Zitto ajutia kuingia kwenye siasa?


Zitto hatawapa mnachotaka.
 
Zitto hatawapa mnachotaka.

Mkuu bigilankana nimesoma utetezi wako wote kwa Zitto - umejaribu sana na nakupa pongezi lakini sasa naona unaanza kuchoka. Kama umefikia kusema kuwa Zitto hatatupa tunachotaka, bila shaka sasa unakubaliana na sisi wengine kuwa kwa mwendo wake huo, hatufai. Naomba umpe ushauri mdogo tu - ukishachagua kuwa mwanasiasa yabidi utekeleze na miiko yake mojawapo ukiwa kuwapa wengi wanachotaka. Kwa kuwa hawezi kutupa tunachotaka, basi aachane na siasa na wengi tutaheshimu huo uamuzi wake. Kafulila, rafiki yake mkubwa Zitto, tayari huko NCCR alikohamia kunafuka moshi na hata miezi sita bado !
 

mnaotaka na kusukuma ahame chadema msahau hahami. keshasema mwenye nguvu katika chama huwa hahami. huko NCCR ni majungu tu ya Tanzania Daima. Habari yenyesoma ni fitna tupu. wamezoea vya kunyonga...... vya kuchinja hawaviwezi
 
Nijuavyo, muungwana ukitaka kuacha mke, unakamilisha taratibu zote kunakohusika na wanaohusika kisha unaangalia anga zingine kwa wakati wako. Sidhani kama ni sahihi kuutangazia umma ubovu wa huyo mke na kuzunguka na rasimu ya talaka ambayo unakusudia kumtwanga muda usiojulikana. Pengine ndio kama isemwavyo kwamba kwenye siasa kitu ustaarabu hakipo - ni mikakati tu!
Ugumu wa kuwasilisha hiyo barua ya kujiuzulu unatoka wapi kama kweli Mh. Zitto keshapoteza interest kwenye CHADEMA na siasa kwa ujumla? Au uongo? Ni kweli kuwa ni maisha yake (hayatuhusu) kama wasemavyo wengine, lakini ukishaingia katika public domain na kuwapa tumaini wengi kwa vipaji na ujasiri kama alivyoonyesha huyu dogo hapo nyuma, tutasema tu kuwa tumekuwa disappointed na hii anticlimax inayojitokeza sasa.
 
mnaotaka na kusukuma ahame chadema msahau hahami. keshasema mwenye nguvu katika chama huwa hahami. huko NCCR ni majungu tu ya Tanzania Daima. Habari yenyesoma ni fitna tupu. wamezoea vya kunyonga...... vya kuchinja hawaviwezi

nianze kwa kukiri kuwa mimi siyo chadema ila ninaipenda sana chadema na nipo tayari kutoa support yeyote muhimu kwa chadema. Endapo nitaamua kujiunga na chama chama hicho kitakuwa ni chadema. Lakini nakiri kuwa Zitto hafai kuwa kiongozi wa chadema kwa sasa.

Kiongozi mzuri hawezi kupinga maamuzi ya vikao halali vya chama tena ktk vyombo vya habari, vinginevyo awe amejiuzuru kwa kutokukubaliana na maamuzi ya chama. Zitto anaendeleza ajenda yake ile ile kwamba yeye pekee ndiyo kiongozi anayefaa chadema. I'm sorry to say it.
 

Collin Powel alimkubali Obama na akatangaza hadharani, uliona mahari alipokemewa na kutishia kufukuzwa na chama chake?

Juu ya maamuzi kuwa siri, nani kakuambia kuwa yalikuwa ya siri? Si Slaa alitangaza hadharani kuwa wale ni sisimizi? Hilo linastahili kupigiwa makofi siyo!!
Tatizo letu waafrika na kutoweka wazi misimamo yetu, tunacheza na mazingira ndo tunaamua.

Kukaa kimya kwa Salim kulimpa kile alichotaka? Jiulize!!
 

Nadhani mfano wa mke na chama haviendani, kama Cjadema kuna ubaya unaendelea ni vizuri tukaujua, kesho waksihika nchi tusilie! Ila kama kweli chadema ina ubaya kwa nini huyu dogo asijiuzulu badala ya kutishia tu ana barua? nauliza maswali haya kuweli wanaujua chadema na zito wao, something is wrong somewhere!


Good!

Na chama kizuri hakiwezi kubaki na kiongozi anayewapinga hadharani? kwa nini unaangalia upande mmoja??

swali ni kwa nini inakuwa hivyo?

I do think mawazo yetu tuyaelekeze kukijenga chama, sasa kama chama hakiwezi kumuondoa Zito, I doubt!!
 
