Habari zenyu Wana-JF ...Ndiye mimi umsolopagazi Platozoom. Kwanza nashuru kwa kukaribishwa kwenye kipindi cha Zinduna Talk Show. Na bila shaka moyo unassuzika kwa sababu ninaweza kuona laptop yake kwa uzuri zaidi! Naanza kujibu maswali ya Zinduna kama hivi:
1. Je umezaliwa awamu ipi ya utawala katika nchi yetu?
Nimezaliwa katika awamu ya Kwanza ya utawala.
2. Hebu nipe kwa kifupi historia kuhusu maisha yako ya shule, yaani ni changamoto gani ambazo ulikabiliana nazo na leo hii ukiangalia ulipotoka unajiona kama shujaa.
Ebanaa eeh, mara ya kwanza kupelekwa nkwa ajili ya kuandikishwa ticha mmoja alinikataa kwa madai bado mdogo, enzi hizo unazungusha mkono wa kulia kwenye sikio la la upande wa wa kushoto.
Kuna nyakati nyingi shuleni sikuwa na viatu, na haikuwa shida sana kwa sababu karibia robo tatu hawakuwa navyo. Hakuna kilichoharibika kwa sababu hakukuwa na class za walionazo na wasio nazo.
Changamoto kubwa zaidi ni uwezo wa wazazi ambao ulikuwa wa kupanda na kushuka lakini sikuwahi kuiba wala kudhulumu. Nashukuru nilizaliwa Wilaya na mtaa wa wababe na wavuta bangi lakini sikuwahi kuitia mdomoni japo harufu yake nilivuta!!
3. Hebu nipe historia yako ya hapa JF kwa kifupi, yaani ulifahamuje kuhusu JF, ulijiunga lini na ni nini kilikusukuma hadi ukajiunga na JF?
Mimi ni msomaji mzuri wa magazeti tokea nikiwa mdogo bila kusahau vitabu vya Willy Gamba (Njama, kikosi cha kisasi n.k), magazeti (Mfanyakazi, Uhuru n Hoja) kwa hiyo ilikuwa rahisi kwangu kupata taarifa za Jamii forums na kwa sababu ya udadisi nikawa nasoma posts za watu tokea 2006 japo nilijiunga rasmi February mwaka huu.
Inaendelea..............