Zipo wapi zile kejeli za wachambuzi waliokuwa wanaishambulia Yanga Sc haswa kwenye michuano ya kimataifa?

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Ama kweli Yanga Sc imewafunga midomo wachambuzi wa michongo waliokuwa wanatumika vibaya kuiponda Yanga Sc kila kunapokucha.

Nakumbuka msimu uliopita Yanga Sc ilipotupwa kwenye michuano ya kombe la shirikisho waliibuka watabiri /waganganjaa waliokuwa wakichambua Yanga Sc kila kukicha "mala oh oh Yanga haitofika mbali" mala ohh ohh Yanga sc kimataifa hawana uwezo siyo michuano Yao kabisa"

NALIA NGWENA nimepita kwenye page za wachambuzi wa michongo wapo kimya Sana na hawaongei chochote kuhusu Yanga Sc hii Ni tofauti na msimu uliopita,

Yanga sc watachuana na Belouzidad ya Algeria cha kushangaza wachambuzi wa michongo waliokuwa wakilipwa ili wasambaze propaganda wapo kimya, hata wazee wa statistics kuchambua ukubwa wa Belouzidad Fc kiuchumi, kimafanikio nao wapo kimya.

Kipigo cha Goli tano kimewafunga midomo wachambuzi waliokuwa wanalipwa ili kuishambulia Yanga Sc.
 
Yanga ina wachezaji bora sana wanaweza kucheza na Timu yeyote swala la matokeo ni kitu kingine kinachotakiwa Yanga huko Algeria wawaheshimu wapinzani wetu basi wasitake kupishana na Waarabu uzuri wa Yanga wanaweza kutunza mpira kitu ambacho ndio sumu ya Waarabu wote ukiwa na wachezaji wenye uwezo wa kumiliki mpira lolote linatokea...
 
Kila la heri kwetu.
 
na msimu huu sio kunyamaza tu watakimbia mji kabisa...
 
Mmeanza kukua kama SIMBA tulizeni akili na muishukuru sana Simba kwa kuwa ndio roll model wenu
 
Acha kujitoaufaham wewe, sasa unataka waandikwe kwa kipi cha ajabu walichofanya huko CL?, au ndo kumfunga Simba basi unataka hao wachambuzi waseme/waandike sasa nyuma mwiko wamejihakikishia kufika Robo CAFCL sio?
 
Watu mkilala mpira, mkiamka mpira. Kila la kheri
 
Akili matope hizi,sisi role model wetu ni mamelod sundowns..Simba awe role model wetu wakati hata shirikisho haujawahi kufika semi final!!
Lala ukue, halafu ureje tena kwenye jukwaa hili kusahihisha huu ujinga wako uloandika kwenye huu uzi.
 
Hiyo ni sumu kwa waarabu uchwara pekee sio wale wanaoujua mpira... Hata Sundowns waliweka posesheni futbol pembeni kwanza japo ndo utamaduni wao na waka opti kucheza dairekti futbol na wamebeba AFL, hutaki endelea kukaza ubongo.
 
Allende anamiliki mpira Mokwena anatunza mpira Zwane anatunza mpira Zungu anatunza mpira Mudau ndio kabisaa aliwafunga waarabu wote kwa sababu wana uwezo wa kutopoteza mpira kizembe ni pass nyingi hata ukiangalia possession yao waliwazidi karibu Waarabu wote ukiona Timu beki anamwanzishia Kipa ndani ya sita mpira wa kuanza jua hao watu Mpira wanajua hawabahatishi mpira upo wazi na kila mtu kaona...wale Mazembe walipokua wanawafunga Waarabu walikua na watu wenye uwezo wa kumiliki Soka...
 
Hiyo ni sumu kwa waarabu uchwara pekee sio wale wanaoujua mpira... Hata Sundowns waliweka posesheni futbol pembeni kwanza japo ndo utamaduni wao na waka opti kucheza dairekti futbol na wamebeba AFL, hutaki endelea kukaza ubongo.
Hivi gemu za mameload uliangalia kweli mkuu.
 
Acha kujitoaufaham wewe, sasa unataka waandikwe kwa kipi cha ajabu walichofanya huko CL?, au ndo kumfunga Simba basi unataka hao wachambuzi waseme/waandike sasa nyuma mwiko wamejihakikishia kufika Robo CAFCL sio?
Kwani kipindi kile wachambuzi wanaipamba monastr ya Tunisia river ya nigeria, Tp mazembe kwani Nani alikua anawaambia waandike.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…