Zitto ajutia kuingia kwenye siasa?

Zitto ajutia kuingia kwenye siasa?

Ni maswali mazuri na muhimu kujibiwa. Hata hivyo nachelea kuyajibu kwani nitaishia kuambiwa ama nami “naropokwa” mambo yao ama naongea kwa niaba ya Zitto kitu ambacho daima sio kweli.

Jana niliangalia majibu ya Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema akiongelea kuhusu msimamo wa Zitto. Kwa kweli nadhani wengi wanapaswa kumsikiliza na CHADEMA wanahitaji kujifunza kutoka kwake.

Ni wazi kuwa kama ilivyo CCM hata CHADEMA na vyama vingine vilivyopo bado kuna tatizo la kukubali, kuthamini na kuheshimu misingi ya UANADEMOKRASIA. Huwezi kupigania DEMOKRASIA bila ya wewe kama mtu binafsi ama kama asasi kujijengea UTAMADUNI wa KIDEMOKRASIA….

Wengi tunatumia dhana ya Demokrasia kama njia tu ya kufanikisha matamanio yetu kisiasa na hata kiuchumi na sio kuwa tu waumini wa kweli wa DEMOKRASIA...Hili ni tatizo kubwa ambalo sisi kizazi cha baada ya mwalimu tunapaswa kulitatua kama kweli tunataka kujenga Tanzania njema iliyo tofauti na hii tuliyonayo sasa..

Mkuu Omar Asante kwa Angalizo lako, binafsi nachelea kutoacomment zangu unless Swali langu limejibiwa na the good thing swala liko open kwa yeyote yule

Nini ulikuwa mpango wa CHADEMA Kigoma Kusini kabla Kafulila hajajivua Uanachama na kwenda NCCR-Mageuzi?

Nitafurahi kama nitajibiwa tunahitaji kuufanya huu mjadala uwe wenye afya zaidi kuliko Ushabiki. Maana tusipoangalia mjadala utatekwa na Mashabiki wa CHADEMA kwa upande mmoja na Mashabiki wa Zitto kwa Upande Mwingine

Asante
 
Mkuu Omar Asante kwa Angalizo lako, binafsi nachelea kutoacomment zangu unless Swali langu limejibiwa na the good thing swala liko open kwa yeyote yule

Nini ulikuwa mpango wa CHADEMA Kigoma Kusini kabla Kafulila hajajivua Uanachama na kwenda NCCR-Mageuzi?

Nitafurahi kama nitajibiwa tunahitaji kuufanya huu mjadala uwe wenye afya zaidi kuliko Ushabiki. Maana tusipoangalia mjadala utatekwa na Mashabiki wa CHADEMA kwa upande mmoja na Mashabiki wa Zitto kwa Upande Mwingine

Asante

I like this idea; pia the very same question unaweza ukauliza kwenye thread ile ya Slaa, ambayo Lunyungu ameianzisha ili tupate mwanga wa haya mambo, you know our judgment are based on what we hear from these sides, na bado inaonekana kuna vitu vingi vinafichwa au havijulikani

Kafulila kwenda NCCR kwa style ya kuisema vibaya Chadema I hate that to death, how can you stay in the party for longtime silently leo unakurupuka wanakuonea! kuna greedy ya uongozi ya Kafulila which I hate,
 
Ok, kama ni busara kumwacha Ok,

Mbowe, Mrema, Zito, Mwakyembe,Kubenea etc kwa nyakati tofauti wametoa au kuandika statement ambazo zinaelekea kumpa sifa JK! I am against it!

Yes, Zito,Omarlysa, Ridhwan Kikwete etc, waligomea matokea ya urais, wao walikuwa wanamtaka mtu wao na sisi katika kambi yetu ya wahandisi tulisimama kuichukua Daruso, nilikuwa ndani ya chamber wakati kura zinahesabiwa, na kwakweli tulishinda.Mitazamo ya akina Zitto walijua tumebebwa na kwa sababu muda huo VC alikuwa mhandisi basi moto ukawaka.Vurugu zilikuwa kubwa kiasi cha kufungiwa ofisini na kuna wakati askari walikuja kutulinda ili tuendelee na kazi.

