Mengi tu ila nalokumbuka kwa haraka ni kufaulu kwenye mtihani wa darasa la Saba.
12. Je unapenda kuvaa nguo za aina gani?
Za mtumba tena zinazofit mwili wangu.
13. Ukipata fursa ya kupata staftahi na King'asti, Je ungapenda kujadili jambo gani na yeye?
Kabla ya kujadili naye jambo lolote ningependa kumchungua kama ana kijungu na chuchu saa sita au saa kumi na mbili saa za kigoma! Halafu baada ya hapo ningependa tujadiliane naye kwa nini siku hizi mabinti wanapenda vibabu, halafu baada ya hapo ningemuuliza vipi Yule mzungu aliyemwachia e-mail kwa ahadi ya kumtumia tketi ya kuingia mamtoni ana mpango wa kumroga au ndio nipotezee tundi limekwenda bure? Zaidi ya hivyo ningependa nijadiliane naye kwa nini mabinti wa JF wanajigonga sana kwa Mods!
Ningependa kuwashukuru wasaidizi wangu waliofanikisha interview hii, fundi mitambo yupo Young Master akisaidiana na Mentor, na C6. Anayefanikisha kurusha matangazo haya ni Bujibujiakisaidiwa na Nicas Mtei na pia Jiwe Linaloishi.
swali kwa omura omweito platozoom...
kwanini ulitahiriwa kwa ganzi? huoni kama ni kinyume cha mila na desturi???? je hukuona fahari na wewe kwenda "kibhagha"?????
Nitatumia robo tatu ya bajeti kuhakikisha nalima mashamba makubwa ya mazao ya chakula na kufuta kabisa tatizo la njaa. Unafikiri hiki kizazi kwa nini ni kina akili kama za mchwa au panzi? Ni kwa sababu hakikupata chakula cha kutosha kwenye makuzi yao (kumbuka unga wa Yanga).
Mzungu akiwa na njaa ndipo akili yake inafanya kazi ya kuvumbua na kutatua matatizo lakini Mwafrika akishiba ndio akili yake inafanya kazi vizuri, lakini akiwa na njaa anakuwa mwizi, muuaji, mbea, mshari n.k.
swali kwa omura omweito platozoom...
kwanini ulitahiriwa kwa ganzi? huoni kama ni kinyume cha mila na desturi???? je hukuona fahari na wewe kwenda "kibhagha"?????
Nilipigana ilkuwa nyakati za foolish age, nilimg'oa jino (ingawa tayari lilikuwa bovu na limelegea), ugomvi wenyewe ulihusu nani zaidi. Pamoja na kunitwisha ngumi za haja lakini kwa sababu nilimtoa damu "nikatangazwa' mshindi.
Ya pili ni ugomvi wa mawe (nilikozaliwa hii ilikuwa kawaida) akanitoa ngeu ila yaliisha salama!
heheheheheeeeee
nahisi ulikuwa unalamba vidole na sahani............na sufuria pia wlaiendea ulambe
lol! maana kutaja tu mdomo umekucheza hahahahaaaa safi sana