lyinga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2013
- 2,496
- 1,057
Ndugu wanajamvi,
Nimekuwa nikiumia sana kwa jinsi siasa mbovu za hii nchi yetu zilivyoingizwa kila sekta ya nchi. Nakumbuka wakati ambao tulikuwa hatujaingiliwa na mmomonyoko wa maadili kulikuwa na shule nzuri kama Ilboru,Azania,Forodhani,Tabora boys,Rungwe, na nyinginezo zilikuwa zinafanya vizuri sana.
Lakini kuanzia viongozi waanze kumiliki shule zao binafsi wametuulia elimu nzuri iliyokuwepo hapo awali, zimebaki shule za makabwela na waliokuwa nacho na hata mitaala wanayoitumia ni tofauti.
Huwa najiuliza nchi moja inawezaje kuwa na matabaka mawili ya elimu wakati njia tunayokwenda ni moja?
Nawaonea huruma watoto wa kizazi hiki kwa kuwa wanajengewa mazingira ya chuki kutokana na kuwepo na tabaka la waliokua nacho na wasiokuwa nacho.
Tunachokiona sasa kwenye nchi za wenzetu uarabuni kwa miaka ijayo yatatufika Tanzania ni nani alieiuwa elimu ya Tanzania?