Niliwahi kusema hivi mwaka jana na subirini mtaona mengine, maana jana nasikia vinara wake na wanaomuunga mkono hawajapendezwa na mahojiano yake na TBC wanadai ''kajianika'' sana

 

Here we go again!

Acha siasa kama unamjua huyo mhadihiri chuo kikuu we mtaje tu hapa, ninaowajua vibaraka wa CCM ni Mkandara, Bana, Shivji naye haeleweki kwa sasa!

Please, I beg to differ kuwa Zitto ni mtu hatari sana ndani ya chadema kiasi ambacho chadema hawawezi kumchukulia hatua!! chadema kama chama kimwogope Zitto!!!, you must be joking! acha matusi kabisa, siasa hizi kawapelekee huko huko! Pinda naye alisema kuna watu hatari sana wakiguswa nchi itatikisika let leave them!!!!! huwa nasema nataka vitu unique kutoka vyama vya upinzani, hizi statement zako kama ni kweli, basi hatuna vyama bado kwa maana na quality ya chama! Believe me kama Chadema ni chama, kiko far milion times more than any existing individual!ikiwa kinyume basi kuna tatizo!

Mwisho naomba unipe jina la mpinzani anayeishi Tanzania, asiyeifurahisha serikali-ukiacha Tundu Lisu tu na Slaa tu. japo wanaweza wakawa na madhaifu yao but they are simply great!

Swala la Zitto kujianika nilishasema tangu anarudi nchini , kuwa mkuu akwepe kabisa media hizi, nikatania na kusema nchi hii kila mtu atakuja kuwa na gazeti lake ! swala la yeye kuhojiwa na TBC ni dalili ya mtu asiyeshaurika ndio tunajua ana kihoro na uchungu wa uchaguzi, but it has gone too far, kiasi cha kuwa hatutabaki kwenye same landmark! maadam amekubali kuwa kiongozi wa chama, akubali yote! hataki aondoke, asipoondoka kuna tatizo akikosoa chama nacho kisipomchukulia hatua nacho kina tatizo! hakuna swala la uangalifu wa hali ya juu kwenye swala la Zitto!

Nilichosema huko nyuma , swala la ungalifu unaousema ni consequences za kutofanya uchaguzi, Mbowe hajui kwa namna gani anapendwa, kutoa maamuzi kwake ni ngumu ndugu!!! this is simple and clear! Siku zote inaleta raha na nguvu kufanya maamuzi ukijua kuna watu watakuwa upande wako
 
Nadhani Zitto anatafuta sababu ya kutimuliwa CHADEMA ili aweze kurejesha nafasi yake kisiasa ambayo kwa kweli ameanza kuipoteza kutokana na kauli zake tata. Mwanzono nili-sympathise naye wakati wa Mchakato wa Uchaguzi wa CHADEMA na aftermath lakini sasa ukiongeza yalosemwa kwenye magazeti hasa Mwananchi naona kama anapoteza mwelekeo.

Kitu nachowapongeza CHADEMA ni kumwangalia tu na kusubiri atakachoamua yeye Zitto na ni vema watulie na wasikurupuka kumvua Uongozi au Uanachama kama walivyowafanyia Kafulila na Juju nadhani muda si mrefu tutamsahau kama tulivyowasahahu Wanasiasa wengine waliovuma kama vile Dk Lamwai na Dk Kaborou. Hata hivyo, nahisi Zitto anaweza kuwa Msaliti mkubwa sana wa Vyama vya Upinzani baada ya kuondoka CHADEMA na navishauri vyama vingne vya Upinzani kujihadhari na Zitto hasa hao NCCR ambao nadhani wana mpango wa kumsimaisha Kafulila ambaye anaungwa mkono na Zitto kule Kigoma.
 

umejiunga na haters. maneno yako yote hayana basis na yamejengwa na matofali ya CHUKI.
CHADEMA wanamwangalia tu? kuwafukuza watu wake na kusambaza majungu ni kukaa kimya? hujui usemalo. Zitto hatoki CHADEMA na hicho chama hakimfukuzi kwani hana kosa kwa mujibu wa katiba yao. labda wasikilize watu wenye chuki kama wewe na uliojiunga nao
 

SI kweli Bigila, Nimekuwa pro Zitto na hata wakati Mwananchi wanatoa habari zake za barua anayotembea nayo nk bado sikuwaamini. Kauli zake alipohojiwa na Clouds FM niliyaheshimu sana na nikawomba wana JF waliokuwa na wasiwasi naye waheshimu kauli yake katika Clouds FM. Lakini mahojiano yake na TBC ni kama vile anafuta msimamo wake kama alivyosikika na Clouds Power B/Fast.

