Zipo wapi zile shule zetu za vipaji maalumu?

lyinga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2013
Posts
2,496
Reaction score
1,057
Ndugu wanajamvi,

Nimekuwa nikiumia sana kwa jinsi siasa mbovu za hii nchi yetu zilivyoingizwa kila sekta ya nchi. Nakumbuka wakati ambao tulikuwa hatujaingiliwa na mmomonyoko wa maadili kulikuwa na shule nzuri kama Ilboru,Azania,Forodhani,Tabora boys,Rungwe, na nyinginezo zilikuwa zinafanya vizuri sana.

Lakini kuanzia viongozi waanze kumiliki shule zao binafsi wametuulia elimu nzuri iliyokuwepo hapo awali, zimebaki shule za makabwela na waliokuwa nacho na hata mitaala wanayoitumia ni tofauti.

Huwa najiuliza nchi moja inawezaje kuwa na matabaka mawili ya elimu wakati njia tunayokwenda ni moja?

Nawaonea huruma watoto wa kizazi hiki kwa kuwa wanajengewa mazingira ya chuki kutokana na kuwepo na tabaka la waliokua nacho na wasiokuwa nacho.

Tunachokiona sasa kwenye nchi za wenzetu uarabuni kwa miaka ijayo yatatufika Tanzania ni nani alieiuwa elimu ya Tanzania?
 
Mkuu, kama ataamua kusomesha hapa nchini, ni "kiongozi" gani asiyependa binti yake asome St. Francis, Marian Girls, Eden Garden, Rosmin Sisters, n.k? Ni mtawala gani asiyependa kijana wake asome Marian Boys? St. Joseph Millenium? Eden Garden? St. Gasper, Fezza, n.k.?

Kama wanavyokimbilia kutibiwa India, SA, Germany, St. Thomas, na kwingineko hadi kuua kabisa zahanati zetu, ndivyo hivyo wanavyozimalizia shule zetu tulizoachiwa urithi tangu enzi za Baba wa Taifa.
 
Viongozi wengine wasingeenda shule za msingi,sekondari na vyuo kama mazingira ya wakati huo yangekuwa kama ya leo.Wengine hata viatu walivivaa walipokuwa sekondari
 
rungwe na azania hazijawahi kuwa shule za wenye vipaji maalum
 
Ada ya hizo shule usipime!! sisi tusio na kipato tunathaminiwa wakati wa kampeni na uchaguzi !! eee Mwenyezi Mungu tunusuru na hili tanuri la moto, tumeanza kuungua tungali duniani.
 
Kuna ule usemi unaosema mwenye shibe hamjui mwenye njaa, natumaini hata wakipitia hapa hawataelewa. Watasema ni chuki na upinzani usio na maana. Tunazifagilia shule za kata majukwaani, lakini hatuwapeleki watoto wetu huko? Lazima tujitathmini upya kwenye hili na kuchukua hatua madhubuti, la sivyo mfumo huu unaoendelea utakuja kuleta madhara makubwa baadaye kuliko tunayoyaona sasa.
 

Mkuu mbona hujataja Alharamain, Kinondon Muslim, Almuntazir, Thaqafa, Ubungo Islamic, Qiblaten, Osama high school, Kirinjiko...,???
 
Shule nzuri kama Iyunga tech, mazengo tech,ifunda tech n.k zilikuwa zinachukua na kuandaa Engineers weledi kupindukia lakini maskini ya Mungu watawala wameziua! shule zilikuwa na wanafunzi the best in mathematics and science in general. Lakn sikuhizi watoto wanaopt science ni wachache sana na as a result hata walimu nao ni very very scarse!
Mungu tunusuru wajawako.
 
Iliboru, Tabora boys,Kibaha,Mzumbe mpaka leo mwendo mdundo kaangalie waliofanya vizuri mitihani yao huwakosi shule hizi,hizi zinazo ibuka kama uyoga tena mpaka paper zivuje ndo utazisikia hivyi hiyo fezza ilikuwa ya ngapi matokeo kidato cha sita mwaka uliopita? ilikuwa na one ngapi? ukipata hilo jibu linganisha na hawa magwiji wa taaluma.
 

kaka nimesoma ulichoandika nimeshawishika na mimi kucomment.....

1. tanzania ni nchi masikini kwa sasa, na ilikuwa masikini toka zamani. (kabla hata ya uhuru tulikuwa masikini).
suala la msingi lililopo tunashindwa kujua kwa nini sisi masikini, ukianza kuuliza mtu mmoja mmoja,, kwa nini sisi
masikini basi 80% hawana jibu sahihi, zaidi utasikia ufisadi,rasilimali zetu nk

2. umeongea point ya maana sana, technical school, masomo ya science. nani anasoma haya masomo kwa sasa,
ukienda kwenye shule zetu utakuta madarasa ya arts na biashara ndio yamejaa, kwenye vyuo vyetu watu wanasoma
procurement, political science, bussiness administration, accountants,laws hivi vitu havina nafasi katika taifa lolote
masikini, ukitaka ushahidi soma mataifa yaliyoendendelea wakati yapo masikini yalifanya nini kujikwamua?? nchi haina
technologists wakutosha na watu hawataki kusoma, kazi inayohitaji wahasibu 4 unakuta wameomba watu 3000, kazi
inayohitaji engineers 4 utakuta wameomba watu 3,

3. hakuna mwanasiasa mpaka sasa niliyemsikia anaongelea hili wote CDM, CCM, CUF, NCCR wako kimya kwenye hili, nchi haina technologist na hakuna mikakati yoyote, vijana hawataki kusoma field za science,,, kila mtu anasomea kuja kukaa ofisini,, site/polini tumeacha wazungu, wenyewe tuko mjini unategemea nini hapo, mwisho wa siku vijana wakikaa kwenye mitandao wao ni facebook, tweeter nk,, kwa sababu hawana cha kusoma humu, sio matechnologist, field walizosoma hazina impact kwenye dunia yetu inayokimbia.