Baadaye walikubali tuendelee na uongozi baada ya kupewa onyo kali, na kipindi hicho Marehemu Chachage aliplay major role ya kutupatanisha kambi ya Zitto na yetu.

Kitu ambacho nitamtetea siku zote Zitto ni kuwa sijapata sababu ya wazee wa chama kumtaka asigombee uenyekiti, to me democracy hapa haipo

kumbu kumbu zako hazina tofauti na za samaki,sasa kama mtu anakiri mwenyewe kuwa siasa siyo chaguo lake halafu leo umpe uwenyekiti unategemea hicho chama atakipeleka wapi,kilaza we
 
vyovyote vile, lakini mimi nasema mtu mnafiki ktk mageuzi hatufai,tunataka wanamageuzi wa kweli kutoka ktk roho zao, na siyo dizaini ya akina zito,ni hatari kwa mustakabali wa vyama pinzani,amenitoka moja kwa moja siwezi kumwamini tena daima
 
Mkuu Omar Asante kwa Angalizo lako, binafsi nachelea kutoacomment zangu unless Swali langu limejibiwa na the good thing swala liko open kwa yeyote yule

Nini ulikuwa mpango wa CHADEMA Kigoma Kusini kabla Kafulila hajajivua Uanachama na kwenda NCCR-Mageuzi?

Nitafurahi kama nitajibiwa tunahitaji kuufanya huu mjadala uwe wenye afya zaidi kuliko Ushabiki. Maana tusipoangalia mjadala utatekwa na Mashabiki wa CHADEMA kwa upande mmoja na Mashabiki wa Zitto kwa Upande Mwingine

Asante


Mpango wa CHADEMA ulikuwa na bado ni kusimamisha mgombea katika jimbo hilo. Kugawa fomu kwa wagombea na kufanya kura za maoni za uteuzi. Wagombea hakuwa kafulila peke yake, alikuwa kwa pia Muslim Hassanal ambaye aligombea pia mwaka 2005. Wote hawa walitakiwa wakijenge chama na baadaye apatikane mgombea mmoja kwenye kura za maoni. Naamini CHADEMA wataendelea na utaratibu huo wa kidemokrasia hata baada ya Kafulila kukimbia chama.

serayamajimbo
 
kumbu kumbu zako hazina tofauti na za samaki,sasa kama mtu anakiri mwenyewe kuwa siasa siyo chaguo lake halafu leo umpe uwenyekiti unategemea hicho chama atakipeleka wapi,kilaza we

Mkuu umekosea kuandika au? kwa nini unasema kumbukumbu zangu ni sawa na za samaki? kwani kipindi anagombea uongozi alishareveal kuwa siasa ni chaguo lake la pili? mwisho ni mwanasiasa gani unayemfahamu wewe ambaye siasa was/is his first priority? kuna professional inaitwa siasa? JKN mwenyewe alikuwa mwalimu.

Please watch your language, watu 8000 waliomo humu huwa hawatukani, tunaheshimu kila wazo la mtu hata kama baya kabisa, the best way ni kujibu hoja kwa hoja, lugha uliyotumia hapo si ya busara.Just imagine na mimi ningeanza kukujibu kwa kashfa , tusi n.k!

Sijajua rate yako ya kuja kwenye forums, ila I am sending this very message to your PM mail.
 
Mpango wa CHADEMA ulikuwa na bado ni kusimamisha mgombea katika jimbo hilo. Kugawa fomu kwa wagombea na kufanya kura za maoni za uteuzi. Wagombea hakuwa kafulila peke yake, alikuwa kwa pia Muslim Hassanal ambaye aligombea pia mwaka 2005. Wote hawa walitakiwa wakijenge chama na baadaye apatikane mgombea mmoja kwenye kura za maoni. Naamini CHADEMA wataendelea na utaratibu huo wa kidemokrasia hata baada ya Kafulila kukimbia chama.