Siwezi kumchukia Zitto, kwanza ni home boy na misimamo yake niliiunga mkono lakini pennye ukweli ;lazima tuseme na tuna uhuru wa kutoa maoni kama yeye Zitto alivyotoa maoni yake ila ni wazi kwangu kuwa Bwana mdogo ameenda extra mile na anaongea sana sana kiasi kwamba tunashindwa kumuelewa na tunashindwa kujua anataka nini na anaelekea wapi hasa Kisiasa.
 
Re: Zitto ajutia kuingia kwenye siasa?
- Nafikiri anapswa kujutia kuwa exposed, hivi watu wanawezaje kujua kuwa kwenye briefcase yako kuna barua ya kujiuzulu, si mpaka uwe umewaambia mwenyewe, sasa wewe kweli unaweza kuaminika na siri muhimu za chama? Licha ya za taifa as kiongozi?

- Sasa what this has to do na siasa mpaka kufikia hatua ya kuijutia? I mean somebody help me sioni the connection hapa! To me humo kwenye siasa Zitto amepanda exactly anachovuna, sasa anajutia what? siasa au matendo yake yasiyofanana na siasa anayoitaka lakini haiwezi?

- I mean I am lost!

Respect.


FMEs!
 
Nakubaliana na we FMES.
Siasa is for the thick skinned.
Zitto over exposed himself katika masuala mbali mbali ingawaje atapewa a pat on the back for trying.
Masuala yaliyo muangusha ni hatima ya Tanesco na mitambo yake.
He dithered, and noticeably too.
Pengine ataelewa kuwa siasa haina huruma, no mercy kabisa.
The other wrong move is not toapologize to his constituent supportes kwa makosa aliyofanya, na kuendelea ku-propound his wrong moves, kama kuendelea kusupport indirectly knowingly or unknowingly a leaf of fisadis in the form of mitambo ya Dowans.
Mashambulizi mazito aliyoyapata Mhe Zitto mnamo mwishoni mwa mwaka 2009,humu humu JF, must have seriously shaken his resolve to go along with politics.
SOMO: politics is a dirty game, retreat to fight another day and dont stay in the limelight for too long.
 

Kwisha habari yako Zitto, huna mashiko tena
 
Zitto kasema azma yake toka mwanzo ilikuwa ni kufundisha ..
ila anajisikia uchungu sana pale anapowafikilia walioingia kwenye siasa kupitia yeye

Bado sijaelewa hiyo kauli

Kafulila amefulia kafulishwa na Zitto. Pole yeye! Ila to be honest, Tanzanians are tired of Zitto since Dowans ila nilikutetea hapa basi. You better go to Uni lakini mwanangu akija huko nitamwambia tabia zako. Mabandiko yako yote kuanzia ile Barua ya machame kwa mama yao nimeyaweka.
 
..wakati mwingine wenye matatizo ni waandishi wetu wa habari. hapa palihitajika pawe na follow up questions.

..labda angeulizwa atamsaidia in what capacity and level.

..pia angeulizwa kama atamuunga mkono na kumsaidia mgombea atakayesimamishwa na Chadema Kigoma Kusini.

NB:

..Mkapa alipowaponda hawa ndugu zetu hakuwa amekosea sana.
 
Kuhusu Zitto na mgogoro wake haswa kuhusiana na misimamo yake ndani ya chama cha chadema,matatizo yalianza mara baada ya yeye kujiunga kwenye kamati ya madini ya JK kinyume nadhani na matakwa ya chama chake....Nakumbuka mjadala ulikuwa mkali sana hapa enzi hizo jambo forum,Zitto akidai kuwa yeye ni mtu mwenye "Principle" Nilimuuliza ni kivipi maamuzi yake hayo yamfanye yeye kuwa mtu mwenye principle kwasababu kila mtu alikuwa akimwuliza ni kivipi kamati ama tume vitafanya jambo la tofauti,maana vilishaundwa vingi tu na wengi wakidai kuwa ni njia za ulaji tu.
 
Naona Waberoya na Bigilankala wamejitahidi sana kumtetea Zitto maana kila aliyetofautiana na misimamo ya Zitto wao wamekuwa wakipinga. Mimi nitawajibu kwa kifupi.

Kama Chadema wameshamuona Zitto hafai wasije wakalogwa kumfukuza wala kumshirikisha kwenye mambo nyeti ya chama waachane naye awepowepo tu kama mtu mzima atajistukia mwenyewe kuwa hatakiwi.

Waberoya anauliza hasara zitazotokea Zitto akiondoka Chadema, hasara gani mimi sioni hasara kwani Zitto amefikia umaarufu kumzidi Kabuoru, kabuoru alikuwa Kabuoru kule Kigoma hadi CCM wakamzushia si Mtanzania. Sasa huyu Zitto hata CCM wenyewe wameshadharau anajimaliza mwenyewe hawataki lawama ni kama kumpiga nyundo marehemu utanunua kesi bure kwanza ni kumpa umaarufu wa bure.

