Zitto ajutia kuingia kwenye siasa?



Naungana nawe. Wakati mwingine Waandishi wetu wa habari wanachangia mno katika kuleta mifarakano ndani ya vyama katika jitihada zao za kuuza magazeti.
Huyu amesema 'Zito Amvaa Slaa' unategemea kabisa kuwa watu hawa wawili wamekutana ofisini na kutupiana maneno lakini unasoma mpaka mwisho wa habari unaona ni mawazo ya muandishi tu ya kile anachoona yeye ni Zito kumvaa Slaa. Muandishi wa namna hii anapokutana na Mwanasiasa ambaye hachungi kauli zake lazima kutokee kutokuelewana ambako pia huchochewa moto zaidi na hao hao waandishi!
 


Mzee Waberoya imebidi nirudie post zako zote kumhusu Zitto nimeelewa msimamo wako kwamba,
-kwa mwenendo ulivyo sasa anasitahili kufukuzwa Chadema tena haraka,
-Chadema ni tatizo kwa nini wanaogopa kumfukuza,
-Hakuna demokrasia ndani ya vyama nk.

Kimsingi kuna mengi nimeyakubali lakini tunatofautiana kwenye utekelezaji wake. Nakubaliana na wewe Zitto kufukuzwa lakini kufukuzwa inategea unamfukuza nani Zitto kwa sasa is a public figure ingawa mbele ya chama wanachama wote ni sawa lakini impact ya kufukuzwa mimi mwanachama wa kawaida na Zitto inatofautiana. Kwa hiyo inatakiwa busara ya hali ya juu ndiyo maana Chadema wanachelea kutoa maamuzi na kuchelea kutoa maamuzi si kwamba wanamuogopa au kina udhaifu ni mambo ya kiufundi tu ndugu yangu. Kinaonyesha uvumilivu na ukomavu badala ya udhaifu unaousema.

Kuhusu demokrasia ndani ya vyama hakuna chama chochote duniani kinachoweza kusema kina demokrasia 100% vinatofautiana tu kwa viwango ukichunguza sana vyama vikongwe au vikubwa ndivyo vyenye viwango vya chini zaidi kuliko vile vichanga viko tayari hata kutoa roho kufanikisha matakwa yao. Kwa hiyo tusivilaumu sana hivi vyama vya upinzani bado vichanga vinajitahidi kwa kiasi chake tuvipe support, hata NCCR kuwapokea kina Kafulila si kwamba wanataka kupambana na Chadema basi tu wafanyeje wanataka na wao wasikike.

Kuhusu wenyeviti umewataja Mbowe, Mrema nk nilishasema uongozi ni kazi sana jaribu wewe kuwa hata mwenyekiti wa kwaya uone kama si kila siku wanakwaya wanatwangana makonde.

Mwisho umesema Zitto alitaka kuiangusha serikali yako ya Daruso 2003-2005 kwani tatizo lilikuwa nini hebu tumegee basi kidogo ili tumjue zaidi kwasababu ni kiongozi wetu sote. Na mimi pia nitakupeni uzoefu wangu ndani ya Daruso wakati wa kunji kubwa la 1990 hadi chuo kikafungwa mwaka mzima wanafunzi wote ilibidi turudie mwaka ukaitwa mwaka wa Mwinyi eti tumemtukana Rais matusi ya nguoni. Enzi za kumbeba Mtikila Nkhruma kusukuma gari la Mrema baada ya kumwaga sera Nkhruma nk.
 

Ok, kama ni busara kumwacha Ok,

Mbowe, Mrema, Zito, Mwakyembe,Kubenea etc kwa nyakati tofauti wametoa au kuandika statement ambazo zinaelekea kumpa sifa JK! I am against it!

Yes, Zito,Omarlysa, Ridhwan Kikwete etc, waligomea matokea ya urais, wao walikuwa wanamtaka mtu wao na sisi katika kambi yetu ya wahandisi tulisimama kuichukua Daruso, nilikuwa ndani ya chamber wakati kura zinahesabiwa, na kwakweli tulishinda.Mitazamo ya akina Zitto walijua tumebebwa na kwa sababu muda huo VC alikuwa mhandisi basi moto ukawaka.Vurugu zilikuwa kubwa kiasi cha kufungiwa ofisini na kuna wakati askari walikuja kutulinda ili tuendelee na kazi.

