Cute Wife
Platinum Member
- Nov 17, 2023
- 3,054
- 8,449
Baada ya miaka 11 ya kuibuka kwa kashfa ya Tegeta Escrow mwaka 2014 iliyoihusisha Shirika la Umeme (Tanesco) na Independent Power Ltd (IPTL), sakata hilo limeendelea kuibuka kila mara likija na madai kwa Serikali.
Jana Machi 27, wakati Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kicheere akikabidhi ripoti ya mwaka 2023/24 Ikulu Dar es Salaam, alisema Tanesco inadaiwa Sh238.71 na IPTL ikijumlisha deni halisi la Sh111.48 bilioni na riba ya Sh127.2 bilioni pamoja na mgogoro kuhusu kutohuishwa kwa leseni ya IPTL kati ya mwaka 2017 hadi 2022.
Alisema kampuni hiyoimewasilisha madai mengine mengi ya fidia, gharama za uzalishaji na ada za kisheria, huku Tanesco ikidai kuwa mgogoro huo ulishatatuliwa kwa kesi Namba 200 ya mwaka 2015.
“Kwa upande mwingine, hadi Juni 2024 IPTL ilikuwa haijarudisha Dola za Marekani 148 milioni sawa na Sh389.83 bilioni zinazodaiwa na Serikali tangu Februari 2022 zilizotokana na makubaliano kuhusu fedha za Tegeta Escrow,” alisema.
Alipendekeza Tanesco kufanya tathmini ya madeni yote yanayohusiana na kampuni ya IPTL ili kubaini uhalali wake, usahihi wake ili kufikia makubaliano ya kisheria.
Kufuatia kauli hiyo, Kiongozi mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe aliandika katika ukurasa wake wa X akisema IPTL dude linalofufuliwa kila awamu.
“Mahakama ilishamaliza suala hili tena mahakama ya rufaa. Kampuni haipaswi hata kuwepo kwenye rejesta ya Brela. Yeyote anayethubutu kurudisha mzimu huu atazikwa nao.”
Zitto aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za mashirika ya Umma (PAC) mwaka 2014 alisimamia suala hilo hadi Bunge la Jamhuri ya Muungano lililopotoa maazimio kwa Serikali na wadau wengine.
Chimbuko la IPTL/Tegeta Escrow
Kufuatia uhaba wa umeme ulioikumba Tanzania mwaka 1994, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) liliingia mkataba na IPTL ya uzalishaji umeme kwa miaka 20.
Hata hivyo, mgogoro huo ulianza pande hizo kutoelewana kuhusu kiwango kinachotakiwa kulipwa kwa kila upande.
Tanesco walidai kuwa sababu ya kushindwa kufikia malengo katika maelewano ya kiasi cha kulipa walichokubaliana kati ya Aprili na Septemba 1998, IPTL walipaswa kugharamia mradi kimkakati na kwa uaminifu.
Hata hivyo, IPTL nao walidai kuwa Tanesco haikuwa imejiandaa kuingia kwenye makubaliano kwa nia njema.
Katika uamuzi wake, Mahakama haikutoa hukumu ya fidia ya fedha, badala yake ilitaka kuwepo ufafanuzi wa kiwango halisi cha tozo na ufafanuzi wa uvunjaji wa mkataba na kuagiza kila upande kutekeleza majukumu yake yaliyomo kwenye mkataba.
Mahakama pia ilielekeza kuundwa kwa akaunti ya Escrow ili tozo zilizokuwa zikikusanywa ziendelee kuwekwa hadi makubaliano ya mwisho yatakapofikiwa.
Matokeo yake fedha hizo ndizo zilikuja kuzua mtafaruku na utata, kwamba zilikuwa fedha za Serikali au za watu binafsi.
Kesi hiyo ilikuja kuzaa kesi nyingine ya Standard Chartered Bank na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ICSID Novemba 2012.
Msingi wa kesi hiyo unarudi nyuma Novemba 1, 1994 ambapo kampuni ya Mechamar na VIP Engineering ziliungana na kuunda kampuni ya IPTL (asilimia 60 ya Mechamar na asilimia 40 ya VIP).
IPTL ndiyo ilisaini mkataba na Tanesco (Power Purchase Agreement (PPA) kuzalisha umeme na ilisaini mkataba wa utekelezaji na Serikali (IA).
Juni 28, 1997 IPTL ilichukua mkopo kutoka kwenye benki za Malaysia ili kufadhili mradi huo kwa makubaliano kuwa malipo ya mkopo yatatokana na mapato ya mradi. Baadaye mkopo huo ulirithiwa na kampuni ya Danaharta Ltd na mwaka 2005.