serayamajimbo

Asante sana Sera ya Majimbo nadhani ni vyema mjadala ukajikita hapo
 
11 January 2010

Ndugu Wanabidii,
Wiki iliyopita kulikuwa na mjadala hapa Wanabidii kuhusu haja ya kutenganisha uchaguzi wa Rais na Wabunge. Mada ambayo ilichangiwa na watu wengi ikiwemo mimi binafsi. Ninaamini ni mada nzuri kabisa ambayo aliyeileta alikuwa na nia njema kwa nchi yetu na sisi wachangiaji tulichangia kwa nia njema kabisa.
Nilitahadharisha katika mada ile kuwa tatizo la mijadala kama ile ni kwamba ni rahisi watu kuhama kutoka katika hoja na kujadili watu. Hicho ndicho kilichotokea.
Gazeti la Tanzania Daima la Leo Jumatatu limeandika habari kuwa mimi ninataka JK aongezewe muda wa Urais. Chanzo cha habari hii ni mjadala wa humu katika wanabidii. Tanzania Daima ina waandishi na wahariri ambao tunafahamiana na wana mawasiliano nami. Hawakuthubutu kupata maoni yangu katika habari ile.Hii ni kinyume kabisa na maadili ya uandishi wa habari na kwa vyovyote vile, kulingana na hali ya kisiasa ilivyo nchini hivi sasa, habari ile ina nia mbaya kwangu binafsi kama Zitto na kama Mbunge na Kiongozi wa CHADEMA.
Nimezungumza na Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima Ndugu Kibanda ambaye naye ni MwanaBidii kumweleza masikitiko yangu. Naye pia amesikitishwa na habari iliyotolewa na gazeti lake yenye kichwa cha habari Zitto: JK aongezewe Muda
Nimemwomba waniombe radhi kwa habari hii. Mara yangu ya kwanza kutaka Tanzania Daima kufanya hivi hata kama huko nyuma wamewahi kuandika habari ambazo hazina ukweli wa kutosha. Kwa hili la leo nimeshindwa kuvumilia kwani habari ile itanijengea hisia mbaya mbele ya wananchi na wanachama wa chama changu.
Mimi napenda sana mijadala. Mijadala ni afya kwa Taifa. Licha ya mara kwa mara kunukuliwa ndivyo sivyo katika mijadala kadhaa bado sikusita kutoa maoni yangu juu ya mambo mbalimbali yanayohusu nchi yetu. Nimekuwa nikikataa ushauri wa watu wengi sana kuwa nisichangie katika mijadala kama humu Wanabidii au hata JF. Hata hivyo, nikiwa muumini wa mijadala yenye afya na vile vile katika hali ya kusahihisha masuala fulani fulani au kuweka rekodi sawa nimejikuta nikiingia katika mijadala.
Sasa, naona ni vema nichukue ushauri wa watu na vile vile kufuata hisia zangu binafsi. Ninaomba niondolewe katika orodha ya Wanabidii na sitachangia tena katika Jukwaa hili. Nimechukua uamuzi huu kwa moyo mzito sana. Nitawakosa sana. Wenye nia mbaya kisiasa, ambao sasa naamini wamedhamiria kutekeleza nia zao hizo nao watanikosa naamini.
Kwa herini na kila la kheri.
Zitto,
Hamburg.
 
