Zinduna Talk Show: Exclusive interview na Ciello kuhusu ushindi wake wa Miss chit chat wa jana~~~~!

No.3:Katika hatua za mwanzo kwenye kupendekeza majina ya washiriki wa miss chit chat nilimpendekeza shosti wangu wa ukweli lara 1,hata nilipoulizwa kwanini sijipendekezi nilijibu wakati wangu bado,wadau walinipendekeza na katika hatua ya nusu fainal baada ya kuona nimepata mwitikio mkubwa, ndipo nilipoamua kujitosa mazima.kiukwel naona fahari moyoni na hili shindano limenisaidia kujitambua.shukrani kwa waandaaji na wadau wote mlioshiriki.
 
Last edited by a moderator:
Hatimaye malkia Ciello ndani ya nyumba. Haya tiriri tiriri mwali wetu, tunakutazama wewe sasa!
 
Last edited by a moderator:
No.5:C6 kama mdau wa chit chat anahaki ya kikatiba kukata rufaa.kama aliona mchakato haukwenda sawa ni vyema kuwasilisha vielelezo kwa kamati husika.
 
No.6:kama wadau wengine walivyopopose nadhani itakuwa jambo jema waandaaji wazungumze na mods kuwe na utaratibu wa poll count,ambayo itakuwa automatic kuepusha malalamiko.
 
No. 10: Kutunikiwa shahada yangu ya kwanza....Ilikuwa siku niliyotimiza ndoto ya marehemu mama yangu!
 
No.9:Tukio la kuondokewa na mama yangu kipenzi (Mungu amlaze pema) zikiwa zimebaki siku 10 nimalize elimu ya msingi.Ni tukio lililoumiza moyo wangu na kuyabadili maisha yangu kwa sehemu kubwa.

Pole sana, ni mapenzi ya Mungu, na kazi yake haina makosa.
je ni jambo gani muhmu maishani ulijifunza baada ya kifo cha mama.
 
No.9:Tukio la kuondokewa na mama yangu kipenzi (Mungu amlaze pema) zikiwa zimebaki siku 10 nimalize elimu ya msingi.Ni tukio lililoumiza moyo wangu na kuyabadili maisha yangu kwa sehemu kubwa.

Pole sana bibie!
 
No. 10: Kutunikiwa shahada yangu ya kwanza....Ilikuwa siku niliyotimiza ndoto ya marehemu mama yangu!

Ndoto ya mama yako ilikuwa ni wewe kutunukiwa shahada, Je ndoto yako ni nini?
 
Samahani Ciello, mtanange wa maswali unaweza kuwa mkali kulingana na jinsi utakavyokuwa unajibu maswali. jitahidi uwe una cover swali lote bila kuacha shaka.
Iwapo lipo swali ambalo uta feel uko offended, unaweza kusema huna jibu, inatosha.

Kribu tuendelee
 
Last edited by a moderator:
Hapana sijawahi tendwa,nilikuwa na mtu tulitofautiana mitazamo ya maisha so tukabreakup peaceful,at the moment niko kwenye dillema coz kuna mtu ameonyesha interest bt bado sijawa tayari.
Kwenye bold, fafanua please.
Au unamaanisha ulishawahi kutendwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…