Katika makubaliano ya mkopo huo, Standard Chartered Bank ilijiwekea ulinzi kupitia mkataba wa PPA na IA na makubaliano ya garantii ya Serikali.
Mwaka 2010 IPTL ikashindwa kulipa mkopo huo na hivyo SCB ikaanza kufuatilia deni lake kupitia mikataba hiyo na hivyo ikafungua kesi mbili ICSID.
Kesi ya kwanza ililenga kwenye mkataba wa BIT kati ya Tanzania a Uingereza na nyingine kwenye mkataba.
Pamoja na mengine SCB iliiomba Mahakama kwamba Tanzania ilipe fidia ya si chini ya dola 118,609,392.31 (zaidi ya Sh297.11 bilioni) ikiwa ni thamani ya uwekezaji ya 30 April 2010 ambayo ni mkopo wa IPTL ukiwa pamoja na riba.
Katika uamuzi wake, Mahakama ilikubaliaa na matakwa ya mkataba kati ya Tanzania na Uingereza kifungu cha 8(1) kinachotaka kuimarishwa kwa ushuriano na mwekezaji na uwekezaji wake.
Hata hivyo, ilimtaka mdai kuonyesha uhusika wake kwenye uwekezaji huo, ushahidi kwamba mdai aliufadhili mradi hautoshi. Hakukuwa na fidia yoyote iliyotakiwa kulipwa.
Baada ya Standard Chartered Bank (Hong Kong) Limited kushindwa kesi hiyo, ilifungua kesi nyingine ambayo Mahakama ilisema SCB Hong Kong ina haki kisheria chini ya kifungu cha 15.2 cha IA na ina masilahi ya kudai deni lake katika uvunjifu wa mkataba.
Mahakama pia iliona kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imevunja vifungu vya 15.3, 16.1 and 16.2 vya IA ambayo pia ilivunjwa 6 July 2018 kwa mujibu wa madai ya mdai.
Hatimaye Mahakama iliamuru Serikali ya Tanzania kuilipa SCB HK jumla ya dola 185.44 milioni sawa na zaidi ya Sh464.52 bilioni ikiwa poamoja na riba ikianzia Septemba 1, 2018 hadi muda wa malipo na kulipa gharama za kesi za zaidi ya dola 1 milioni sawa na Sh251.22 bilioni.
Katika kesi nyingine ya Standard Chartered Bank (Hong Kong) Limited dhidi ya Tanesco, benki hiyo ilitaka kulipwa fidia.
Hata hivyo, Serikali kwa upande wake ilijitetea kwamba, njia za ulinzi wa mkopo hazikuwa zikikubalika kwa sheria za Tanzania.
Lakini Mahakama ilitoa uamuzi kwamba njia hizo zinakubalika na iliitangaza SCB kuwa mkopeshaji wa IPTL na iliitaka Tanesco kulipa dola 148.4 milioni (Sh371.78 bilioni).
Tanesco ilivyoshindwa kesi
Wakati hayo yakiendelea, Tanesco ilibwagwa mahakamani katika kesi yake dhidi ya IPTL na kutakiwa kuilipa Sh371.78 bilioni.
Pesa hizo zinatakiwa kulipwa kwa Standard Chartered Bank-Hong Kong (SCB-HK). SCB-HK ililinunua deni la IPTL kwa punguzo la bei ya milioni 76.1 kutoka Danaharta Bankin ya Malaysia, August 2005 baada ya Danaharta kushindwa kuchukua mkopo wake kutoka kwa IPTL.
Hiyo ina maana kuwa SCB-HK imepata faida ya dola milioni 172. IPTL ilikopa dola milioni 100 mwaka 1998 kutoka kwenye kundi la benki za Malaysia ili kujenga mtambo umeme Tegeta wenye megawatt 100.
Hukumu hiyo ilitolewa na Mahakama ya inayoshughulika miigogoro ya uwezekaji (ICSID) yenye makao yake mjini Washington DC, Marekani na ipo chini ya Benki ya Dunia.
Kesi hiyo ilifikishwa ICSID Julai 12, 2001 ambapo Tanesco ilikuwa ikiwakilishwa na makampuni mawili ya wawanasheria R.K. Rweyongeza & Co. Advocates na Crax Law Partners ya Tanzania, pamoja na lile la Zurich, Kellerhals Carrard.