na Mobini Sarya: Tanzania Daima

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA) amependekeza Rais Jakaya Kikwete aongezewe muda wa kutawala baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba.
Zitto ambaye katika siku za hivi karibuni amekuwa gumzo katika vyombo vya habari, ametoa msimamo huo katika mjadala unaoendelea katika tovuti ya wasomaji ya Wanabidii akisema rais atakayeingia madarakani aongezewe muda na kuwa miaka sita badala ya mitano.
Aidha, Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA amependekeza pia wabunge wapunguziwe muda wa kuongoza kutoka miaka mitano na kuwa minne.
Mbunge huyo amefikia hatua hiyo akijenga hoja kuwa kufanya hivyo kutasaidia kutofautisha mihimili miwili ya Bunge na Rais kufanya uchaguzi kwa wakati mmoja.
“Tunaweza kuwa na utaratibu ambao mfano 2014 tunafanya uchaguzi wa Vijiji, Mitaa na Madiwani. 2015 Uchaguzi Mkuu wa Wabunge na 2016 Uchaguzi Mkuu wa Rais. Hivyo tunaweza kusema kuwa tunaanzia watakaochaguliwa mwaka 2010,” alisema Zitto ambaye hivi karibuni alitangaza kugombea tena ubunge.
Aliongeza kuwa: “Ukishakuwa na daftari la kudumu la wapiga kura na Tume Huru ya Uchaguzi gharama za uchaguzi huwa haziwi kubwa sana kama iwapo hakuna daftari na Tume ya Uchaguzi mbovu kujaribu kupata fedha nyingi wawezavyo.
“Chaguzi za madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa zinaweza kabisa kuendeshwa na kamati huru za uchaguzi katika ngazi za wilaya. Tatizo hatuna uaminifu katika masuala haya na ndiyo maana hata huu uchaguzi wa mitaa tumetaka usimamiwa na tume.
“Tatizo kubwa katika taifa letu hatuna mijadala ya kina na yenye kufika mwisho kuhusu masuala yenye masilahi kwa taifa kwa ujumla wake.
“Mjadala kama huu Tanzania nina mashaka hautakuwa na tija, kwani Watanzania huwa tunajikuta tunajadili watu badala ya masuala.”
Alisema hoja hiyo itakuwa na maana iwapo itajadiliwa kwa mapana na kusema kwamba nchi kadhaa duniani zenye kufuata mfumo kama wa kwetu, mchanyato wa Rais na Waziri Mkuu mwenye madaraka madogo, wametenganisha uchaguzi wa rais na wabunge.
“Wenzetu rais anakaa madarakani miaka saba na anaweza kuoongoza mara moja na Bunge miaka mitano, hivyo hakuna kipindi ambacho kimoja kati ya Bunge na Urais havipo,” alisema Zitto.
Alieleza kuwa mfumo huo unatumika kwa nchi nyingi zilizokuwa chini ya Mfaransa na kuongeza kuwa nchini Marekani useneta ni miaka sita, ubunge miaka miwili na urais miaka minne.
Alisema kwa mfumo huo, katika uchaguzi nusu ya maseneta ndio huingia katika uchaguzi, hivyo taasisi za taifa kuwepo muda wote licha ya kwamba kuna uchaguzi.
“Kila baada ya miaka miwili kuna uchaguzi Marekani ama wa wabunge, au rais au maseneta. Mwaka 2008 katika uchaguzi mkuu wao walichagua nusu ya seneti na rais. Mwaka 2006 wakati Democrats walipochukua Bunge na Pelosi kuwa Spika hapakuwa na uchaguzi wa urais,” alisema.
Hata hivyo, mbunge huyo alieleza wasiwasi wake kuwa mjadala kama huo nchini hautakuwa na tija, kwani Watanzania hupenda kujadili watu na si masuala.
Alisema hoja kama hii ni rahisi sana kwa wanasiasa kuonyesha kana kwamba ama wanataka wabunge waongezewe muda au Rais Kikwete aongezewe muda.
“Hii ni hoja nyeti sana katika kulinda demokrasia ya vyama vingi na katika kuhakikisha nyakati za uchaguzi taifa halitetereki, kwani asasi za dola 2/3 zinakuwapo. “Wanasayansi ya siasa wanaweza kutusaidia faida na hasara za mfumo ambao tunaujadili na tukafanya mjadala huu mpaka mwisho na kutoa ripoti maalumu ya Wanabidii kwa umma na mamlaka husika. Labda tunaweza kuwa chachu ya marekebisho ya mfumo wetu wa uchaguzi,” alisema Zitto.
 
Zitto Kabwe amekwisha kanusha katakata kwenye mtandao wa unabii kuwa habari hii ni kampeni ya kumchafua! Amekwisha waelekeza waliondika habari hii kumwomba radhi. Habari hii haina uzito wowote na sio maoni yake ila hila za kimharibia na kumwangusha Zitto. Habari haini tija wala mantiki kujadili uongo na propaganda!
 
Will the real Zitto Kabwe please stand up!!

