Ukana Shilungo
JF-Expert Member
- Apr 17, 2012
- 3,041
- 2,422
Upo ??? 😃😃😃🤣🤣Na nyie makamanda uchwara hamjielewi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Upo ??? 😃😃😃🤣🤣Na nyie makamanda uchwara hamjielewi.
Naona sasa nyie CHADEMA kumtaja Prof. Lipumba kwa ubaya ni ibada. Hivi wapinzani waliwahi kukubaliana jambo gani ambalo Lipumba akasaliti?
Kama unamaanisha makubaliano ya UKAWA yakupasa kuelewa Lipumba ndo muasisi wa harakati zile bali Mbowe na Maalim Seif ndo walifanya usaliti kwa kumpendelea mwana CCM Lowassa kutumia jukwaa kugombea urais tofauti na makubaliano yaliyowekwa.
Lakini yakupasa kuelewa kuwa Prof. Lipumba ndo kiongozi wa kwanza wa chama cha siasa kuweka msimamo wa kutoshiriki tena uchaguzi mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita na CHADEMA wakafuata msimamo huo. Bali kwenye uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa vyama vya upinzani vilitangaza kujiondoa na CUF pia iliondoa wagombea wake.
Unawezaje kumfananisha Lipumba na Zitto Kabwe? Hivi si Lipumba na Chama chake waliotoa msimamo wa kutoshirikiana na chama chochote ambacho kingesimamisha kada wa CCM kuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu uliopita? Hi si nyinyi CHADEMA ndo mulimuona Zitto na Maalim Seif waliomsimamisha mwana CCM Membe kuwa mgombea wa ACT wanawafaeni kushirikiana nao? Leo mnalalamika Zitto msaliti?
Acheni unaafiki! Acheni ubaya!
Kwani umelazimishwa kuungana nae?Ukiangalia muendelezo wa mateso ya Upinzani wa ukweli Tanzania hasa CHADEMA, Zitto na Chama chake hawajawahi kuguswa. Ni maneno tu lakini CCM haimgusi.
Zitto Kabwe hana ushirikiano na wapinzani. Siku zote ni SNITCH. Wapinzani wanapoelewana au kuafikiana, yeye Kama Lipumba, anakuja na mchanga na kumwaga kwenye wali. Wapinzani wanapokataa kushiriki uchaguzi wowote hadi tume, huru yeye ni wakwanza kushiriki uchaguzi. Kwa kifupi ni mbinafsi ambaye haeleweki. Zitto anatumika !
Uchaguzi ulioisha Muhambwe, wapinzani waligoma kushiriki, Yeye kashiriki. Leo Asubuhi aliitangazia dunia amegundua Kura feki na maisha yaka yako hatarini, Jioni anaipongeza CCM. Siku zote yeye anafanya vitu kinyume.
Huyu tu ni Kitengo cha CCM. Anatuadaa. Tumkatae na tukimuendekeza, kiu yetu ya TUME huru itabakia kuwa ndoto. Watanzania itabidi tumdhibiti huyu YUDA ISKARIOTI !
Dr Slaa ni mwanasiasa mzuri sanaTatizo la Chadema ya sasa imekosa ustarabu yaani siasa zao tangu aondoke Dr. Slaa zimekuwa za hasira sana badala ya hoja, Mbowe amekuwa mstarabu sana ila amezidiwa na wanaomzunguka wengi sio wastarabu, hii imepelekea wananchi wengi kuwaona chadema kama sio wazalendo hasa kipindi cha JPM kutokana na siasa zao za kupinga kila jambo.
Zito Kabwe ni mwanasiasa mzuri sana ila amekuwa haeleweki eleweki. Kuna awamu anakuwa mkali sana na hukemea na kupinga mambo mengi hata yenye manufaa kwa Taifa, ila kuna awamu ikifika ukosoaji wake unapungua utadhani yeye sio mpinzani tena.
Pamoja na kuwa Dr. Slaa yupo CCM kwa sasa ila wanachi wengi wanamuamini kwamba ndiye mpinzani wa kweli kutokana na misimamo na uzalendo wake.
Sahihi!Zitto ni mdini sana ndugu zangu. Ndiyo maana leo matpkeo yoote kayakubali bila malalamiko hasi. Leo hii hii ukibadili jina la mama akawa Adela Zittp atakataa matokeo
MkuuNa nyie makamanda uchwara hamjielewi.
Sasa unaniuliza mimi ili iweje?Mkuu
Magonjwa Mtambuka, imekuwaje kada kindakindaki mwenzio johnthebaptist siku hizi anamwelezea vibaya hayati JPM wakati alikuwa mstari wa mbele kumpamba kwa udi na uvumba hata kuhimiza serrikali nzima ihamie Dodoma, leo hii inadai Rais abaki DSM na huko DODOMA abaki makamu wa Rais na Waziri mkuu?
Unamfahamu huyu mtu, naamini ulishawahi kukutana naye sehemu mbalimbali maana mijoka ya midimu kwa sasa imegeuka majoka yenye sumu kali yanatema bila hofu
johnthebaptist, jitokeze hadharani ili kuonesha kweli wewe ni jasiri wa kukana misimamo ya zamani (If at all you have guts to punch the technical jab
Mbona unajibu kwa ukali? Hizi ni dalili za chama chenu kwenda kuparaganyika na kusambaratika muda sio mrefu maana kwa sasa mnafuata maslahi binafsi. Kwanini unajibu kwa ukali wakati unaombwa kusaidia ufafanuzi kuhusiana na utata wa mwenendo wa huyo mdau wenu?Sasa unaniuliza mimi ili iweje?
Asante sana mkuuNiliwahi kuandika humu Bwana Mdogo imani imani anaitumia ndivyo sivyo
Yeye na mwendazake wa kisiwani walikuwa na jambo
Ukisikia misimamo kama misimamo
Aliondoka cdm kuamini ni chama cha msalaba
Tumuogope Mungu bandugu
Yajayo yatawachukiza wengi
Hahahhh eti Adela....
Kwani wenyewe ukali unasemaje?Mbona unajibu kwa ukali?...
Suala la udini ni KUMSINGIZIA....Zitto ni mdini sana ndugu zangu. Ndiyo maana leo matpkeo yoote kayakubali bila malalamiko hasi. Leo hii hii ukibadili jina la mama akawa Adela Zittp atakataa matokeo
Unamaanisha wanafiki walimuhama Lipumba kwenye chama cha CUF na kwenda kujiunga na wenzao kina Zitto huko ACT? Au unamaanisha nini mkuu kwa kusema Lipumba hana chama tena?Lipumba hana tena chama mkuu