Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Mkuu ukisema ifanye kazi restrospective tutashindwa kesi nyingi sana. Maana mikataba ya huko nyuma ilisainiwa chini ya sheria nyingine ya madini. Kumbuka mpaka sasa kuna kampuni kama mbili za Canada zimeshaanzisha zengwe juu ya hili. Na wewe umetoa mfano mzuri tu enzi zile za uhujumu uchumi kuwa sheria haifanyi kazi kinyume nyume. Hapa ni kukomaa na hii mikataba yote ya hovyo na iliyojaa udanganyifu .Ila kama huu wa juzi haukuzingatia hii sheria mpya ni tatizo. Lakini mimi naona kwa sababu serikali itapata mgao baada ya mchanga kuuzwa sio mbaya. Sababu kumbe hata huo mchanga ulikuwa unanunuliwa na Kampuni zingine huko nje.Sio Accacia waliokuwa wanaenda kuuchenjua tena. Pia pitia The natural wealth and resources Contract (Review and Re- negotiations of unconscionable terms) Act, 2017. Utaona namna gani hiyo mikataba ya huko nyuma inaweza kujadiliwa bungeni na kisha tukakaa mezani na wawekezaji ili kuabadili mikataba iliyokuwa ya hovyo.Mkuu Chagu, waati tunabadili sheria na kuleta sheria mpya, tayari tulikuwa na mikataba mingi kwa sheria za zamani, sasa ili tufaidike na hii sheria mpya, inabidi i act retrospectively, sasa ili hili lifanyike, lazima hao wenye migodi wawe cnsulted na wakubali, vinginevyo tunazidi kuibiwa!.
Hii mikataba ya juzi imesainiwa chini ya sheria mpya, kwenye eneo moja tuu la mikataba sheria yetu mpya inasema hivi
View attachment 1341896
Sasa tafuta kilichosainiwa ni hiki?.
Unatunga sheria ya kujimwambafy, lakini unapofika muda wa utekelezaji hiyo sheria inayohitaji umwamba kweli, kumbe wewe huna umwamba huo!, kama hivi ndivyo sheria yetu mpya inavyosema, juzi mkataba umesainiwa bila kipengele hiki kufuatwa na hivi tunavyozungumza kimeisha nyofolewa kimya kimya!.
Sheria ilisema hatutasafirisha mchanga!, tumesaini mchanga unasafirishwa!. What is the use kusaini sheria na vipengele kibao vya kimwamba, halafu unapojikuta huu umwamba hatuna, tunapeleka marekebisho kimya kimya!.
P
P