Hivi karibuni kulizuka mjadala kwenye forum ya Wanabidii kuhusu hoja ya kutenganisha uchaguzi wa urais na wabunge. Maada ambayo ilichangiwa na watu wengi akiwemo Zitto mwenyewe, mhariri wa gazeti la Tanzania Daima (Absalom Kibanda), Managing Editor, The Gurdian on suday (Richard Mgamba); na Excecutive Editor, Tanzania Media Women's Association (TAMWA)-- Ananilea Nkya.

Katika kuchangia mada hiyo, Zitto alikurupuka (a rookie mistake), na kutoa mifano mbalimbali ikiwemo Rwanda ambapo rais anakaa madarakani miaka 7 na wabunge miaka 5. Akaenda mbali kidogo na kutoa mifano ya nchi za dunia ya kwanza kama vile marekani ambapo rais anakaa madarakani miaka 4, maseneta miaka 6, na members of congress (wabunge) miaka 2. Kwenye hitimisho la mjadala, Zitto akesema (kwa ki-inglish), nami namnukuu, " I would go for 6 years Urais and 4 years Ubunge.

Siku iliyofuata, gazeti la Tanzania Daima likaandika habari kulingano na alichokisema Zitto kichwa cha habari kikisomeka, "Zitto: JK aongezewe Muda".

Baada ya hapo, Zitto na wafuasi wake (Wanabidii); Richard Mgamba, pamoja na Ananilea Nkya wakaanza kumshambulia mhariri wa Tanzania Daima ndugu Absalom Kibanda huku wakidai gazeti lake (Tanzania Daima) limuombe radhi Zitto. Kwa ushujaa wa pekee, ndugu Kibanda akajbu na kusema, [hell no!]--"hatutarajii kufanya hivyo!"

Kama Mwanabidii and Chief Excutive Officer wa BongoTz group, sikuona kama ni vema nikae kimya. Hivyo nikaingia na kutoa maoni yangu. Nikaandika na kusema, "Binafsi naona kama wanabidii mmekurupuka kwa hisia za ghafla na kuanza kumshambulia ndugu Kibanda wa Tanzania Daima bila hata kukaa chini na kujiuliza swali la msingi: Kwamba, kwanini Zitto anajaribu ku-push uchaguzi wa Rais uwe miaka 6 na wabunge miaka 4? Yes, baada ya miaka sita (2016) Zitto atakuwa na miaka 40--moja ya sifa anazopaswa kuwanazo mgombea yoyote wa urais nchini. Can't you guys see that he [Zitto himself] created this whole conspiracy storm? Kibanda hakukosea kabisa ku-point out hii conspiracy! And I think wanabidii mnakosea katika hili... Binafsi sioni haja ya kuiga nchi za dunia ya kwanza (Ufaransa na Marekani) ambazo huendesha chaguzi zao za urais/bunge katika vipindi tofauti. Bear in mind kwamba nchi yetu ni masikini sana na uchaguzi una gharama zake. Nchi nyigi za dunia ya kwanza zina kiburi cha kuendesha chaguzi zao kwa nyakati tofauti kwasababu resources za kufanya hivyo zipo. Plus, nchi yetu bado haijabobea hata kidogo katika teknolojia ya kisasa ukilinganisha na nchi ambazo Zitto amezitaja kama mfano wa kuigwa kwenye piece[makala] yake. Chukulia kwa mfano Marekani. Wamarrkani most of the time wanatumia "Electronic Voting Machines" ambazo zinafanya zoezi zima la uchaguzi liwe rahisi/effeciency of voting & results declaration...and also it is cost-effective, too. Kama kweli Zitto ana pure intention ya kutaka kurekebisha mfumo wetu wa uchaguzi, kwanini asipendekeze miaka 4 kwa urais na miaka 6 kwa wabunge. Why 6 yrs for presidency? The answer is simple, he'll be 40 by 2016. Oh, well maybe I am a conspiracist, too... But, my name is Gustanza, The Great and I love my country!" Mwisho wa kunukuu nilichoandika.

