Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tanzania hii toka lini kiongozi kuwa mgonjwa wa muda mrefu na kuamua kujiuzulu kwa uzalendo hupi [emoji15] [emoji15]Mkuu,unajua kuwa Jaji Upendo Msuya amekuwa mgonjwa kwa muda mrefu? Msifanye kila jambo kuwa la kisiasa na kuwapakazia watu. Kujiuzulu si dhambi,ni haki ya mtu.
Acha ramli chonganishi kwakuwa,kama wengi wetu,hukuziona barua zao za kujiuzulu zinazoainisha sababu. ID yako feki isikupe haki ya kuropoka na kupakazia.
Kuwa kiongozi tz ni kujua kusoma na kuandika tuu. Au umeshasahau mkuu?Kama ndiyo hivyo hawana sifa ya kuwa Viongozi ila kwa tz inawezekana kwa ndugu zetu wakujitoa ufahamu
Kesi nyingi za serikali zinazopelekwa mahakamani ni vichekesho kwani huwa na mapungufu mengi kuanzia kwa mwendesha mashtaka hali inayopelekea wahalifu wengi kuachiwa kwani majaji wanakosa vifungu vya kisheria vya kuwatia hatianiPetro, lkini she is implicated in granting bail to drug cartel Pakistanis! Labda kwa vile kulikuwa na weakness katika defense??? akapata mwanya huo??? imesemwa hivyo??? Najua alikuwa Tanga of recent, lakini kashifa ya kuwafadhili watuhumiwa wa madawa ya kulevya imesemwa sana.....
sheria gani inazuia watu kuacha kazi? Serikali mkono mrefu km ni kweli watawapata tu .Sasa kama ni hivyo kwa nini hawakukataliwa kuachia ngazi ili badala yake wakamatwe, Washitakiwe ili sheria ichukue mkondo wake?
Watumishi wowote wa Umma wana muda wa kustaafu kwa namna mbili, Moja ni kustaafu kwa Lazima na Nyingine ni kustaafu kwa hiyari. Na kipimo cha kustaafu kwa hiyari ni pale mtumishi wa Umma anapotimiza Miaka 55,, kwaiyo anaweza kuamua kuacha kazi,,kwa maana ya kustaafu. Lakini pia kustaafu kwa lazima ni kwamba lazima ustaafu ukitimiza Miaka 60. Hawa wote wawili wanaostaafu kwa Hiyari na lazima , 55 au 60 lazima walipwe mafao yao(Pensions) na haki zingine zozote za ajira zao.Ukiwa mgonjwa kwa muda mrefu unaomba kustaafu kwa sababu ya kiafya. Jopo la madaktari (Medical Board) huundwa kukuchunguza na kutoa recommendations zake. Likiona kuwa kweli afya yako hairuhusu (unfit) kuendelea na ajira yako kwenye utumishi wa umma, basi mamlaka husika inakustaafisha na kulipwa haki zako zote pamoja na pension yako ya uzeeni.
Kujiuzulu kazi ni suala tofauti. Mtumishi kwa sababu yake yo yote ana uhuru wa kuacha kazi. Atatoa notisi ya mwezi mmoja au ya masaa 24. Akitoa notisi ya masaa 24 anawajibika kumlipa muajiri wake pesa inayolingana na mshahara wake wa mwezi mmoja (in leu of the one month notice). Kwa vyo vyote vile mtumishi aliyejiuzulu kazi ana forfeit haki zake zote pamoja na pension yake ya uzeeni. Kwa hiyo hatutegemei kuwa wamefanya haya kwa hiari yao.
Hawa hawakustaafu. Wamejiuzuru na hivyo kupoteza haki zao zote baada ya kulitumikia taifa hili miaka mingi. Hawakustaafu kwa sababu ya umri wala ya kiafya. Lazima wanakabiriwa na tatizo kubwa la kikazi.
Noted!!Watumishi wowote wa Umma wana muda wa kustaafu kwa namna mbili, Moja ni kustaafu kwa Lazima na Nyingine ni kustaafu kwa hiyari. Na kipimo cha kustaafu kwa hiyari ni pale mtumishi wa Umma anapotimiza Miaka 55,, kwaiyo anaweza kuamua kuacha kazi,,kwa maana ya kustaafu. Lakini pia kustaafu kwa lazima ni kwamba lazima ustaafu ukitimiza Miaka 60. Hawa wote wawili wanaostaafu kwa Hiyari na lazima , 55 au 60 lazima walipwe mafao yao(Pensions) na haki zingine zozote za ajira zao.
