Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,316
- 871,876
Kuna siku nilikuwa nabarizi kando ya mto wenye kivuli kizuri.. Ghafla nikaliona joka la kijani limepiga mbizi mtoni na ghafla likaibuka na samaki kinywani
Kuna sauti ikaniambia pale lile joka la kijani likiulizwa huyo samaki unampeleka wapi kwa hakika litasema likikuwa linamuokoa asichukuliwe na maji.. Kamwe haliwezi kusema uhalisia wenye ukweli ndani take
Uhalisia ndio usahihi wa kila jambo kwakuwa kwenye uhalisia ndio hubeba dhana mbili! Sio tatu
Uhalisia wenye ukweli
Uhalisia wenye unaowakilisha uongo
Tanganyika inapitia kipindi kigumu sana cha uhalisia unaowakilishwa na uongo mkubwa
Tunapitia kipindi kigumu sana lakini pengine cha mpito cha kulazimishwa kuzoezwa uongo
Zinafanyika juhudi za kila aina kutuaminisha ya kwamba yaliyotokea zile siku tano za giza nene zilikuwa sawa na kile kisa cha nyoka aliyejifanya kumuopoa samaki mtoni ili asizame
Je samaki wa majini alihitaji msaada wa nyoka wa nchi kavu kumuokoa?
Tunahubiriwa kwamba kilichotokea ilikuwa ni muhimu kifanyike ili kuiokoa Tanganyika isiangukie mikokoni mwa watu wabaya!
Joka la kijani lililojifanya kumuokoa samaki majini limemmeza bila haya
Damu ya wasio na hatia kwa maelfu imemwagika na kuinajisi vibaya ardhi ya Tanganyika.. Hii ni laana kubwa
Damu ndio inabeba uhai.. Damu imwagikayo bila hatia huwa haiendi bure.. Ni lazima ilipe kisasi ndio inaweza kukauka na kupotea
Kwa kulitambua hilo wanafanya kila juhudi kufubaza kisasi kwa njia za mkato. Hapa ndio wanaharibu zaidi kwakuwa asili haina shortcut!
Kwa mtazamo finyu wa kutaka kufubaza kisasi cha damu wamejikuta wamazalisha zimwi la ziraili wa gizani
Hili kwasasa bado ni kinda kwakuwa bado linawatesa wale wale waliodhurumiwa haki na damu zao zisizo na hatia.. Lakini hili dude linakuwa, linapevuka, linakomaa na kupata ufahamu mkubwa.. Utakapofika wakati likajua linatumika kufubiza kisasi cha damu ndipo kutakuwa na kilio cha kusaga meno kwakuwa badala ya sisi litawageukia wao tena mara mia zaidi!
Nimemtafakari yule nyoka aliyemuopoa samaki majini....!