*** TANZANIA NA AFRICA ZITAKUWA MASIKINI DAIMA,, ISIPOKUWA USINGIZI UKIISHA,, TUMESHAAMBIWA DUNIA NI
YA SCIENCE NA TECKNOLOGIA,, NYIE HAMTAKI KUSOMA SCIENCE....MNAKIMBILIA KWINGINEKO..
 

Umenikumbusha mbali! kipindi nasoma ile shule ya msingi Manyara Ranch( 1988 -1994) kweli Tanzania ilikuwa in a andaa taifa lenye nguvu kila seckta! nakumbuka walikuwa pia wanaletwa wale walio kuwa wanasoma inayoitwa Arusha School ambayo ilikuwa international school cha ajabu ndio waliokuwa hata maksi 200 hawafikishi wakati unakuta kuna majamaa yalikuwa yanapiga hadi maksi 1000 hadi 1200 yaani mtu hafeli! tulikuwa kila mwisho wa mwezi ni mitihani 12 na unatakiwa upate maksi kuanzia 600 hapo ndio umefaulu ukipata 599 umefeli hapo adhabu ya golgota inakuhusu! kweli uzalendo ukakamavu na mambo mengi ya kuipenda nchi na kujitegemea tulijengewa mioyoni mwetu! ubunifu ulipewa kipao mbele huwezi amini hata wanajeshi walikuwa wanakuja kuangalia maendeleo yetu! na yote haya tulikuwa hatulipi hata sumni natulipewa kila kitu bure na ni kwa huduma sawa na watoto wenzetu waliokuwa majumbani! nchi ilikuwa inaandaa wachapa kazi na wazalendo! haya ma Academic na ma international ambayo baada ya uhuru Nyerere aliyafuta wameyarudisha ili kutengeneza fedha tu na sio kwamba wanajali elimu no way! kuabudu kiingereza ndio kuwa na elimu bora!!? ujinga wa kutokupenda vya kwako na kuabudu fedha! China wako wapi na kichina chao?? Viongozi wamebaki na misifa tu ya nina PHD nina MASTER na manenono ya mikogo mikogo wakati ukimpa mtihani kuhusu hilo li CV hajui aanzie wapi! mnawacheka babu zetu walipewa kio wakatoa ardhi na nyie mnapewa makaratasi sasa manatoa hadi vya uvunguni mwenu bora hata babu zetu walipogundua wamedanganywa walipigana kurudisha vya kwetu nyie mtafanya nini zaidi ya kukimbilia Uswis?
MUNGU AWALAAANI NA KILA SIKU AMUONDOE MMOJA WENU HAPA DUNIANI! MNAKERA
 
rungwe na azania hazijawahi kuwa shule za wenye vipaji maalum

Hata kama hazikuwahi kuwa za vipaji maalumu lakini zilikuwa zinatoa elimu nzuri siasa zetu hazina tofauti na kupiga ndumba majungu na uchawi, ubinafsi ndio unaoiongoza siasa za tanzania wameuwa elimu, reli, viwanda, mashirika ya uma, km uda wanajimilikisha wenye nacho halafu wana kuambia eti kiswahili ni lugha ya taifa itumike kufundishia mashuleni, huwa najiuliza mbona hizo wanazopeleka watoto wao zinatumia kiingereza tena mitaala wanayotumia ni ya nje ukienda kwenye mahakama na mikataba yote imeandikwa kiingereza jamani ndugu zanguni tuamke hawa watu hawana nia nzuri na sisi watakuja kutuchonganisha hawa tuwe kama jamuhuri ya kati ilhali wenyewe na uzao wao wapo ulaya wanakula bata 2015 tuukatae ukoloni mambo leo.
 
Walimu wenyewe pia ni scarce... Wengi wao wanaofanya kazi ya ualimu wanajishikiza tu, lakini si kutoka moyoni. Elimu byebye..!!!
 

Hamjui tatizo lilikuja baada ya watoto wa wakubwa kuwa wanafeli hata hizo shule wakawa hawana uwezo wa kwenda kusoma. Baba zao kama akina Mungai na wengine wakaona bora wazifute nakumbuka miaka ya 1990s na mwanzoni mwa miaka ya 2000 kulikuwa na ushindani sana wa shule kama Mzumbe, Ilboru, Kibaha, T.Boys, Kilakala,Msalato,T.Girls na nyingine nyingi hata Wanagunzi walikuwa wakisoma wakiwa na mawazo ya kwenda ktk hizo shule. Lakini sikuhizi eti ukiwa unasoma St unaonekqna unaakili
 
Mkuu mbona hujataja Alharamain, Kinondon Muslim, Almuntazir, Thaqafa, Ubungo Islamic, Qiblaten, Osama high school, Kirinjiko...,???

Eti anajiita team mbowe,huku anajifucha nyuma ya udini na islamophobia,,

chama chenu kishakufa wehu nyinyi
 
Mkuu mbona hujataja Alharamain, Kinondon Muslim, Almuntazir, Thaqafa, Ubungo Islamic, Qiblaten, Osama high school, Kirinjiko...,???


Comments kama hizi zinanifanya niendelee kuamini ya kuwa CHADEMA always wako against muslim and Islam....nitawachukia Daima
 

Mazengo imerudishwaa kwa wamiliki wake wa awali kabla serikali haijaibinafsisha...sahvi ni St Johns University. ..nimesoma pale....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…