Baada ya hapo watu wengi wakakasirika na kutaka mjadala huu ufungwe kwasababu eti sisi tulio wachache hatukukubaliana na matakwa ya walio wengi (wafuasi wa Zitto).

Labda nimnukuu Mwanabidii, Jovias Mwesiga, aliyechangia hoja hiyo pia na kuweka hoja zetu (tulio wachache/tuliopinga hoja ya Zitto) katika maneno matamu yafuatayo, "...kwa demokrasia iliyopana si dhambi mtu kutofautiana na mawazo na uongozi wake kimawazo ilimradi havunji taratibu za chama chake...Tumezoea sana mambo ya kiimra imra ndo maana hata kwenye CCM ikitokea mtu akaongelea vitu vinavyogusa interest za nchi huku serikali ikiwa imeboronga utasikia huyu si mwenzetu mara huyu ananiambaya. Nani kakuambia mtu ukiwa kiongozi wa ngazi za juu wa chama ni mtakatifu na [eti] unaloliamini wewe ni sahihi? ...Colin Powel alimsupport Obama sijasikia nyumba yake kitiwa moto wala kufukuzwa Republican sasa ngoja Zitto akutane na Chiligati bar wanunuliane bia mbili tatu kesho utasikia anataka kuamia CCM. Lazima tufikie mahala tukomae kifikra."

Yes, Wanabidii inabidi mfike mahara mkomae kifikra. Msikurupuke kutetea hoja zisizo na kichwa wala miguuu eti tu kwasababu kasema Zitto. Acheni kuongozwa na hisia. Rather, use facts and evidence to support your arguments/claims.

Mungu ibariki Tanzania!
 
Kwa hili mnamuonea Zitto. Alitoa maoni yake na mtizamo wake katika suala zima la viongozi wa ngazi mbalimbali Tanzania. Alikwenda mbali na kutoa maelezo kwanini anadhani mfumo huo unafaa. Swala la msingi ni kugonganisha mawazo na hatimaye kufikia mwisho mzuri.

Inaonekana sasa kuwa Zitto popote hatakiwi kutoa maoni yake kama Mtanzania? Kwa hili hamumtendei haki, na baada ya kuisoma posti yake kwenye mtandao wa mwanabidii.
 
Katika kuchangia mada hiyo, Zitto alikurupuka (a rookie mistake), na kutoa mifano mbalimbali ikiwemo Rwanda ambapo rais anakaa madarakani miaka 7 na wabunge miaka 5. Akaenda mbali kidogo na kutoa mifano ya nchi za dunia ya kwanza kama vile marekani ambapo rais anakaa madarakani miaka 4, maseneta miaka 6, na members of congress (wabunge) miaka 2. Kwenye hitimisho la mjadala, Zitto akesema (kwa ki-inglish), nami namnukuu, " I would go for 6 years Urais and 4 years Ubunge.

Labda tufute kwanza neno kukurupuka kwenye paragraph hapo juu, au ulikuwa na maana ya hakujiandaa au alipoitolea si mahala pake, then niseme.

Kama sikosei alisema msingi mkuu wa hoja yake ni kuona angalau wakati wa uchaguzi tuwe na mihimili miwili inabaki, kutenganisha uchaguzi wa rais na bunge kama tunakuwa na uchaguzi wa wabunge Serikali na Mahakama zina kuwepo tukiwa na uchaguzi wa rais, Bunge na Mahakama zinakuwepo mimi naona si wazo baya, labda ubaya utajitokeza kwenye gharama.
Sijui aliposema uchaguzi wa rais uwe baada ya miaka 6 na ubunge baada ya miaka 5 alikuwa na maana kuwa mwaka 2016 kwa vile atakuwa na 40yrs atagombea urais nashindwa kuamini hilo. Tuijadili hoja yenyewe na si Zitto maana kuna wengi tu watakuwa na 40 wakati huo.