Baadaye walikubali tuendelee na uongozi baada ya kupewa onyo kali, na kipindi hicho Marehemu Chachage aliplay major role ya kutupatanisha kambi ya Zitto na yetu.

Kitu ambacho nitamtetea siku zote Zitto ni kuwa sijapata sababu ya wazee wa chama kumtaka asigombee uenyekiti, to me democracy hapa haipo
 

Waberoya
Sijasema wamwache nilichosema wasikurupuke kumfukuza kama wananifukuza mimi nisiye na mfusi hata mmoja yeye ana jimbo, ila kwa anachofanya sasa si u-gentleman kwa kiongozi yeyote akitaka kuondoka aondoke mwenyewe asipojitoa awepoawepo tu kama waziri asiye na wizara maalumu.

Kuhusu Mbowe, Zitto,Mrema,Kubenea, Mwakyembe kumsifia JK ni kweli ila sijui ni statement gani Mbowe aliyoitoa ila wengine zipo wazi.

Kuhusu DARUSO ndugu yangu kwa macho ya nje utasema kinatetea maslahi ya wanafunzi lakini kimegeuzwa kuwa cha kisiasa zaidi, viongozi wake wako kwenye payroll ya serikali ni kitengo cha kisiasa kama ilivyo REDET sijui kama na wewe ulikuwa kwenye hiyo payroll.

Hilo la kina Zitto kugomea matokeo ya Daruso siwezi kuthibitisha ni yupi alikuwa sahihi inawezekana waliokuwa wanalindwa na polisi ndio walikuwa na makosa sijui. Mfano huu unanipa picha kuwa Zitto yuko serious zaidi wakati hasa wa kuhesabu kura yuko tayari kwa lolote hata kama anavunja katiba mfano uchaguzi Mkuu wa UVCHADEMA mbali ya kura kuzidi wapiga kura still yeye alitaka matokeo yahalalishwe wakati yeye alitakiwa ndiye awe chachu ya kuilinda katiba.

Hivyo alivunja katiba waziwazi bado anataka wamuone kuwa anamsimamo hataki kukiri alivunja katiba aonekane anamsimamo, kweli watani zangu Waha wabishi. Huyu ndiye kiongozi tunayemtetea.
 


Unatakiwa kufahamu DARUSO imeharibika lini, na marais gani wakiwa pale huwa serious, sitambi ila viongozi wa DARUSO wengi waliotoka engineering wako serious na huwa mwiba-isipokuwa mmoja tu ambaye mpaka leo anaona aibu!!. so usicrame kuwa kila rais anapata fedha ya wakubwa

Kabla ya serikali yetu alikuwepo Rugemarila, he is the one who signed agreed with loan board watu kupewa loan kwa asilimia, serikali zetu na iliyofuata tulipinga na utekelezaji wako umekuja kuanzia 2008! wakati ulitakiwa kutekelezwa 2003!

Kingine, DARUSO ina wizara na mawaziri, they are same-like real government, kuna wengine wanaweza wakawa clean lakini wengine wakawa dirty!

binafsi, sijawa na ushahidi wa serikali nzima moja kwa moja kuwa wanalipwa fedha na serikali, ukitoa huo ushahidi utakuwa umefanya jambo la maana,

Mimi naweza kukuambia kila serikali na waziri gani alikuwa fisadi! ila siyo serikali yote, na huja kugundua baadaye, kumbuka wako mwaka mmoja tu madarakani! siyo miaka mitano!

Naona bado uko na Zitto, baada ya kura kuzidi na matokeo kutotangazwa kilifuata nini? uchaguzi wa UV/chadema ulirudiwa?? and what makes you to believe kuwa kura zilizidi? kama zilizidi unafikiri upande gani walikuwa wamefanya faulo?
 

Ni wazi kama nawe ulikuwepo katika kiongozi wa kizazi kile cha kuwatukana viongozi matusi ya nguoni, kuendekeza unyanyasaji wa Mzee Panchi na hata kuwabeba mafashisti wa aina ya Mtikila na Mzee wa Kiraracha ni wazi huwezi ukaelewa aina ya saisa ambazo zitto anajaribu kuzifuata....
 


Na huyu naye atajiita mwanademokrasia......

