Pakome
JF-Expert Member
- Dec 8, 2024
- 1,651
- 1,129
Zipo baadhi ya tabia ambazo Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere alisema ni za kipumbavu ikiwemo Udini na Ukabila, Je kwanini tumeruhusu tena?
Lazima Tanzania turejelee upya kauli na maonyo ya Baba wa Taifa ili Tanzania ipone
Katika tabia ambazo Baba wa Taifa aliziita ni za kipumbavu ilikuwemo Udini na Ukabila
Baada ya maonyo yale tulipaswa kuachana na huo upumbavu ili tusonge mbele
Nikama tumesahau sasa habari za Udini zimeshamiri si haba kusikia Wakatoliki au Waislamu wamefanya hivi wamefanya vile mara Father Kitima mara Shehe fulani
Si haba kusikia habari za Wazanzibari na Watanganyika imefikia pahali watu wameanza kuitamka sana Tanganyika na Zanzibar badala ya Tanzania lakini jambo kubwa zaidi hawakumbuki tena kuwa Tanganyika na Zanzibar ilishaungana tangu mwaka 1964
Si vibaya kuizungumzia Tanganyika bali ingekuwa sahihi kuizungumzia kama historia kubwa iliyowahi kutokea hapo zamani wala si vibaya kuizungumzia Dini kwani ndiyo msingi wa maadili lakini tujiulize je tunaizungumzia dini katika taswira ipi? Je katika kufundisha maadili au kuchokozana?
Sote kwa pamoja lazima tukubali kuwa tunakosea na tukubali kuwa tumeamua kuwa wajinga kama baba wa Taifa alivyosema
Na tujiulize je tumeamua kurudi nyuma kwenye ujinga aliotutoa Baba wa Taifa au tunataka kwenda mbele?
Kucha kutwa chokochoko na vijembe kama Kidawa badala ya kujadili namna ya kuleta maendeleo makubwa zaidi ya haya tuliyonayo
Mataifa Makubwa kama China na Japan pamoja na kwamba yana maendeleo makubwa sana bado yanakiri hayajafanikiwa katika kiwango kinachotosha
Je ni kipi kinachotufanya turidhike na kujiingiza kwenye vimaneno vya chini chini visivyoisha badala ya kuhangaika na maendeleo?
Je tumelogwa na nani? Binafsi naona ni sahihi kutunga Sheria ya kudhibiti vimaneno vya chini chini pengine itatusaidia kutukumbusha kuwa tunatakiwa kuelekeza akili zetu kwenye maendeleo na sio migogoro ambayo inaweza kusambaratisha Taifa