Binafsi mimi sikufuatilia kipindi hiki, lakini kama anasema tena on public kwamba maamuzi ya vikao yalikuwa batili huyu kijana si makini, anahitaji kumaliza matatizo yake ndani ya vikao vyao. lakini kama karudia tena kauli zake amefanya makosa makubwa, watanzania walifanya kosa sana pia kumwamini huyu dogo kama mwanamapinduzi wa kweli - nafikiri hizi njaa bado ni tatizo kubwa hasa kwa wanasiasa vijana.
Hata kama umetofautiana na viongozi wako kwa namna yoyote ni mwiko kusema mambo ya siri ya chama nje, ni sawa na kusema siri na mkeo kikojizi mbele za kadamnasi inakuwa aibu ya nani? hii ni miiko ya kisiasa. kwa nini msimalize matatizo yenu humo ndani ya chama chenu? kutuambia sisi mambo yenu ndiyo tuone wewe unaonewa?
Fuaten nyayo za wanasiasa wavumilivu, uanasiasa si kuagiza kitimoto na bia baridi jamani, kuna mifano bora mizuri ya kuiga kwa wakongwe walivyofanyiwa na chama chao
a) Mzee malechela asingekuwa mvumilivu asingekuwa hapo alipo, baada kukatwa jina lake baada ya kazi ngumu kuzunguka nchi nzima kutafuta wadhamini.
b) Mzee Salim asingekuwa mvumilivu asingekuw.a hapo alipo baada ya kusemwa yeye sijui ana damu ya uarabu......
Wapo wengi tu, Zitto ndugu yangu mimi nilifikiri hutaongea tena on Public sasa umerudia kosa tena? sasa kutembea na barua mfukoni kuna maanisha nini? office za chadema unazijua kwa nini usiipeleke? au unangoja wakuite wakuulize tuhuma zako?. We unakijua chadema vizuri hawatakuita ninachokiona kazi yako itangumu zaidi na umeanza kuisha polepole.
Unaweza kuwekwa kundi moja na Mrema usipokuwa makini nduguyangu