Chuki na UKADA FEDHULI umewajaa.....kama ilivyo kwa Ujamaa, Demokrasia pia ni IMANI na bila ya kuwa na watu wenye kuamini, kuheshimu na kutukuza UANADEMOKRASIA kwa mitazamo na vitendo ni bora tukaendela na GENGE CCM na MFUMO FISADI tuliojizoelea...
 
Kabla ya serikali yetu alikuwepo Rugemarila, he is the one who signed agreed with loan board watu kupewa loan kwa asilimia, serikali zetu na iliyofuata tulipinga na utekelezaji wako umekuja kuanzia 2008! wakati ulitakiwa kutekelezwa 2003!

Umeeleza swala la DARUSO pengine mimi ninamfahamu vizuri Zitto kuliko nyie wote, kwani ndiye aliyetaka kuipindua serikali yangu ya DARUSO(2003-2005)!

Kaka acha upotoshaji wa historia...
 
Kitu ambacho nitamtetea siku zote Zitto ni kuwa sijapata sababu ya wazee wa chama kumtaka asigombee uenyekiti, to me democracy hapa haipo

Kaka jibu lake ni rahisi tu. Kama Zitto aliamua kukubali ushawishi/maoni/shinikizo ama ushauri wa wazee hawa na akajitoa lakini wenzake wameendela kufanya haya mnayoyaona na msiyoyaona bila ya kujali hatima ya chama chao na matamanio ya watanzania waotao mabadiliko, unadhani angekataa ushauri huo na kuelekea kwenye uchaguzi wangelifanya nini?
 
Kaka acha upotoshaji wa historia...

oK, Acha nipitie tena makarabrasha yangu ya historia tena


Chadema is dead! from he first day Mtei aliposema na waandishi wa habari kuwa kuna watu wamepewa hela na CCM kuharibu uchaguzi. That statement ilichukuliwa kwa mitazamo tofauti, lakini ndani ya chama ilionekana kama Zito msaliti. walifanya hivyo makusudi kuharibu jina la Zito na influence yake, very same people wakampa unaibu katibu mkuu, mtu ambaye viongozi wamemfanya mpaka mwanachama wa kawaida amwangalie Zito kama msaliti!

It is hard and believe I can feel the pain that Zito is bearing, kuwa kiongozi ndani ya cham chako at the same time kuwa excommunicated from that very same group is not easy to live with!

I have lots of friend who have lost their faith on Chadema, as I speak today, Chadema is not the same, and I will not stand to see the very same Chama I loved most doing things that are exactly the same as CCM.

Nitakuwa najidanganya kuwa kuindoa CCM ni lazima kije chama chochote hata kama ni hiki cha wabakaji wa demokrasia! Kama kuzungumza ukweli ni vibaya basi I do doubt watanzania wengi tuna double standard na hii ndiyo imetufanya tuwe hapa, we dont want to call things by their names!

Chadema wamecover ishu ya uchaguzi iliyopita kana kwama nothing happened, kesho very same chama kinaweza kushika nchi na kukataa kufanya uchaguzi wa kitaifa, it will be too late, Kenya wametufundisha..
 
Waberoya

ila sijui ni statement gani Mbowe aliyoitoa ila wengine zipo wazi.

.

.

Mbowe alisema JK avunje baraza la mawaziri! aunde baraza jipya, this is worse statement to be made by chairman in opposition party in the entire 2009

Kuwa JK ni msafi na hana tatizo lolote , ila watendaji wake ndio wana matatizo!
kwani hili haukusikia??

statement zinazofanana na hizo ni ya mwakyembe, mrema, Kubenea yeye kila toleo kama sikosei naandika kwa nakshi na big hidden agenda. Zitto alisema yeye ana admire tolerance ya JK, sikuipenda hii statement maana sitaki any relation ya wapinzani na CCM!

haujajibu maswali yangu ya kuhusu uchaguzi wa UV/Chadema, kuwa baada ya matokeo kuttangzwa nini kilifuata?
 

