Toka mwaka 1999 Bunge limekuwa na hoja binafsi moja tu, ya Buzwagi. Toka mwaka 1995 Bunge limekuwa na Muswada binafsi mmoja ambao haujawasilishwa - sheria ya Maadilii. Mara ya mwisho Mbunge kuwasilisha muswada binafsi Bungeni ni Jenerali Ulimwengu mwaka 1995.
...Unceremoniously muswada ukaondolewa kwenye order paper siku ya kuwasilishwa baada ya kikao cha kamati ya uongozi wa wabunge wa CCM.
.... wabunge wa CCM ndio wenye uamuzi wa mwisho kwani wao ndio wengi ndio maana utume wangu kwa Taifa ni kumaliza ukiritimba wa chama kimoja bungeni - ending single party dominance
Sawa.
Hizo statistics za miswaada binafsi ni absolutely appalling.
Sasa hicho kigezo cha uwingi wa CCM ndo nina tatizo, especially kuhusiana na hivi vikao nje ya Bunge.
Ni hivi, Zitto, hiki "kikao cha kamati ya uongozi wa wabunge wa CCM" siku zote kitakuwa na wabunge wa CCM tu! Si ndio ? Hata CHADEMA ingekuwa madarakani. Sasa sidhani kama sheria inakipa chama tawala uamuzi wa miswaada gani ije bungeni ipi isije kwa kulazimisha kuipitisha kwenye hii bottleneck ya "kikao cha Kamati ya uongozi wa CCM." Utaratibu gani huo kisheria (statutory ama Standing Orders) ?
Ningependa kujua miswada binafsi inakwamishwa wapi kwa nguvu gani ?
Muswada wako wa sheria ya Maadili ulisema Marmo aliuwekea mizengwe mpaka ukafa kifo cha mende. Well, japo yeye ni Waziri wa ofisi ya Waziri Mkuu, taratibu za Bunge, lakini Marmo anapata wapi nguvu za kuamua miswaada gani iende, ipi isiende ? Executive branch haijapewa nguvu ya kuliamulia Bunge mpangilio wa kuleta miswaada! Kwa katiba ya Tanzania - najua utashtuka kusikia hii idea - lakini kwa structure ya Katiba ya Tanzania, Bunge la Tanzania ndio linatakiwa liwe executive!! Linasimamia Serikali! Linatakiwa liwe juu ya Serikali. Kwa nini mkubali mizengewe ya Serikali ?
Nitachopenda kuona mimi ni miswaada inafika Bungeni halafu inakuwa voted down na CCM halafu wananchi wanaona. Lakini mkikubali iwe inaishia ishia huko kwenye vikao na kamati za vificho vificho vya CCM wananchi hawataweza jua. Utakuja hapa utatulelezea watu 50, mia, wa Jamii Forum lakini the preponderant of the masses hawana clue kuhusu michezo ya chini chini ya CCM.
Halafu, kingine, usipokazana sana ku assert hizi rights za kisheria, kama zipo, za kufikishiwa miswaada yako bungeni unaweza kuanza kuoneka kama unatumia kisingizio tu. Kwamba, ""aaaah, nilileta muswaada wakaukataa... wao ni majority." Halafu ikawaje ? "aaaah, tunasubiri tuwe majority!" Kama ni hivyo basi the minor party hakina haja ya kuwepo Bungeni!