Baba Vladmir
JF-Expert Member
- Aug 31, 2021
- 413
- 726
Tiba asili za mimea ni hazina kubwa na ya thamani sana katika ustawi wa afya ya binadamu. Kwa miaka mingi, mimea imekuwa chanzo kikuu cha utatuzi wa changamoto mbalimbali za kiafya, na hata dawa nyingi za kisasa zinazotumika hospitalini leo hii asili yake imetokana na kemikali hai zilizovumbuliwa ndani ya mimea.
Mimea ina uwezo mkubwa wa kutibu na kuleta afya njema ikitumiwa kwa usahihi na msingi wa maarifa.
Hata hivyo, siku za hivi karibuni nimekuwa nikiona machapisho (posts) mengi sana mitandaoni ambapo watu na wataalamu mbalimbali wamekuwa wakitoa ushauri wa matibabu kwa kuelekeza uchanganyaji wa mimea mingi sana kwa wakati mmoja ili kuunda dozi ya kutibu magonjwa fulani. Dhana hii imekuwa ikishawishi na kuaminisha jamii kuwa, kadri mchanganyiko unavyokuwa na mimea mingi zaidi, ndivyo unavyokuwa na nguvu na uwezo mkubwa wa kuondoa magonjwa mengi kwa pamoja.
Kutokana na ushawishi huu unaoendelea kusambaa katika jamii, leo nimeamua kutoa ushauri wa kitaalamu kwa waganga, wanahabari wa afya mtandaoni, na watumiaji wote wa tiba asili ili kulinda afya zetu.
ASILI HAIMAANISHI HAINA MADHARA"
Huu ni msingi mkuu unaopaswa kueleweka. Kila mmea una kemikali zake za asili (phytochemicals). Ukweli ni kwamba, sumu kali zaidi zinazojulikana duniani pia zinatoka kwenye mimea ya asili. Hivyo, uwepo wa kitu katika hali yake ya ki-asili hautoi dhamana ya usalama wa 100% usipozingatia kanuni za kisayansi za vipimo na utayarishaji.
MADHARA MAKUBWA YA KUCHANGANYA MIMEA MINGI ILI KUUNDA DOZI:-
Kitaalamu, kuchanganya mimea mingi kwa wakati mmoja (Herbal Polypharmacy) huingiza mwili kwenye hatari kuu zifuatazo:
1. Mwingiliano wa Sumu (Synergistic Toxicity): Unapochanganya mimea 5 hadi 10, kemikali za mimea hiyo zikikutana zinaweza kujenga misombo mipya ya kemikali yenye sumu kali ambayo haikuwepo kwenye mmea mmoja mmoja.
2. Kukatana kwa Nguvu ya Dawa (Antagonism): Mmea mmoja unaweza kufuta kabisa uwezo wa kutibu wa mmea mwingine, na kufanya dozi hiyo kuwa kazi bure au kupoteza muda wa mgonjwa kupata matibabu sahihi.
3. Kufeli kwa Ini na Figo (Organ Failure):
Ini na figo ndivyo viungo vinavyochakata na kuondoa sumu mwilini. Shehena kubwa ya kemikali mbalimbali kutoka kwenye mimea mingi huleta mzigo mzito wa kazi (metabolic overload), jambo linaloweza kusababisha ini na figo kushindwa kufanya kazi (Hepatotoxicity & Nephrotoxicity).
4. Ugumu wa Kubaini Athari (Adverse Event Tracking):Mgonjwa anapopata madhara (kama mzio, presha kushuka ghafla, au kichefuchefu), inakuwa vigumu mno kibaolojia kubaini ni mmea gani hasa uliosababisha tatizo hilo.
IDADI SAHIHI NA SIFA ZA MIMEA INAYOPASWA KUCHANGANYWA PAMOJA
Kitaalamu na kisayansi, uundaji wa dawa za mimea unahitaji usahihi wa hali ya juu (Formulation Precision):
Idadi Inayotakiwa: Dozi iliyosawazishwa vyema kitaalamu inapaswa kuwa na mmea mkuu mmoja (1)na ikibidi, uongeze mmea saidizi 2-3)pekee. Uchanganyaji wa zaidi ya mimea Zaidi ya5 bila utafiti wa kimaabara ni hatari.
SIFA ZA MIMEA INAYOPASWA KUCHANGANYWA:
1. Ushirikiano wa Kazi (Synergistic Compatibility): Mmea msaidizi lazima uwe na kemikali zinazosaidia kuongeza unyonywaji (absorption) au kufanya kazi pamoja na mmea mkuu bila kupingana.
2. Ukingaji wa Madhara (Toxicity Moderation): Mmea msaidizi unapaswa kuwa na sifa ya kupunguza ukali au athari za pembeni (side effects) za mmea mkuu (kwa mfano, kupunguza ukali kwenye tumbo au mfumo wa chakula).
3. Usalama kwenye Mfumo wa Metabolic Safety: Mimea hiyo haipaswi kushindana kwenye enzymes za ini zinazochakata dawa, ili kuzuia kemikali kujilundikana mwilini na kusababisha sumu.
HITIMISHO:-
Tiba asili ni nguzo muhimu ya afya, lakini inapaswa kuongozwa na sayansi, utafiti, na tahadhari badala ya mhemko au imani za kufikirika.
Kwa waganga na wanaotoa ushauri mtandaoni: heshimuni miili ya wateja wenu kwa kutoa dozi chache zilizofanyiwa utafiti. Na kwa watumiaji: kuweni makini na mchanganyiko wowote wa mimea mingi inayotangazwa kama "tiba ya kila ugonjwa".
KUMBUKA:
Dawa bora sio yenye mimea mingi, bali ni ile yenye mmea sahihi, kipimo sahihi, na usalama wa viungo vyako vya ndani.
MCHANA MWEMA.