Tanzania imekuwa nchi ya kutisha sana. Inapotokea mtu anagusa maslahi ya mafisadi halafu akaugua ghafla ni lazima watu tushtuke kutokana na mafunzo tuliyopata katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Amina aligusa mahala padogo tu, matokeo yake akaugua kimchezomchezo mwishowe yakawa makubwa hadi leo bado tunaomboleza. Balali alijua kitu fulani kuhusu wizi wa BOT tu, akaugua ghafla hadi leo hatujui alikuwa akijua nini.
Historia za namna hiyo zimenifanya niwe nachukulia kwa uzito sana swala lolote la mtu kuugua ghafla huku ikijulikana kuwa mtu huyo alikuwa anapingana na mafisadi. Inawezekana kabisa kuwa Mh. Zitto ana tatizo la kawaida kabisa lakini position yake katika mduara wa kisasa hapa kwetu inanifanya niwe concerned sana. Nitafurahi sana kupata updates kuhusu hali ya mheshimiwa huyu; kama kuna anayejua kuwa anaendeleaje tafadhali sana atuarifu.