Kama hoja ndio hiyo mimi nafikiri badala ya kuwa na vipindi vya miaka 6-6 kwa urais tubaki na huu wa 5-5 na ubunge uleule wa 5-5 ila kama hoja ni kutenganisha basi aidha tukubaliane mwaka fulani wa uchaguzi si lazima huu au uchaguzi wa ubunge uahilishwe mwakammoja au wa urais uahilishwe mwaka mmoja vipishane lakini tubaki na vipindi vile vile vya miaka mitano i.e ubunge 2010,2015.... urais 2011, 2016.. au kinyume chake.
 
Zitto Kabwe amekwisha kanusha katakata kwenye mtandao wa unabii kuwa habari hii ni kampeni ya kumchafua! Amekwisha waelekeza waliondika habari hii kumwomba radhi. Habari hii haina uzito wowote na sio maoni yake ila hila za kimharibia na kumwangusha Zitto. Habari haini tija wala mantiki kujadili uongo na propaganda!

mtandao gani tena huu?
 
Labda tufute kwanza neno kukurupuka kwenye paragraph hapo juu, au ulikuwa na maana ya hakujiandaa au alipoitolea si mahala pake, then niseme...

Mkuu, I respectfully disagree with you on that! Zitto amekurupuka. Period. Mwanasisasa kama yeye anapaswa kujua kuwa kila neno analolisema/andika litaafsiriwa vingine. So alitakiwa kutulia, apime maneno yake kabla ya kukurupuka na kusema, " he's for 6 yrs kwa urais and 4 kwa wabunge."
 
Mimi binafsi sijaona tazizo la Zitto hapa kusema uchaguzi wa rais na wabunge utenganishwe, kweli huwa natofautiana naye kwa masuala mbalimbali kama kupinga hadharani maamuzi ya vikao vya chama ambapo yeye ni kiongozi lakini kwa hili yuko huru kabisa kutoa maoni yake ambayo kimsingi bado nayaona yana mantiki.

Ila kama kweli alitamka JK aongezewe muda that is the issue people might judge him differently ajifunze kwa Mrema na Mtikila ambapo siku hizi hawaeleweki kama ni viongozi wa upinzani au la. Lakini kama hakusema hivyo then ile heading ya Kibanda basi ilikuwa na makosa at least ingesomeka 'Chaguzi za Rais na Ubunge zitenganishwe:Zitto'. Mimi si mwandishi wa habari lakini ni msomaji mzuri wa habari nilisoma ile habari sikuona popote Zitto aliposema JK aongezewe muda.
 
Mimi binafsi sijaona tazizo la Zitto hapa kusema uchaguzi wa rais na wabunge utenganishwe, kweli huwa natofautiana naye kwa masuala mbalimbali kama kupinga hadharani maamuzi ya vikao vya chama ambapo yeye ni kiongozi lakini kwa hili yuko huru kabisa kutoa maoni yake ambayo kimsingi bado nayaona yana mantiki.

Ila kama kweli alitamka JK aongezewe muda that is the issue people might judge him differently ajifunze kwa Mrema na Mtikila ambapo siku hizi hawaeleweki kama ni viongozi wa upinzani au la. Lakini kama hakusema hivyo then ile heading ya Kibanda basi ilikuwa na makosa at least ingesomeka 'Chaguzi za Rais na Ubunge zitenganishwe:Zitto'. Mimi si mwandishi wa habari lakini ni msomaji mzuri wa habari nilisoma ile habari sikuona popote Zitto aliposema JK aongezewe muda.

Oh, well, politics is a dirty game. And I think Zitto should know better. I re-read the Tanzania Daima's piece, and I find no evidence that it's a bad journalism. In fact, I think it was a true creativity of a foward-looking journalist. Of course, any good journalist would have somewhat read too much into what Zitto said [no question about that]!But seriously, Zitto's mess is one of his own making, and I don't blame Tanzania Daima at all for that(even though I wish if they had worded their headline a bit different). That said, every good politician, should and must know how to weigh and measure his words more carefully knowing that there is a danger out there for common citizens and/or journalist to enterpret, construed, even apply 'em words far from its normal/original meaning. Any politician who doesn't weigh his words more carefully, I must say, is doomed to make rookie mistakes just as awful as Zitto. The bottom line is, Zitto did not mince his words carefully.
Ah, I guess our country is deep trouble!
 
