Kwanza ni vyema kufahamu kuwa kuna wakati si rahisi kujua kwa dalili kuwa hapa sukari imeshuka ua imepanda. Ingawa kwa watu wa afya, historia huweza kusaidia kujua nini kinaendelea. Ushauri huwa ni kupima ili kujua nini hasa kinaendelea kwa uhakika, kwa ujumla dalili hutegemea ni kwa kiasi gani tatizo husika ni kubwa.
Dalili huusisha:
[*]kutoka jasho sana
[*]njaa kali
[*]kizunguzungu
[*]uchovu uliopitiliza
[*]kusikia kichwa kinakuwa chepesi
[*]kutetemeka
[*]kichefuchefu au kutapika
[*]ulimi kukauka/kutetemeka
[*]kuchanganyikiwa
[*]ganzi kwenye ulimi
[*]kutokuona vyema
[*]kujisikia kusinzia
[*]kichwa kuuma
[*]kuwa mkali
[*]kuwa mwenye wasiwasi
[*]moyo kwenda mbio
[*]ganzi mwili mzima
[*]kuongea wakati huwezi kutamka maneno vizuri
[*]kupoteza fahamu