Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts?

Thubutu!! Amekufa kizembe, anaidharau Corona kama aluvyoudharau Nkurunzinza na Corona imemuonyesha kazi. Asubiri tu Ijumaa akawe chakula cha sisimizi na minyoo tukishamfukia kwenye futi 6 chini ya ardhi
 
Mkuu tusubiri marehemu apumzishwe tuanze mjadala.

Hata huko watakuwa tayari kusoma.

Ntaongelea masuala kadhaa yanayoshabihiana na hoja na suali lako.

Ila nikupe hints tu.

Marehemu JPM aliwahi kusema kule kwenye mradi wa bwawa la umeme serikali ilikuta kuna hoteli ya kulipia dola 3000 kwa usiku mmoja!.

Pia kulikuwa na barabara ndogo za kuruka vindege vidogo vipatavyo 38 na vitalu haramu vya uwindaji 47!

Ndo maana kulikuwa na kelele za kueleza mradi huu ungeharibu mazingira.

Mimi pendekezo langu kwa serikali (nafahamu watakuwa wamefikiria) ni kuweka kambi za jeshi (JWTZ) katika maeneo yote yenye miundombinu na iwe "part of National Infrustructure Security" kwa miradi yote ya kimkakati.

Tumefanya Mererani na huko iwe ni kawaida.
 
My God, Tumaini lako ni kwa MFU.
Its a new era, Dictotor kwa sasa yuko Huko na Mungu ndio anajua yuko wapi kwa sasa
 
We Bi Dada, Hajamfikia Doctor Adlh Hitler.
Au Hujui Historia, kasome na Kuangalia Jinsi HITLER alivyozikwa
Mwisho wa siku atalala kaburini na ataoza kama Binadamu wengine
 
Huu ndio wakati wa kutekelezwa kwa bandiko hili, ndio huu. Leo Dangote kushuka mjini.

Asante kwa taarifa hii, huu ni muendelezo wa mwanzo mzuri wa Mama Samia, to restore confidence kwa investors ni hatua muhimu sana kwa investiment climate yetu.

Hongera sana rais Mama Samia for healing the nation.
Pasco
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Huoni soni kuandika haya?
 
