Zingatia mambo haya ukiwa gerezani

Mkuu mimi nilifikiri ukifungwa unaondolewa uhuru wako na unatakiwa kupewa mahitaji yote ya msingi kama binadamu isipokuwa ule uhuru wako wa kuchangamana na watu wengine, je, ni sahihi wafungwa kufanya kazi wakiwa gerezani endapo hukumu zao hazikueleza kwamba wanapewa kifungo na kufanyishwa kazi, ziwe nyepesi au kazi ngumu. Mwenye uzoefu wa mataifa mengine anaweza kutupatia pia....
 
Gerezani ikifika saa 10 jion inatakiwa muwe tayari mmeshalala na ukiwa huna ramani utakula had maji ya ukoko
Asubuhi utapangwa kwenye genge la kilimo alaf majembe yote unabebeshwa wewe, mkifika mbugani kila mmoja anatakiwa achukue jembe lake kimbembe inakua kila jembe zuri ukigusa kila mtu anakwambi ni la kwake

Mwisho unabaki na jembe bovu kinoma, mnaenda kukatiwa maeneo ya kulima hapo ndo utatamani ardhi ipasuke uingie ndan maana dunia inakua siyo sehem salama tena maana una jembe bovu alaf shamba ukiliangalia huon mwsho wake na unatakiwa ulime mistari kadhaa hadi mwsho wa shamba na wala siyo ombi ni amri ukifanya mchezo utachezea fimbo nyingi sana na hakuna wa kuja kukutea utalima tu kama kufa we kufa ndugu zako watarudishiwa nguo
 
Ongeza nyama kwa wale wafungwa wanaogeuzwa wanawake hii ni kweli
Gerezan huwez kugeuzwa mwanamke labda tu wewe mwenyewe uwe shoga ukifika utoe kwa hiyari kutokana na ushoga wako au upende maisha ya kitonga kwa kujitoa utu wako ila hakuna wa kukulazimisha na ni bonge la msala askari magereza wakigundua ww pamoja na mwezako mnaokulana patachimbika hapo ndan mtailewa vizuri Nini maana ya show show
 
Niliwai kufanya kazi kwenye gereza moja uko nyanda za juu kusini kuhusu Mambo ya kilimo aisee nilijifunza mengi ikiwemo

✓ mfungwa anapo ongea na bwana jela (askali magereza) inabid achuchumae chini

✓ watu wengi wanafungwa kutokana na kiburi au jeuri ( wafungwa wote nilio fanya nao kazi nilikuwa nawahoji kwa nn upo hapa lkn baada yakunijibu nilijua bila kiburi na jeuri uyu jamaa asinge kuwepo hapa)

✓ usijaribu kuomba sigara kwa mfungwa mwenzio wakati imezimwa maana huwa wanatabia ya kuchanganya na mihadarati so ikiwa on apo unaweza kugongea lkn akikwambia subilia nikuletee kataa

✓ Bwana jela anaweza kuchagua nyampala kwa muda wowote ule na kwa sababu yoyote ile kwaiyo ukiwa na nidhamu unaweza kuwa Nyampala pia Nyampala inabidi avae mkanda kiunoni kama utambuzi

✓ wale wafungwa wanyonge walikuwa wanaitwa Wajoli [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Mwisho akuna kitu kizuli kama uhuru Mkuu so ukiwa urahiani ebu tumia uhuru wako vizuri maana kule sio poa kama unaroho nyepesi ata Bwana jela uwezi kuishi maana utaona unaenda kinyume na maandiko matakatifu

Tuombeane uzima na mwisho mwema maana nafsi ya mwanadamu inahitaji maombi
 

Mkuu habari ya siku nyingi!? Skuizi umeachia front seat kwa vijana sio!?
 
Sana mwanaume hili nimelijua toka nimefikisha miaka14 kuhangaikaaa
Nimewahi mtembelea mshkaji alipigwa miaka 5,aisee vile nilimkuta nililia sn sn.Ni mwezi tu alikuwa amekaa lakini hali niliyomkuta nayo inasikitisha.



Wanaume tumeumbwa mateso
Ee
 
Kwa maelezo haya ni dhahiri Magufuli yupo motoni, maana pamoja na dhahama zote hizi yeye alikuwa anaona hazitoshi aliwasema Askari magereza wawatese kwelikweli wafungwa.

Sijawahi kuona Mtanzania katili kama huyo mwendakuzimu.
 
Chief hapa duniani kabla haujafa hauna assurance yoyote. Kitu pekee ambacho kipo certain ni kifo tu. Haya mengine yanakuja na kupita so mtu asidhani kuwa haya yaliyoandikwa hapa hayamhusu. Ni njia yetu wote.
 
Umeongea point sana dawa ni kuwaavoid watu wanaoweza kukupeleka uko
 
Miaka mitatu iliyopita nilifahamiana na ndugu mmoja wa mwenye nyumba wangu kigamboni, jamaa alikua ana muonekano wa kihuni na kiteja. Nilikuja kufahamu kua jamaa alikaa gerezani kwa zaidi ya miaka 7 kwa kesi ya mauaji yeye pamoja na wenzake.

Jamaa alikua anatembea kama mlemavu, hyo ilitokea kipindi akiwa jela baada ya kuvunjwa mguu na askari magereza, anasema kisa cha kuvunjwa mguu ilikua ni fujo walizoanzisha gerezani. Jamaa anasema kama kuna kitu cha kuogopa sana kwa mfungwa ni fujo na utovu wa nidhamu gerezani.

Miezi mitatu kabla ya kufariki aliwahi kukutana na yule askari aliyemvunja mguu mitaa ya posta yalipokuepo makao makuu ya jeshi la magereza. Jamaa anasema alionana uso kwa uso na poti alishangaa kumuona jamaa yupo nje kwa msamaha wa Rais.
Alipomkumbusha kisa cha kumvunja mguu poti alijibu "nilikua kazini nikitimiza majukumu". Kuna msemo unasema 'ugali mtamu lakini sio wa jela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…