Ni wazi kuwa yaliyotokea na yanayoendelea kutokea CHADEMA, tunayoyasoma na kuyasikia katika vyombo vya habari na ambayo hatuyasomi wala kuyasikia, yameathiri momentum iliyokuwepo ambayo ilikuwa mtaji mkubwa wa mafanikio katika uchaguzi wa mwaka huu. Hata hivyo nadhani ni mapema mno kusema kuwa CHADEMA kimekufa. Kumbuka kuwa katika vyama vya upinzani ni CHADEMA na CUF kimeweza kujijenga kiasasi katika miaka ya karibuni. Tatizo linakuja pale asasi hizo zinapotumika kwa maslahi binafsi ya baadhi ya viongozi. CHADEMA inaweza kudorora kwa sasa na kama hawajafanya juhudi ya kuangalia makosa yao kama CHAMA na sio kukimbilia kutafuta wachawi miongoni mwao ama nje yao itaweza kurudi nyuma hata kuliko ilivyokuwa 2005 lakin sio kufa kama CHAMA.



It is hard and believe I can feel the pain that Zito is bearing, kuwa kiongozi ndani ya cham chako at the same time kuwa excommunicated from that very same group is not easy to live with!
Naamin yote hayo ni blessing in disguise kwani yanaendelea kumjenga kama kiongozi na kumpa nafasi ya kufanya self reflection kwake kama kiongozi wa chama kinachopaswa kuwa tofauti na CCM na chenye jukumu la kujenga taifa la kidemokrasia, kitu ambacho amekuwa akikifanya sana.

I have lots of friend who have lost their faith on Chadema, as I speak today, Chadema is not the same, and I will not stand to see the very same Chama I loved most doing things that are exactly the same as CCM.
Ni wazi mpo wengi sana.....msikate tamaa. Nafasi bado ipo ya kukirudisha kwenye mstari na haswa umuhimu wa kuwa waumini wa kweli wa DEMOKRASIA na MAENDELEO yenye kujali TANZANIA zaidi kuliko personal ambitions na UKADA FEDHULI unaojijenga
 

Unaweza ukatujuza? Omar tatizo langu mimi na Zitto ni KUROPOKA kwenye vyombo vya habari kwa maamuzi ya vikao halali. Wewe unaona sawa? Mbona Mbowe na Slaa wako kimya? Ingesaidia pia.

Nisaidie kuhusu hili, wengi hatujui yanayotokea humo CHADEMA. Zaidi ya Kafulila na Danda kuvuliwa nyadhifa?
 
Chadema is dead! from he first day Mtei aliposema na waandishi wa habari kuwa kuna watu wamepewa hela na CCM kuharibu uchaguzi

Is this a closed conclusion or an open conclusion which need some clarifications.
 
I have lots of friend who have lost their faith on Chadema, as I speak today, Chadema is not the same, and I will not stand to see the very same Chama I loved most doing things that are exactly the same as CCM.

As many as those who have lost faith on Zitto
 
Nina maswali

Kabla ya Kafulila kijivua Uanachama wa CHADEMA, je nini ilikuwa mipango ya CHADEMA? kusimamisha mgombea Kigoma Kusini au Kuunga mkono NCCR-Mageuzi?
 

Nina maswali
Kabla ya Kafulila kijivua Uanachama wa CHADEMA, je nini ilikuwa mipango ya CHADEMA? kusimamisha mgombea Kigoma Kusini au Kuunga mkono NCCR-Mageuzi?

Ni maswali mazuri na muhimu kujibiwa. Hata hivyo nachelea kuyajibu kwani nitaishia kuambiwa ama nami "naropokwa" mambo yao ama naongea kwa niaba ya Zitto kitu ambacho daima sio kweli.

Jana niliangalia majibu ya Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema akiongelea kuhusu msimamo wa Zitto. Kwa kweli nadhani wengi wanapaswa kumsikiliza na CHADEMA wanahitaji kujifunza kutoka kwake.

Ni wazi kuwa kama ilivyo CCM hata CHADEMA na vyama vingine vilivyopo bado kuna tatizo la kukubali, kuthamini na kuheshimu misingi ya UANADEMOKRASIA. Huwezi kupigania DEMOKRASIA bila ya wewe kama mtu binafsi ama kama asasi kujijengea UTAMADUNI wa KIDEMOKRASIA….

Wengi tunatumia dhana ya Demokrasia kama njia tu ya kufanikisha matamanio yetu kisiasa na hata kiuchumi na sio kuwa tu waumini wa kweli wa DEMOKRASIA...Hili ni tatizo kubwa ambalo sisi kizazi cha baada ya mwalimu tunapaswa kulitatua kama kweli tunataka kujenga Tanzania njema iliyo tofauti na hii tuliyonayo sasa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…