Tukirudi upande wa Utumishi wa Mahakama na tukiwazungumzia Majaji,, Nao pia wanaweza kuamua kuacha kazi /kustaafu kabla ya kufikisha miaka 60, Na kwa hapo akikubaliwa na Raisi kuacha kazi atalipwa haki zake zote za utumishi kama zinavyoelezwa sheria ya Utumishi wa Mahakama,,, namaanisha,,(Pension), Nauli, Atapewa Gari, pia atapatiwa haki zote pamoja na lump sum payment. Na kwa hapa Kuna Majaji kama Chingwile, Kalegeya,,,, hawa nao walistaafu kwa utaratibu huo ,,,yaani kabla ya kutimiza miaka ya kustaafu kwa lazima,, walikubaliwa na JK,, Na walilipwa haki zao zote kwa mujibu wa sheria.
Hata jaji James Mwalusanya naye alistaafu kwa utaratibu huo, kabla ya kutimiza umri wa kustaafu kwa lazima ,na alikubaliwa na Raisi Mkapa,, akalipwa haki zake zote.
Ukisoma Ibara ya 110(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya Mwaka 1977(Sura ya 2 T. 2002), kama ilivyofanyiwa Marekebisho;-
Mambo mawili hapo juu ni wazi kabisa kwamba Jaji aliyetimiza miaka 55 anaweza kujiuzulu kwa hiyari, ikiwa raisi ataridhia,,,Na hapa ndipo Majaji hao wakina Mujulizi walipoangukia. Sababu ya kujiuzulu haijalishi ,,ilimradi/kigezo ni kutimiza miaka hamsini ,,,whether unakwenda kutibiwa, au unakwenda kulima haijalishi, kufuga, kuolewa, kuchoka hiyo kazi.
- Kila Jaji wa Mahakama Kuu atalazimika kuacha kazi yake atakapotimiza umri wa miaka 60 lakini masharti ya ibara hii ndogo yatatumika bila ya kuathiri masharti yafuatayo katika ibara hii.
- Jaji yoyote wa Mahakama Kuu anaweza kujiuzulu kazi katika utumishi wa Umma wa Jamhuri ya Muungano wakati wowote baada ya kutimiza umri wa Miaka 55, isipokuwa kama Raisi ataagiza kwamba asijiuzulu na iwapo Raisi ataagiza hivyo, basi huyo Jaji atakayehusika na maagizo hayo ya Raisi hatakuwa na haki ya kujiuzulu mpaka upite kwanza muda wowote utakotajwa na Raisi kwa ajili hiyo.
Kwaiyo siyo kweli kwamba Majaji hao wanamatatizo makubwa na hawatapata mafao yao,, hayo ni mambo ya kuunda na kutunga.Kama ingekuwa hivyo Raisi angetumia madaraka aliyonayo katika ibara ya 110(5),6,7,8 ya katiba ya kuunda jopo la uchunguzi.
Na hata katiba inazungumza maneno kujiuzulu au kuacha kazi interchangeably,,,,,angalia ibara 110(2) na 110(4) ya Katiba ya JMT ambapo neno kuacha kazi na kujiuzulu yametumika INTERCHANGEABLY.
Hoja yako ya kuundwa kwa medical board ili kumruhusu ,tu kuacha kazi kwa ugonjwa,,, huwa inatumiwa tu pale ambapo mtumishi wa Umma hajatimiza, umri wa kustaafu kwa hiyari au kwa lazima. Yaani kama mtumishi hajatimiza miaka 55 na anaumwa kwaiyo anataka kustaafu kwa ugonjwa ndipo masharti hayo ya kuundwa jopo la wataalamu yanatumika.Na akiruhusiwa ndipo anapata haki ya kupatiwa mafao ya kustaafu kwa Ugonjwa
Kwaiyo majaji hao wamestaafu kwa hiyari baada ya kutimiza miaka 55,,,,, threshold ya kustaafu kwa hiayari,,,neno kuacha kazi lilotumika lisikupe tafsiri tofauti. Watapata haki zao zote za mafao,,kama ilivyoelezwa kwenye sheria ya mafao ya majaji.
Asante mwananzengo