Zipi ni Spark Plug sahihi kwa gari lako?

Zipi ni Spark Plug sahihi kwa gari lako?

Acheni kudanganyana kwa kubahatisha. Ukitaka plug sahihi kwa ajili ya gari lako. Ikiwa huwezi kunavigate mtandao mppaka ukapata, nenda kwa wakala au distributor brand ya gari yako kama ni toyota, mitsubishi, benz, bmw etc watakwambia plug sahihi au alternative inayofaa kwenye gari yako.

Kununua plug hovyo hovyo madukani ndiko kunasababisha injection system za magari kuwa za hovyo, zinakosa nguvu na ni kuhatarisha injini.

acheni mazoea ya karne ya 19
 
Kwa nini haifungwi kwenye IST wakati engine ni hio hio?SO aina ya engine sio primary factor kutakuwa na factor nyingine.Nafikiri kama mwanasayansi na sio kama fundi gari.

Nilikosea kidogo. Hiyo plug inayofunga kwenye Rumioni ambayo ni FK16HR11 inafunga kwenye IST zenye 1nz fe ambazo model zake ni NCP110 na NCP115 tu. IST zilizobaki ambazo zina 1nz fe hazifungi plug hiyo.

Mfano IST yenye 1nz fe ambayo model yake ni NCP61 na NCP65 zinafunga plug za FK20HR11.

Tofauti ya FK16HR11 na FK20HR11 ipo kwenye heat range. Yaani rate ambayo hiyo spark plug inaondoa joto kadri inavyokuwa inalipokea.

Hiyo heat range kinaweza kuonekana ni kitu kidogo lakini ina uwezo mkubwa sana kwa kuathiri operating temperature ya spark plug ambayo ni 500C mpaka 950C

Joto likiwa below 500C spark plug haitoweza kuchoma vzr mafuta. Ikiwa juu ya 950C kutakuwa na pre ignition kwa maana ya kwamba mafuta yatakuwa yanaungua tu hata kama spark plug hitoi cheche sababu ya joto kali na hivyo inaweza kupelekea knocking ya engine.
 
Sidhani kama watu huwa wanazingatia hili binafsi nilikuwa sijui,mimi nauza spare but kuna hii iridium plug SK20R11 ni ya pin 1 wengi sana wanaipiga mande,yupo mmoja alitaka kuitia kwenye Corolla 5A-FE engine.

Mafundi wengi mitaani wamewakaririsha watu kwamba plugs zikiwa za sindano ufanisi wa engine unakuwa mzuri zaidi so hata ambaye gari yake haizikubali anaingia kwenye mkumbo.

Hiyo plug inafunga kwenye engine nyingi sana.

1MZ, 3MZ, 1az, 2az, 4a GE, 3s ge, 1uz, 3uz, 2zz n.k. Ni kweli kwenye mazingira kama haya ni rahisi sana mtu kuingia mkumbo.

Plug ya sindano ni nzuri kwenye nzuri kwenye engine zilizotengenezwa kwa ajili ya performance kinyume cha hapo you are looking for troubles.
 
Acheni kudanganyana kwa kubahatisha. Ukitaka plug sahihi kwa ajili ya gari lako. Ikiwa huwezi kunavigate mtandao mppaka ukapata, nenda kwa wakala au distributor brand ya gari yako kama ni toyota, mitsubishi, benz, bmw etc watakwambia plug sahihi au alternative inayofaa kwenye gari yako.

Kununua plug hovyo hovyo madukani ndiko kunasababisha injection system za magari kuwa za hovyo, zinakosa nguvu na ni kuhatarisha injini.

acheni mazoea ya karne ya 19

Nani anamdanganya nani?

Hivi ushajiuliza ukienda toyota msimbazi kule ukitaka kununua plug wanakuambia lete kadi ya gari?
 
Hivi ni kwanini watu wengi wanaamini iridium sana wakati unakuta recommendes ni platinum?

Ni changamoto. Kama hiyo niiyokutajia ni platnum.

Kuna baadhi ya plug zinafunga kwenye engine nyingi sana. Hivyo baadhi ya watu huingia kwenye mkumbo kudhani zinaweza faa kwenye kila engine.

Japo kiuhalisia Iridium ndio plug ngumu ikifuatiwa na platnum na copper ni ya mwisho.
 