Duh...!.
Sisi wengine wenu kuna vitu tuliuliza humu,


hatukuwahi kujibiwa ila matokeo ndio tumeshuhudia!.
P
 
  • kama itakuwa applicable retroactively kwa mikataba hii ya kinyonyaji iliyopo sasa, then Tanzania tutakuwa automatically tumevunja mikataba yote ya uwekezaji kwenye maliasili zetu!, hakuna tena kutishiwa kushitakiwa popote nje ya Tanzania, hakuna cha IICD wala cha MIGA, mambo yote sasa ni kwa sheria zetu za JMT. Huu ndio uzalendo, huu ndio uanamume, na kama hawataki kufuata sisi wenye mali tunachotaka, bora wafungashe, virago vyao na wakwende zao!.
  • But hapa naomba tuambiane ukweli, jee sisi Tanzania, tunao uwezo huo?, can we stand?. Do we have the guts and the capacity to challenge them?. Nyerere alijaribu kwenye nationalization na matokeo tunayajua, jee Magufuli atasimama na hii Magufulification na Magufulinaization yenye kila dalili za pseudo dictatorship into full dictatorship, ambazo the rule of law sio issue sana kivile?,
  • ikibidi kuzibadili sheria zetu ili zitufaidie sisi, then tunazibadili bila kujadiliana na yeyote na hata kama kuna atakayeathirika na mabadiliko haya, potelea pote, kwanza tubadili ndio tuje tukae mezani kutafuta a win win situation kwa kutumia sheria mpya!. Hili litawezekana?.
  • Kwavile wengi humu ni vijana wadago, kwa sisi wazee wa umri wangu, tunakumbuka vita ya uhujumu uchumi ya Edward Sokoine, kwanza wahujumu uchumi walikamatwa wakatiwa ndani, kisha Bunge letu likatunga sheria ya uhujumu, kisha sasa tukaitumia sheria hiyo mpya kuwahukumu wahujumu hao, kuna watu wanajua what happened to Sokoine?.
  • Kwa umasikini wetu huu, with a very poor intelligence, Tanzania do we have the ability and the capacity kum protect Magufuli ili ayatekeleze haya? Mtu asije akatafutiwa sababu akaondoshwa watu tukabaki tumeduwaa!.
  • Baada ya Sokoine kuondoshwa, wanamume walitinga mahakamani, Mahakama Kuu ilitupilia mbali kesi zote, serikali ikashindwa vibaya, na kudaiwa fidia ya mabilioni na ikatamkwa wazi kuwa sheria hiyo ni batili!.
  • Sasa tumetunga tena sheria nyingine batili!, Mtunga sheria mkuu wa sheria hii ni mwalimu wangu Prof. Kabudi aliyetufundisha kuhusu retroactive laws ni bad laws!.
  • Tanzania tunafuata mtindo wa sheria wa nchi za Jumuiya ya Madola ambayo unataka sheria iwepo kwanza ndipo ukiivunja unakuwa umetenda kosa, ili kosa lifanyike, lakini kwanza sheria iwepo kutamka jambo fulani ni kosa. Lakini kama jambo fulani wakati linafanyika halikuwa kosa, lakini huwezi kutunga sheria na kutekekezwa retroactively.
  • Naomba kuwaandaa kisaikolojia kuwa baadhi ya vipengele vya sheria hii mpya ya madini na Rasilimali za Taifa zina vipengele batili, ama soon zitarudishwa Bungeni kufumuliwa, na kurekebishwa ama ikilazimishwa kutekelezwa kwa lazima, Tanzania tunakwenda kupigwa mwereka mahamani mapema asubuhi!.
  • Lakini kama sheria hizi mpya, zitaanza kutumika kwa mikataba mipya itakayoingiwa kuanzia sasa, baada ya kuwepo kwa vipengele hivi, then Watanzania wenzangu, wala tusishangilie saana kivile, kwa sababu, tutaendelea kuibiwa kupitia mikataba mibovu iliyopo mpaka ama imalizike, ama tukae mezani ku renegotiate na wawekezaji hawa ambao baadhi yao ni wanyonyaji, wanaweza kabisa wakagoma ili kuhakikisha kuwa wame extract madini yetu yote, na gesi yote na Tanzania tukaachiwa tuu mashimo!.
  • Ili sheria hii iwe na maana ni lazima ianze kutumika kuanzia sasa ilipopitishwa, ila kwa vile sheria huwa hazi act retroactively, kwa mikataba iliyofungwa kabla ya sheria hii, inakuwa haifungwi na mabadiliko haya, wanasheria mliopo humu tusaidieni, jee vipengele hivi vipya, havivunji mikataba iliyopo inayotaka usuluhishi kwanye vyombo vya kimataifa?.
  • Jee nini hatma ya Tanzania kwenye mikataba ya kimataifa tulioridhia ikiwemo MIGA?.
  • Nini hatima ya Tanzania katika uwekezaji kupitia FDI?, wenye fedha zao kweli watakuwa tayari to take such risks?.
  • Jee tushangilie tuu, au pia tujiulize na the consequences, jee Tanzania tuna guts to stand the international pressures za mabeberu hawa, ama tunapitisha tuu sheria hizi kwa mbwembwe, lakini hatuna uwezo wala jeuri ya kuzitekeleza na ama soon kibano kikitufika, tutaufyata kwa kuzirejesha Bungeni kufumuliwa na kurekebishwa ili kuheshimu mikataba ya kinyonyaji iliyopo!, na amini usiamini, hakuna mwekezaji yoyote wa kimataifa atakubali kuja kuwekeza kwenye nchi yenye sheria za ajabu kama hizi!.
  • Ushauri wa The Best Way Forward ni Renegotiation to Reach A Win Win Situation
    Kupitisha sheria mpya kwa hati ya dharura bila ushirikishwa ni kosa, maadam tumeisha fanya kosa, kufanya kosa sii kosa, kosa kurudia kosa!. Hivyo huu ni ushauri wangu wa the best way forward kwa situation iliyopo ni kukaa mezani na wawekezaji wote tuliosaini nao mikataba kabla ya sheria hii mpya kupitishwa, kuwapigia magoti, kuwaomba wakubali kupitia upya mikataba yao katika win win situation, sisi tupate na wao wapate, hii ya kulazimishana.
  • Nawaombeni sana msishangilie na kumvimbishwa kichwa rais Magufuli kuwa tunaweza kila kitu, tuwalazimishe lazima wafuate tunachotaka sisi wenye mali, asiyetaka na afungashe, aondoke!, jee tunaweza?, tunayo jeuri hii?. Kuna watu kama Billy Gates au Dangote, akikohoa tuu, nchi zinatetemeka!, can we stand?.
  • Kitakacho Tokea
    Kitakacho tokea ni ama baadhi ya vipengele vya sheria hizi mpya vitapuuzwa, ama ili kuepuka aibu ya kupitisha sheria mbovu kwa mbwembwe, serikali itapeleka kimya kimya, marekebisho ya baadhi ya vipengele vya sheria hii, kikiwepo hicho kipengele cha arbitration, kitaondolewa ili kurejesha confidence kwa wawekezaji. Kwenye hili, time will tell, kama Nyerere na Sokoine walikuwa ni wakali ukweli ukweli, lakini walishindwa, hivyo kwenye hili la sheria kutekelezwa kwa retroactively, naowaomba mimi niwe mkweli bayana wa nafsi yangu, Mwalimu wangu Prof. Kabudi na wanasheria wake, waliotunga sheria hii kwa mtindo wa zimamoto, wamemdanganya rais Magufuli kwa kumtungia sheria yenye vipengele vya ajabu, halafu rais aka assent, then sheria hii itashindwa kutekelezwa, hivyo soon watapeleka marekebisho Bungeni na kumrudia rais a assent marekebisho hayo, na hili likitokea, naombeni hoja za bandiko hili zizingatiwe, Tanzania tutaonekana ni nchi ya ajabu, tunatunga sheria za ajabu kwa mbwembwe, tunazipitisha kwa mbwembwe, rais wetu ana zi assent kwa mbwembwe, lakini katika utekelezaji ndipo tunajikuta kumbe Bunge letu, na serikali yetu, iliyosheheni wanasheria manguli tena wengine ni waalimu wetu wa sheria wa chuo chetu kikuu cha Dar es Salaam ambao sisi tulipokuwa wanafunzi tukisomea sheria, waalimu hawa ndio waliotufundisha kuwa sheria yoyote inayotungwa kama ita act retroactively is a bad law, it's illegal, lakini leo, waalimu hawa hawa ndio wamegeuka wanasiasa na wao sasa ndio hawa wametunga illegal law, wakaipitisha, wakampelekea rais akaisaini ianze kutumika, huku wanajua fika retroactively law is illegal law kwenye jumuiya ya Madola, lakini bado wamepitisha, sasa siku ya kurejea Bungeni kuyarekebisha haya madudu yao ya kisheria, hizi sura zao wataziweka wapi?.
 
