Watumishi wowote wa Umma wana muda wa kustaafu kwa namna mbili, Moja ni kustaafu kwa Lazima na Nyingine ni kustaafu kwa hiyari. Na kipimo cha kustaafu kwa hiyari ni pale mtumishi wa Umma anapotimiza Miaka 55,, kwaiyo anaweza kuamua kuacha kazi,,kwa maana ya kustaafu. Lakini pia kustaafu kwa lazima ni kwamba lazima ustaafu ukitimiza Miaka 60. Hawa wote wawili wanaostaafu kwa Hiyari na lazima , 55 au 60 lazima walipwe mafao yao(Pensions) na haki zingine zozote za ajira zao.
Tukirudi upande wa Utumishi wa Mahakama na tukiwazungumzia Majaji,, Nao pia wanaweza kuamua kuacha kazi /kustaafu kabla ya kufikisha miaka 60, Na kwa hapo akikubaliwa na Raisi kuacha kazi atalipwa haki zake zote za utumishi kama zinavyoelezwa sheria ya Utumishi wa Mahakama,,, namaanisha,,(Pension), Nauli, Atapewa Gari, pia atapatiwa haki zote pamoja na lump sum payment. Na kwa hapa Kuna Majaji kama Chingwile, Kalegeya,,,, hawa nao walistaafu kwa utaratibu huo ,,,yaani kabla ya kutimiza miaka ya kustaafu kwa lazima,, walikubaliwa na JK,, Na walilipwa haki zao zote kwa mujibu wa sheria.
Hata jaji James Mwalusanya naye alistaafu kwa utaratibu huo, kabla ya kutimiza umri wa kustaafu kwa lazima ,na alikubaliwa na Raisi Mkapa,, akalipwa haki zake zote.
Ukisoma Ibara ya 110(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya Mwaka 1977(Sura ya 2 T. 2002), kama ilivyofanyiwa Marekebisho;-
- Kila Jaji wa Mahakama Kuu atalazimika kuacha kazi yake atakapotimiza umri wa miaka 60 lakini masharti ya ibara hii ndogo yatatumika bila ya kuathiri masharti yafuatayo katika ibara hii.
- Jaji yoyote wa Mahakama Kuu anaweza kujiuzulu kazi katika utumishi wa Umma wa Jamhuri ya Muungano wakati wowote baada ya kutimiza umri wa Miaka 55, isipokuwa kama Raisi ataagiza kwamba asijiuzulu na iwapo Raisi ataagiza hivyo, basi huyo Jaji atakayehusika na maagizo hayo ya Raisi hatakuwa na haki ya kujiuzulu mpaka upite kwanza muda wowote utakotajwa na Raisi kwa ajili hiyo.
Mambo mawili hapo juu ni wazi kabisa kwamba Jaji aliyetimiza miaka 55 anaweza kujiuzulu kwa hiyari, ikiwa raisi ataridhia,,,Na hapa ndipo Majaji hao wakina Mujulizi walipoangukia. Sababu ya kujiuzulu haijalishi ,,ilimradi/kigezo ni kutimiza miaka hamsini ,,,whether unakwenda kutibiwa, au unakwenda kulima haijalishi, kufuga, kuolewa, kuchoka hiyo kazi.
Kwaiyo siyo kweli kwamba Majaji hao wanamatatizo makubwa na hawatapata mafao yao,, hayo ni mambo ya kuunda na kutunga.Kama ingekuwa hivyo Raisi angetumia madaraka aliyonayo katika ibara ya 110(5),6,7,8 ya katiba ya kuunda jopo la uchunguzi.
Na hata katiba inazungumza maneno kujiuzulu au kuacha kazi interchangeably,,,,,angalia ibara 110(2) na 110(4) ya Katiba ya JMT ambapo neno
kuacha kazi na kujiuzulu yametumika INTERCHANGEABLY.
Hoja yako ya kuundwa kwa medical board ili kumruhusu ,tu kuacha kazi kwa ugonjwa,,, huwa inatumiwa tu pale ambapo mtumishi wa Umma hajatimiza, umri wa kustaafu kwa hiyari au kwa lazima. Yaani kama mtumishi hajatimiza miaka 55 na anaumwa kwaiyo anataka kustaafu kwa ugonjwa ndipo masharti hayo ya kuundwa jopo la wataalamu yanatumika.Na akiruhusiwa ndipo anapata haki ya kupatiwa mafao ya kustaafu kwa Ugonjwa
Kwaiyo majaji hao wamestaafu kwa hiyari baada ya kutimiza miaka 55,,,,, threshold ya kustaafu kwa hiayari,,,neno kuacha kazi lilotumika lisikupe tafsiri tofauti. Watapata haki zao zote za mafao,,kama ilivyoelezwa kwenye sheria ya mafao ya majaji.
Asante mwananzengo