Zitto amezidi kuwachefua Watanzania

Zitto amezidi kuwachefua Watanzania

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Nakumbuka kabisa alifanya usaliti mkubwa sana kukivuruga CHADEMA kikiwa na nguvu kubwa kiasi Cha kutaka kukamata dola. Akawa anakula rushwa na kuvuruga chama Kwa kufanya uzandiki.

Leo hii anatumika kuhujumu Watanzania wasipate katiba mpya kisa tu ACT Wazalendo ni vibaraka wa CCM na yeye anajipigia pesa kupitia migongo ya wapemba.

Anataka Chadema iwe branded kama chama cha kigaidi kama ilivyo Islamic brotherhood ya Misri. Hii yote ili ACT ipate nguvu. Hata avue nguo hadharani ACT haiwezi kupata kick hapa Tanzania.
20220207_050508.jpg
 
Nani kakuambia kila Mtanzania anaipenda Chadema? Wapi Zitto amewakataza Chadema kudai katiba mpya au mnatafuta wa kumsingizia?

Watu washaachwa wavae T-shirt na kufanya mikutano ya hiyo katiba mpya sasa tatizo liko wapi wakati wananchi wanajionea wenyewe?

Halafu hao unaoita Wapemba nao ni Watanzania halali kabisa wana haki ya kupenda chama chochote kile.
 
Sasa ni nyuzi mfululizo za malalamiko juu ya zitto ama mfa maji haishi kutapatapa!
 
Nakumbuka kabisa alifanya usaliti mkubwa sana kukivuruga Chadema kikiwa na nguvu kubwa kiasi Cha kutaka kukamata dola. Akawa anakula rushwa na kuvuruga chama Kwa kufanya uzandiki...
Afadhali tusiwe na vyama vya upinzani kuliko kukiamini chama kinachoongozwa na Zito kuwa kinaweza kuwa chama cha upinzani.
 
CDM bado hajamsahau ex wake Zitto. Zitto anaishi maisha yake happily
Nashangaa walimfukuza akaanzisha chama chake ila mpaka leo wanaweweseka na zitto wanataka afuate misingi na misimamo yao wanasahau kuwa ana chama chake.
 
Nashangaa walimfukuza akaanzisha chama chake ila mpaka leo wanaweweseka na zitto wanataka afuate misingi na misimamo yao wanasahau kuwa ana chama chake.
Nadhani tatizo siyo Zito kuwa na chama chake, tatizo la Zito ni unafiki na ukigeugeu.

Ni Zito, baada ya wanachama na wapenzi wa chama chake kuuawa kule Zanzibar wakati wa uchaguzi, aliyetamka kuwa hawatayatambua matokeo ya uchaguzi Zanzibar, na hawatashirikiana na Serikali ya CCM Zanzibar. Wenzake kutoka vyama vya upunzani wakamwunga mkono.

Ghafla akabadilika, ja kusema yupo kwenye SUK. Waliomwunga mkono, akawaacha hewani.

Akasema ACT wazalendo itapigania katiba mpya, ghafla akabadilika kuwa wanaunga mkono mpango wa CCM wa Tume ya uchaguzi kwanza.

Kigeugeu wa namna hii utamwamini kwa lipi? Hata CCM wakifanya kosa la kumwamini Zito, watashangaa siku atakapowageuka. Zito ni popo, si mnyama, si ndege.
 
Nadhani tatizo siyo Zito kuwa na chama chake, tatizo la Zito ni unafiki na ukigeugeu.

Ni Zito, baada ya wanachama na wapenzi wa chama chake kuuawa kule Zanzibar wakati wa uchaguzi, aliyetamka kuwa hawatayatambua matokeo ya uchaguzi Zanzibar, na hawatashirikiana na Serikali ya CCM Zanzibar...
Kila mtu anahitaji milestone. Kwani sio chadema waliozunguka nchi nzima wakisema lowassa fisadi? Lema hadi akasema ni baraka kwa Mungu fisadi lowassa kupigwa mawe.

Lakini si chadema iligeuka ikampokea baada ya kuona itazoa kura nyingi? Sasa kwanini iwe nongwa kwa zitto kama vile chadema uwa hawageuki geuki? Alichofanya zitto kinhefanywa na chadema mngesema ni good political move.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Nashangaa walimfukuza akaanzisha chama chake ila mpaka leo wanaweweseka na zitto wanataka afuate misingi na misimamo yao wanasahau kuwa ana chama chake.
Zito Ongelee chama chake yeye hawezi kufeel uchungu wa mbowe kama familia yake na wanachadema angekuwa muungwaana ange washauri chini ya jukwaa sio kuwaongelea kwenye majukwaa kama wao ni mabubu,haya mambo ya kiitikadi mnataka kutaleta tunawa Zoom tu.
 
Basi sawa
 
Back
Top Bottom