Mimi kwenye Altezza 3SGE niliweka hio SK20R11 gari ikawa ina misfire, nikaweka ya platinum bker6p11 gari ikatulia jamaa mmoja ameniletea Denso IK2#4 sijataka ubishi nimeweka miss ipo kwa mbali sana
 
Mimi kwenye Altezza 3SGE niliweka hio SK20R11 gari ikawa ina misfire, nikaweka ya platinum bker6p11 gari ikatulia jamaa mmoja ameniletea Denso IK2#4 sijataka ubishi nimeweka miss ipo kwa mbali sana

Huwa inatokea. Mfano kuna avensis moja ambayo ina engine ya 1az fse D4 ilikuwa inamisi. Wakaenda toyota wakanunua plug zake tena original kabisa ambazo ni Denso SK20BGR11 wakaja kufunga. Guess what?

Misi ikawa kubwa kuliko hata zile plug zilizokuwepo ambazo siyo za engine ile. Baadae ilikuja kuonekana misi inasababishwa na shida iliyokuwepo kwenye njia ya mafuta. tatizo likarekwbishwa ila plug hawakubadili.

Kama week mbili zimepita ile gari ilipata shida tena. Nilienda kuirekebisha ikakaa sawa. Halafu ndio nikafunga na zile plug zake sasa original zilizogoma kipindi kile, gari ikatulia kabisaaa.
 
Nani anamdanganya nani?

Hivi ushajiuliza ukienda toyota msimbazi kule ukitaka kununua plug wanakuambia lete kadi ya gari?
YES...ukitaka nikupe mpaka akaunti yangu na jina langu ukathibitishe mimi ni mteja wao. Na ndicho nilichomaanisha. wanavyotaka kadi ya gari yako wanataka kutafuta kipuri sahihi original au mbadala kwa ajili ya gari yako kwa kusoma chasisi number ya gari yako.

Si lazima uende na kadi ya gari. cha msingi ni kujua chasis namba ya gari yako. wengi mnazorotesha performance ya magari yenu kwa sababu mnadhani spares hasa injection systems unaweza kununua au haijalishi mradi ni plud au oil unamwagia au kupachika tu kwenye injini.

Unatakiwa ujue chasis numbe na ununue replacement sahihi hata kama si original utaambiwa replacement sahihi/mbadala ya gari yako ni hii.
 
Kwenye number kuna vitu vina part number lakini kuna vitu vinafunga common kulingana na model fulani ya gari.

Model ya gari ipo ndani ya chassis number. Ishu ya spark plug ipo ndani ya model number na si chassis number. Mfano kuna model moja tu ya toyota Rumion toleo la kwanza. Na plug zinafunga za aina moja japo gari zina chassis number tofauti.

Mfano case kama ya sensors hapo ndio chassis number inamatter. Au unaweza kwenda na part number.

Simple.
 
View attachment 1785306

Zipo spark plug za aina nyingi sana. Yapo mambo mengi sana yanayoweza kutofautisha spark plug za gari na gari jingine.

Mambo hayo ni

1.Material yaliyotengeneza hizo plug (iridium copper n.k)

2. Urefu wa thread (nyingine zinakuwa na thread ndefu nyingine fupi)

3. Gap (nyingi zina gap la 1.1mm lakini linaweza kuongezeka au kupungua na hawashauri kuliadjust)

4. Idadi ya pini ( pin1, pin 2, pin 3 n.k.

5. Material ya tip (platnum tipped, nickel tipped n.k.)

6. Ncha ya tip (Nyingine ni sindano na nyingine zipo kawaida)

Kwa kifupi hakuna plug ambayo ni best kwa kila gari. Ndio maana, kila engine ina plug zake ambazo ni OEM ameshauri zifungwe.

Kwa baadhi ya engine ukifunga plug ambazo si sahihi matokeo yake inakuwa ni sawa tu na gari ambayo plug zake zimechoka.

Plug zilizochoka zinaweza kuwa na dalili hizi.

1. Kutetemeka engine

2. Gari kuwaka kwa shida.

3. Gari kuzima yenyewe muda mwingine.

4. Matumizi makubwa ya mafuta.

5. Gari kuchelewa kuchanganya. (Poor acceleration).

6. Pia taa ya check engine inaweza kuwaka na kutrigger code namba p0171 system is too lean. Japo hii code inaweza kuletwa na mambo mengi.

Gari yako ina engine gani? Comment model code ya gari lako nikuambie plug sahihi za kufunga.

*******######**********

1. Pia kama unahitaji Diagnosis na marekebisho kwa gari lako karibu Magomeni Mwembechai Dar.

SIMU: 0621 221 606

WHATSAPP: +255 621 221 606

View attachment 1785305
1nz engine model ya toyota Allex ya 2001 plug gani inafaa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nifunge plug gani kwenye 1ZZ Toyota wish?
 
Back
Top Bottom