Mkuu umebeba maana halisi ya Great Thinker..

Mabandiko yako mengi yamekuja kuthibitika mbele ya safari. Walau, kwa uchungu wa shubiri
 
Bwana Mayala: haya yooooote unaweza kuyasema kwa neno moja: RULE OF LAW, i mean maneno matatu.

Ni huo ushauri mbovu, si katiba mpya. Nakumbuka wote mlishangilia hiyo sheria isiyo sheria ilipopitishwa uweje sasa mnatupa crocodile tears?
Hapa ni kukujulisha sii wote tulishangilia!.
P
 
Pascal Mayalla upo mbele ya wakati mkuu, sijui kwa nini hauonekani na mamlaka za uteuzi !
Matumaini ingekufaa taifa hili katika utumishi wa uma.

Lakini pengine ni bora kua hivyo ilivyo kwa majaliwa wa muumba kwaajili ya mada kama hizi, huwenda ingekuwa unatumikia kwingineko usingepata nafasi ya kuandika mada nzuri kama hizi.
 
Cha kushangaza wewe mayala mwandishi wa makala hii ambae unaexposure na haya maswala Kila siku upo bize. I don't get it. Sikuelewi kabisa we mzee.
Mkuu crankshaft huwa tunajitolea sana kusaidia, basi tuu!.
P
 
..jambo lingine linalompoza Mama Samia ni uoga wake kwa nchi za magharibi.
Mkuu JokaKuu , sio uoga bali ni kuzingatia ukweli mchungu kuwa mabeberu ndio wanaoendesha dunia!. JPM alikaza na kuwagomea, nini kilichompata na sasa yuko wapi?.

Hawa jamaa sio mchezo!. Niliwahi kuuliza humu

P
 
Paskali kwenye ubora wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…