikichochea wananchi wengi kutafakari kwa mapana; si kwa hisia, bali kwa hoja.

Hata hivyo, kwa kipindi hiki hali inaonekana kuwa tofauti kabisa. Tukiwa tumebakiza siku chache tu kuelekea uchaguzi, ambapo ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaonesha kuwa utafanyika Oktoba 29, 2025, hali ya ukimya imegubika anga ya mijadala ya kisiasa na elimu kwa wapiga kura. Nyakati kama hizi, wadau walikuwa wakipishana kutoa elimu kwa umma na kuhamasisha makundi mbalimbali kujitokeza kugombea.

Mfano, kwa sasa tuna vyombo vingi zaidi vya habari kuliko hapo awali, lakini sauti za kielimu na mijadala yenye tija inayoweza kuwapa wananchi nguvu na uelewa wa kuchagua viongozi bora ni finyu. Ni nadra kupata mijadala huru au taarifa zenye uchambuzi wa kina zinazoweza kupanua wigo wa uelewa kwa umma.

Najiuliza maswali na kutafakari:

Kwa nini mijadala hii imepungua licha ya kuwa na rasilimali nyingi zaidi?

Je, ni ishara ya kupungua kwa uhuru wa kujieleza, au tumelegeza dhamira ya kuhamasisha raia kuchagua kwa maarifa?

Je, ni ujumbe kuwa zoezi la kuchagua na kuchaguliwa limepoteza mantiki halisi, au tunaamini uelewa wa wananchi sasa ni wa kutosha?

Na je, tunaweza kutarajia uchaguzi wenye maamuzi bora bila msingi wa elimu ya uraia kuwa imara?

Kama taifa lenye uhitaji wa viongozi bora na matumaini ya kupiga hatua. Ni wakati wa mamlaka husika hasa Tume Huru ya Taifa Uchaguzi (INEC) na mamlaka nyingine zenye kusimamia maslahi ya umma na Taifa kwa ujumla kutafakari kwa kina suala hili.

Ninachoelewa kwamba licha ya changamoto mbalimbali za harakati na shamrashamra kipindi cha uchaguzi, lakini bado kuna tija zaidi ambazo utokana na harakati hizo kipindi cha uchaguzi.
 
Uchaguzi bila chadema ni sawa na Send Off bila Ndoa.
 
No reform no election
 
Chadema msiwe na haraka, mtaona Tv zote zimejaa mpaka usiku wa matisa
 
No reform No Election.
 
No chadema hakuna uchaguzi
 
Majuzi nilisikia kwenye kituo fulani Cha redio mkoa Kanda ya kaskazini,wakitangaza wanafunzi wanaohitaji kujiunga na chuo fulani Dodoma. Na mwishoni wakatangaza kwamba uongozi wa chuo hicho unapenda kuwakumbusha wananchi waliojiandikisha kupiga kura wajitokeze kwa wingi mwezi October kwa ajili ya uchaguzi mkuu.
 
Back
Top Bottom