Mimi nafikiri hasara anayoisema waberoya ni kupoteza jimbo, kipi bora kupoteza jimbo au kuua chama. Kama wakimwacha aendelee kuropoka (ila wasimfukuze kuna mbinu nyingi tu za kumfanya asisikike) atakiangamiza chama kizima na kupoteza hata majimbo mengine.

Zitto ni mchanga sana kisiasa nadiriki kusema hajui siasa ni nini, mengi yamesemwa ila nitakupa mfano mmoja umelala wewe na mkeo majambazi yanaingia yanataka pesa mkeo anajiunga nayo kukushambulia sijui kesho yake mtaangalianaje na mkeo. Ni sawa na Zitto anavyotaka kuwasaidia NCCR kupitia kwa Kafulila na wewe unataka Chadema waendelee kumchekelea tu Zitto, sijui kama anajua anachotaka kukifanya kama anajua basi simuungwana (gentleman) wala si mwanasiasa ana malengo yake wala si ya kisiasa.

Waberoya unaweza kunipa sababu tatu tu unazoona kuwa Zitto ni mwanasiasa mahili au anafaa kuongoza chama cha siasa nafikiri sifa za kiongozi bora unazijua si bora kiongozi ukiacha tukio la kufukuzwa bungeni na Richmond/Dowans. Nasikia ana rekodi ya kufukuzwafukuzwa Chuo kikuu wakati akiwa Daruso ila sina data kwa hili.

Chadema waendelee na mipango yao kama kawaida Sangara mbee kwa mbele mchuzi mzito pilipili kwa mbaaaliiiiiii na kachumbari pembeni.
 

Sorry my friend you got me very very wrong!

Tatizo ninaloliona humu ni kutokujadili maada na tatizo lililopo bali mtu, na kwa sababu hiyo ndiyo unanipa cheo cha kumtetea zito!

tunachofanya hapa ni kujadili one dimension na sio mult.

Niliposema watu kujitoa katika chama ni kudhoofisha siasa ya upinzani,na huwafanya watu wasipige kura, haina maana panapobidi mtu kufukuzwa asifukuzwe! nimejadili kueleza kuwa migogoro ya hivi vyama ndiyo vinafanya watu wavidharau, consequently they dont vote! hapa sio kumtetea zito ni kueleza hali halisi!

Post namba 58,64 na 89 zilitosha kabisa kujua msimamo wangu juu ya Zito. Mimi nimeangalia kwenye chama na nimegusia kwa nini hawamfukuzi, msimamo wangu ni afukuzwe na Chadema! asipofanywa hivyo ndiyo nime raise questions why? nikaelezea ni udhaifu wa chama kutokuchukua maamuzi na sababu nimetoa!

kwa nini humu jamani mnataka woote tuwaze sawa, tuitikiane yes yes, aliye kinyume ni adui! again, umeweka maneno kwenye kinywa changu , hakuna sehemu yoyote niliyosema Zitto ni kiongozi mzuri!!! please acha hizo mkuu!

Umeeleza swala la DARUSO pengine mimi ninamfahamu vizuri Zitto kuliko nyie wote, kwani ndiye aliyetaka kuipindua serikali yangu ya DARUSO(2003-2005). kama ningekuwa nina kinyongo naye basi ningeandika ubaya hata wa kutunga na vithibitisho

Here we are discussing issues that concern our nation, issues that touches everyone. Kesho Chadema wanaweza kushika nchi, na wakifanya vibaya huwa hamchelewi kugeuka na kuanza kulaani kuwa kwa nini wanafanya hivi

There is no way you can say Zitto's problems without saying Chadema's problems. Unless hatuko serious au we are not critical analyser.


kwa nini tuwe wanafiki! Zito ana matatizo, Chadema nayo ina matatizo as a whole, kama kusema chadema ina matatizo ndiyo kumtetea Zitto, pole we!

rejea post zangu zijaona mtu akizijibu ndiyo napata wasiwasi kuwa huwa tunajadili nini humu?,au kupoteza muda siku ziende! au mpaka sasa hivi hamjagundua cancer ya chadema kupitia haya maneno ya Zitto? its seems kina individuality,makundi na hamna kufuata katiba na kanuni! this alone is serious crime!

wenye ushabiki huwa wanakosa cha kusema humu, stay as referee do not choose side , ushabiki will always make you speechless na kujipinga huwa hamuwezi.

Yes zito ana makosa ya kwenda kinyume na chama, chama kina makosa kutomchukulia hatua! nikaeleza matatizo ya Chadema ni kama ya CCM yako kwa mfano mwingine tu!

Mwisho nataka urejee tabia za chama, muundo,katiba, kanuni, operations n.k angalia chadema kama ina sifa hizo! be honesty!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…