Zipi sababu za mgawo wa umeme usioisha Tanzania

Zipi sababu za mgawo wa umeme usioisha Tanzania

Saa 12 au saa 1 asubuhi unarudi jioni saa 12, au wanakata saa 12 jioni unarudi saa 6 usiku halafu na kesho tena wanakata tena sasa huko kwenye kutunza vyakula Mungu atusaidie tu
Shida sana
 
Wanajukwaa,habari za wakati huu baada ya harakati za kutwa nzima ama za utumishi wa jamii, kujitafutia mlo wa siku ama kuzitafutia familia mahitaji ya kila siku. Ni matumaini yangu kuwa wengi wetu tuu buheri wa afya. Pia nitoe pole kwa wote wenye changamoto mbalimbali, iwe ni za kiafya, kijamii, kiuchumi na zinginezo nawaombea kwa Mungu mpate wepesi katika changamoto mnazopitia.

Baada ya kuwatakieni Kheri, ninalo jambo linanipa maswali mengi na kuninyima majibu. Wanajukwaa mtakubali kuwa mimi sii mwandishi wa hoja humu,ila kwa hili imenilazimu.

1. Bila shaka wengi wetu tumekuwa tukishuhudia kwa vipindi tofauti vya mwaka huu tatizo la umeme.

2. Tumekuwa tukielezwa sababu za upungufu kuwa ni sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja na ukame wa muda mrefu na kupewa matarajio,ikiwa ni kupatikana nafuu,pindi mvua ikinyesha,pamoja na kuongeza uzalishaji umeme kwa kutumia gesi.

3. Wengi tunashuhudia kiwango kizuri cha mvua,kwa kipindi cha karibuni mwezi mmoja sasa kiasi cha kuleta maafa kwa baadhi ya maeneo.

4. Wengi tumeshuhudia kuongezeka sana kwa mgao wa umeme hata baada ya matarajio ya kupata mvua hadi kuipata mvua.

5. Uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi tunayozalisha wenyewe bila shaka unaendelea,na mitambo tunayo ile ya ubungo,na kinyerezi 1 hadi 3 kama sijakosea na pengine sijasikia iwapo kama uzalishaji umesimama kwa tatizo lolote.

6. Ni maoni yangu kuwa ni vyema tuache yale mambo ya sirikali,kama yapo matatizo yanayopelekea kujikuta katika hali ya sasa,yawekwe wazi ili kujua namna ya kutatua tatizo,kwani wahenga wanasema mficha maradhi kifo kitamuumbua.

7. Wito wangu kwa wazalendo wa kweli,mwenye kujua changamoto ilipo,tulonge/tubutue tulikomboe taifa letu.

8. Vinginevyo niseme hii ni karata tarajiwa ya wanasiasa kuelekea uchaguzi ujao,kama sivyo popote walipo wafanye kama wanajikuna tuondoke kwenye hili linalodidimiza taifa letu,uchumi wa watu wake na kulemaza kazi za uzalishaji Mali na ujenzi wa taifa kwa ujumla.

9. Ukweli utatuweka huru,ukweli utachangia maendeleo ya taifa letu.Tanzania ni yetu sote tusikubali kuona inateketea.

Tatizo haliwezi kutatuliwa na akili zilezile zilizolicreate kiongozi, labda tukafunge na maombi na kupanga tunguli zetu upya! So sad, kunywa mtori subiri nyama ziko chini, hata inyeshe mvua ya dhahabu bado akili kisoda zitasema nyaya zimekatwa na kunguru japo mabwawa yamejaa, mgao upo miaka 25 sasa unashtuka leo? Wao hawajui washasahau wanajua umeanza jiwe alivyokufa
 
Hadi stock ya magenerator iishe ndio mgao wa umeme utaisha hi nchi imeshashikwa na mafisadi

Jana Kuna sehemu nilikuwa nimekaa kkoo mtaa wa Uhuru Kila Baada ya dk 5 au 10 ilikuwa inapita Zusuki Carry imebeba Generator jipya
 
Kwani zile kampuni zinazozalisha umeme kwa gesi na kuuzia Tanesco, zimelipwa madeni yote? maana inawezekana hizo kampuni hazijalipwa malimbikizo ya madeni na wakaamua kufunga koki.

Wakati unaaangalia hayo, ukumbuke kuwa mkurugenzi wa tanesco wakati akiapishwa, anakula na kiapo cha kutunza siri zote za serikali atakazozijua wakati wa kutekeleza majukumu yake, kitu ambacho kinambana kuongelea ukweli huo wa madeni, mbele ya vyombo vya habari.

Hayo ni mawazo yangu tu. [emoji3][emoji3]
 
Swala la umeme bongo kukoma , ni baada ya 50 yrs ahead uko.
Au labda kichukue chama pinzani japo ni ndoto.
 
Kinachoudhi zaidi ni kwamba muda ambao umeme unahitajika zaidi kwa wengi ndiyo unakatwa.

Kwenye familia nyingi saa moja hadi saa nne usiku ndiyo umeme haukupaswa ukatwe halafu unauleta saa nne usiku ili iweje sasa?
 
Back
Top Bottom