Inaelekea wataalamu wa kupindisha mambo na upotoshaji hawapo katika Tanzaniadaima na magazeti mengineo tu. Kuna watu wanataka kuendelea mchezo huu wa upotashaji wa makusudi ili kujenga picha mbaya kwa huyo wanayemuona adui wao, yaani Zitto.
Zitto hakulalamika kuhusu hoja aliyoitoa bali alilamika kuhusu upotoshaji wa makusudi wa hoja yake ambao umefanywa na muandishi/waandishi na kupitishwa na mhariri wa Tanzaniadaima aliyekouwa kazini siku hiyo, ama ni Ansbert Ngurumo au Absalom Kibanda.

Na katika hili hakuna suala la kukosa umakini kwa upande wa muandishi/waandishi wa habari pamoja na wahariri wake.

Ni wazi kabisa alieandika hiyo habari alikuwa anajua anachokifanya na wala siamini kama ni kazi ya muandishi mmoja bila ya ushirikiano wa waandishi watendaji wa gazeti hili ambao ni wataalamu wa upotoshaji wa makusudi - SPINING.

Ukiangalia ni wazi habari hii iliandikwa ikiwalenga watanzania walio wengi wasio na upeo wa kuchambua habari hizi kwa mapana yake, na ambao hawajui siasa za ndani za vyombo vyetu vya habari na ambao kutokana na uwezo wao kifedha ama utamaduni uliojengeka huishia kusoma vichwa vya habari tu vya magazeti na kufikia conclusions ambazo mwandishi ama waandishi wa habari ndizo wangependa wafikie.

Kinachouma zaidi ni kuwa gazeti hili sio just another newspaper when it comes to Zitto and the ongoing politics in CHADEMA.

Yawezekana kabisa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe hajahusika kabisa na habari hii lakini kuna historia ambayo wote tunapaswa kuiangalia kwa umakini. Wakati gazeti hili ambalo Freeman ni mmiliki wake ambalo liko chini ya kampuni ya FreeMedia kwa kutumia jina la mwanafamilia wake, limekuwa likiandika habari na makala lukuki zenye kulenga kujenga hali ya kutokumuamini na hata chuki dhidi ya Zitto tangia siku aliporudisha fomu ya kugombea UENYEKITI akishindana na Freeman Mbowe.

Mtu wa mwanzo kabisa kuandika aina hiyo ya makala ni ABSALOM KIBANDA ambaye hapa anajaribu kulazimisha kuwa uandishi huu wa Mobini Sarya ulikma ni uzembe tu na sio wenye nia mbaya.

Kibanda ni rafiki mkubwa wa Zitto na pia ni rafiki yangu lakini ukweli katika hili siwezi kabisa kufunika chungu maana ni wazi wameamua kuweka wazi vita yao dhidi ya Zitto kwa manufa yao binafsi na ya wale wanaodhani kuwa CHADEMA ni miliki yao na Zitto ni mzamiaji ambaye wangependa kumona wanammaliza kama wasemavyo.

Ni ajabu sana kuona sumu kama hii inatoka katika gazeti lenye uhusiano na mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ambaye siku moja tu kabla gazeti hilohilo lilimkariri Freeman akidai kuwa yeye hana ugomvi na "mdogo" wake Zitto.

Na kwa wale wanaodhani kuwa eti SIASA NI MCHEZO MCHAFU hivyo tuyaache haya yakiendelea kama vile ndivyo inavyopaswa kuwa, ujumbe wangu ni kuwa hata kama wengi waliopo katika siasa wanaona hivyo lakini sisi wengine tunaoamini katika mabadiliko makini tuna jukumu la kusiamama kidete kuhakisha kuwa tunajenga utamaduni wa SIASA SAFI.

Bila ya kusimama kidete kupigania SIASA SAFi kwa kukemea na kutojihusiaha na siasa chafu kamwe hatutakuwa na uhalali wa kujidai kuwa tunapigania mabadiliko chanya kwa nchi yetu. Tutaendelea kuwa watumwa wa siasa za ujanjaujanja na longolongo zinazotugharimu sasa...
 
Back
Top Bottom