SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Watu wengi hawana upeo wa kuconnect dots kwa hiyo ngoja niwasanue jambo.
Kuna lile tukio lililotokea kule Mwanza lililomuhusisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza aliyejaribu kutumia mamlaka yake vibaya hadi kuzua taharuki kubwa.
Tukio lile halikuwapendeza baadhi ya watu wanaodhani na kuamini wana mamlaka na nguvu fulani fulani nchi hii kwa hiyo bado walibaki na vinyongo wakajiapiza watawanyoosha baadhi ya watu hadi watambue nani ni nani.
Ukiacha tukio la jana na leo la derby ya Simba na Yanga, kuna matukio yasiyopungua mawili yametokea ingawa wengi hawakuyagundua na hawakujiuliza maswali. Binafsi nayaconnect matukio yale na tukio lile la Mwanza.
Jana wakati Simba inazuiwa kuingia uwanjani kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya derby iliyokuwa ichezwe leo, mamlaka za ulinzi zilikuwepo pale uwanjani.
Kuna watu waliovaa nguo za kiraia waliohusika na kuzuia huko ambao sasa hivi kuna watu wanawakana kuwa siyo makomandoo wa Yanga ila cha ajabu hatukuona Polisi wakiwafukuza, kuwakamata wala kuwachukulia hatua zozote zile wale watu. Kwa maana hiyo ni watu waliokuwa wametambulika kuwa walistahili kuwa pale.
Kilichofanyika jana ni kuiambia Simba, nyie si kule Mwanza mliona sisi hatuhitajiki kuwepo uwanjani, sasa likitokea la kutokea msituulize sisi. Hali haitatulia kamwe hadi mbuyu utakapoangushwa. Mengine mtajiongeza wenyewe.
Mpira wetu unaharibiwa na siasa.