Zingatia haya machache kutoka kwa babu

Nyanda Banka

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2023
Posts
333
Reaction score
1,261
Mwanangu,
Kwenye maisha, si kila mlango unahitaji kugongwa,
si kila siri unapaswa kuijua,
na si kila ukaribu una maana ya kwamba una ruhusa ya kuvuka mipaka.

Heshimu mipaka ya watu.
Kuna watu hawapendi kuulizwa maswali ya faragha.
Kuna wengine hujificha nyuma ya tabasamu, na si kwa sababu wanafuraha bali kwa sababu wanapambana kimya kimya.
Usivunje ukuta wao kwa makusudi kwa kisingizio cha "kujua ukweli".

Mwanangu,
Upendo wa kweli una heshima.
Urafiki wa kweli una mipaka.
Na utu wa kweli una mpaka wa kusema, "Hili si langu, nitaliacha."

Kumbuka: Mtu anapokupa nafasi ya kuwa karibu naye,
anakuamini… usivunje mipaka.
Kuwa mwangalifu na maneno yako, kauli zako, na vitendo vyako.
Kwani mara nyingi huwezi kuomba msamaha kwa jambo ulilovuka mipaka kabla hujajua madhara yake BABU
 
Shukrani sana sana BABU mwenye madini ya hekima
 
Hakuna la maana alilozungumza, sasa nakupa jambo la maana moja ambalo kamwe usilipuuze"mwanadamu ishi maisha yako yale unayohsi yanakufaa ikiwa tu unazingatia sheria za nchi hapa duniani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…