Zirudi enzi za Waamuzi kutandikwa Makonde ili Kulinda soka Letu

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Nidhamu sasa imeshuka kwa waamuzi wetu licha ya maonyo na adhabu wanazopewa mara kwa mara hii yote sababu ya tamaa...hii inapelekea kudhoofisha maendeleo ya mpira wa miguu Tanzania.

Pendekezo langu ni kuwa pamoja na bodi ya ligi kuongeza kuwabana hawa waamuzi hebu sasa ile tabia ya miaka ya nyuma ya kuwaadabisha hawa waamuzi pale pale uwanjani baada ya kufanya upuuzi kama ule basi turejee huko ili kuulinda huu mchezo hadi hapo nchi itakapoingia ktk mfumo wa VAR technology bila hivyo hawataacha kusumbua hawa.

Nawasilisha.
 
Wazo zuri hata mm nilikuwa nawaza hivi ila I'm afraid vipigo hivyo vitatokea pindi refa anapowazingua Simba au Yanga tu coz ndo watu pekee wenye mashabiki,Simba/Yanga ikibebwa mashabiki wa timu pinzani wa kumpiga refa wanatokea wapi?
 
Watu wapo hata ihefu ana wafuasi ....kumbuka kipigo huwa kinaakolezwa na watu wa benchi la ufundi
 
Refa atapatikana wapi wakati akimaliza mechi FFU wanamsubiri hapo na difenda wamtoe .

Faini za TFF na kuwafungia haisaidii pia maana anapigwa faini mil 1 wakati kahongwa zaidi ya hapo.

Labda faini iwe mil 5
 
Kwani vipi mkuu,kulikoni au mshabiki wa timu gani ili tuweze kuunganisha na unachoongea...?
 
Refa atapatikana wapi wakati akimaliza mechi FFU wanamsubiri hapo na difenda wamtoe .

Faini za TFF na kuwafungia haisaidii pia maana anapigwa faini mil 1 wakati kahongwa zaidi ya hapo.

Labda faini iwe mil 5
Wapigwe tu maana hakuna namna
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…