Zipi Gharama za kujifungua mama mjamzito hospitali za serikali?

Zipi Gharama za kujifungua mama mjamzito hospitali za serikali?

pale masaki mbele ya Double tree
kuna Hospitali nzuri sana kwa issue kama hizo .Gharama nadha ukikunja 6 ml itapendeza. wa H.facility za viwango.
 
Hivi vifaa unavosema so ndio vile kwenye tangazo lao LA TV, wanasema vinatolewa bure kwa kila mama mjamzito wakati Wa kujifungua!? Na nimarufuku kuuziwa! Kiufupi Huduma za kujifungua ni bure, utacholipia ni malazi na complication zozote zitazotokea za kimatibabu.

Lakini kama wanavosemaga damu haiuzwi, ila unapokuwa na Shida ndo utajua inauzwa? au inabidi uwe na hela ndo uipate!
hakuna cha bure kule
 
Mi naona bora hata manesi watu wazima, hawa wadada wadada ndio shida....
Mara ya mwisho naenda chumba cha sindano nakutana na nesi mtu mzima,namuamkia "shikamoo" kanijibu "nishaamkiwa sana toka asubuhi sema shida yako uondoke" japo nlikua naogopa sindano siku ile nilitulia tuliii maana nimeogopa hata ningetingishika angeweza nitia hata dole kwa hasira.
 
Nakushauri andaa vitu vya muhimu kama ulivyoambiwa kliniki ulipomsindikiza mkeo na pia uwe na pesa ya dharula endapo lolote likatokea.
Vya bure kama vipo utapata mkuu lkn cha msingi ukifika muda tu aweze patiwa huduma inayotakiwa tuu.
Lugha za wauguzi hilo tuwasamehe tuu nao ni binadamu wanashida zao na mapungufu yao pia wengine ni misongo ya mawazo na wingi wa kazi na watu anaokutana nao kuwapa huduma.
Vifaa vya kujiandaa navyo:
Vitenge na kanga za kutosha zisiwe nyingi mpya maana kwa mtoto hazileti joto.
Mipira (glovds )
Karatasi ya nylon

Nb.hivyo si kwa kila hosp vinaweza ongezeka pia kulingana na taratibu zao.

Huduma ya uzazi popote ni bure ktk vituo vya serikali .
Maandalizi mema mkuu
 
Huna bima mkuu!? Ungetaja na mkoa uliopo ili kama kuna wajuzi wakupe coordinates za kituo kizuri na gharama zake. Vituo vya afya vingi vipo poa tu, sema kwa emergency cases za uzazi ni bora uwe katika vituo vikubwa maana hawachelewi kukuambia ambulance mbovu na wakati kishanuka.
Sina bima mkuu.
Nilijaribu kufwatilia bima ila wanadai nimechelewa kujiunga,kwa kipindi hiki cha ujauzito haiwezi kutumika kwa mama mjamzito labda tu ningekua tayari nimeshajiunga miezi 8 kabla ya huo ujauzito.
 
Nipo Morogoro,sijajua ni hospitali ipi ya serikali huku inatoa huduma bora kwa wajawazito,wenyeji mnaweza kunishauri
 
Popote kambi mkuu.
Nenda ya karibu yako usije enda ya mbali gharama ikaja nyingiñe usafiri na wa kukusaidia kipindi chote hcho itakuwa shida.
Kwa wajawazito wote wanatumia bima wanasajiriwa pindi akiwa mjamzito au anapoenda kujifungua kama hakusajiriwa hiyo ni kwa wajawazito wote bila kujali kama ni mtumishi au mkulima sijajua kama mikoa mingine ipo au laah lkn kwa sasa ndy inayotumika kama huku kusini jaribu kuulizia kama hyo kwenu ipo au laah.
 
Hakuna cha bure Mkuu, andaa mkwanja wa kutosha, vifa vyote uwe navyo na kama akijifungua kwa opareshen basi hapo ndiyo ujipange kisawasawa, inaweza kukutoka kiasi cha kutosha kabisa...
 
Nina bima ya nhif. Nimejifungua 3 weeks ago. Cjatoa hata mia pamoja nimefanyiwa c section. Huduma nzuri na nilienjoy zoez... Hosp ya gvt Benjamin mkapA - dodoma
Pole kwa kujifungua kwa CS na hongera kwa kujifungua. Good news ni kwamba siku ukiwa na bima utahudumiwa vizuri.
 
Nipo Morogoro,sijajua ni hospitali ipi ya serikali huku inatoa huduma bora kwa wajawazito,wenyeji mnaweza kunishauri
Kwa hospitali za serikali ni za wilaya au mikoa. Vituo vya afya bado haviko well equipped na inapotokea complications wanarefer hospital ya wilaya au mkoa sasa huo mlolongo wote unaweza jikuta umepoteza mtoto au mama mmemsababishia morbidity. Kwa ushauri wangu kama unaenda kituo cha afya hakikisha hicho kituo kina doctors na midwives wa kutosha, operating theater, anaesthetist na vifaa vya kutosha
 
Wakuu habari za mchana?
Natumaini mko sawa na mishe kama kawa zinasogea.
Nimebahatika kupata mwanamke mzuri ambae mpaka ninapoandika uzi huu ni mjamzito na mungu akijaalia mwezi ujao tunatarajia kupata mtoto.
Kulingana na hali ya uchumi nimeona ni vyema kujiandaa financially mapema atleast nijue ni kiasi gani kinaweza kutosha kulipa gharama katika hospitali za Serikali?
Wenye uzoefu naomba msaada na mawazo katika jambo hili.Asanteni

Kujifungua serikalini ni bure kabisa hata kama ni kwa operesheni ni bure kabisa.....vile vifaa unashauriwa uwe navyo tu kama emergency kwani wakati mama amepatwa uchungu nyumbani na ikatokea amejifungua njiani kabla ya kufika hospitali basi aweze kupewa msaada kwa hivyo vifaa vyake kwa mazingira hayo ya barabarani.
 
Kujifungua kama ni government bure labda vifaa tu uwenavyo, ila kama ni private andaa pesa na ujauzito ni kipindi ambacho unatakiwa kujiandaa kiuchumi kidogo ndomana tunashauriwa hata sie mahospital tuwe tuweka vijiakiba maana chochote kinaeza kutokea kimatumizi,
Nenda Hosp za wilaya utaona mabandiko gharama za kujifungua kawaida na upasuaji ni tofauti sasa cjui ukisema bure unamaanisha hosp za serikal za namna gn,?
 
Mara ya mwisho naenda chumba cha sindano nakutana na nesi mtu mzima,namuamkia "shikamoo" kanijibu "nishaamkiwa sana toka asubuhi sema shida yako uondoke" japo nlikua naogopa sindano siku ile nilitulia tuliii maana nimeogopa hata ningetingishika angeweza nitia hata dole kwa hasira.
Haaa haaaa!!! Umekua mtu wa kwanza kunichekesha leo
 
Back
Top Bottom