Zitto anajua nini anafanya

Zitto anajua nini anafanya

Umeandika kishabiki sana.
1: Hukumu ya mahakama hiyo haina maana kwani Tanzania ana hiyari kuitii au kuipuuza.
2: Lissu hawezi kuwa mgombea mwenza kwani kisheria mgombea mweza anatakiwa kutokea upande wa pili wa muungano.
3: Hata Mbowe alijua Lowasa hatashinda. Bali alilenga wabunge na ruzuku. Na alifanikiwa
Kama ni mwanasheria tufafanulie hiyo hukumu ina maana gani kwa Tanzania. Jibu hoja.
 
Nani alikwambia membe sio muislam? Hoja ya udini bado itawatafuna sana na hawawezi kufika mbali.
 
Siyo kweli, soma post zangu za zamani utaelewa kuwa sijali chama bali najali mabadiliko ya kweli. CDM is done, they know it.

Cdm is done ila sio kwa kukosa wapiga kura ama mvuto, hilo uliweke akilini. Wote tunaona chaguzi za kishenzi, kikatili na kihayawani ili kuhakikisha cdm hawatangazwi washindi. Kama ni kufa kwa mantiki hiyo uko sawa, ila sio kwa kukosa mvuto kwa umma.
 
Kama ni mwanasheria tufafanulie hiyo hukumu ina maana gani kwa Tanzania. Jibu hoja.

Ww hujui siasa bali ni mpuuzi fulani uliyeamua kuleta upuuzi wa propaganda za kizee, ndio maana unaongea vitu vinavyochangia ujinga wako kukaa hadharani.
 
Cdm is done ila sio kwa kukosa wapiga kura ama mvuto, hilo uliweke akilini. Wote tunaona chaguzi za kishenzi, kikatili na kihayawani ili kuhakikisha cdm hawatangazwi washindi. Kama ni kufa kwa mantiki hiyo uko sawa, ila sio kwa kukosa mvuto kwa umma.
Nakubaliana nawe kiasi fulani, kifo cha chadema ni kwa sababu ya kimazingira zaidi ya kufa kwa hoja zao. Kwa sasa wamewekwa kwenye wakati mgumu sana.
 
Ww hujui siasa bali ni mpuuzi fulani uliyeamua kuleta upuuzi wa propaganda za kizee, ndio maana unaongea vitu vinavyochangia ujinga wako kukaa hadharani.
Akhsante kwa kutuonyesha busara zako!
 
Unasema "mwaka 2025 Chadema hawatakuwa na mtu mwenye wasifu wa kugombea Urais", hili sijui umelipata wapi?

Usitake uonekane mganga wa kienyeji humu ndani, siku zote siasa ni matukio, na matukio yanatokea kila siku, hata yule unaemuona leo hana mvuto huwezi kujua hiyo 2025 atakuwa wapi, nani alitegemea mwaka 2016 Lissu angekuwa na haiba na mvuto aliokuwa nao leo?

Unasema Magufuli hajali nani atakuwa Rais 2025, myfriend you must be mad, hujielewi kabisa, na wala hueleweki nini ukichoandika, kama Magufuli anamsimamo huo tusingemuona kila siku akihangaika kulazimisha kuipoteza Chadema, analazimisha kuipoteza Chadema ili chama chake kikose mshindani wa kweli, kwani hao unaowapigia debe wewe ni wasanii tu, hakuna jasusi wala nini.

Umempamba sana Zitto kwenye andiko lako, kama ni mahaba yako binafsi au whatever I dont care, kwa kifupi kuweka matumaini yako yote kwa ACT sababu tu wana Membe ni upofu, hiyo kanda ya kusini bado wewe na wenzako hamjaweza kuthibitisha nguvu ya Membe mpaka pale kura zitakapopigwa na matokeo kutoka, vinginevyo andiko lako lote limejaa ndoto tu!.
 
Hauna aibu hoja hii aliipandikiza kichwani mwako mbowe mpaka leo unayo

Nika mbwa jike umeingiliwa na dume na mmenatana! Phyuu aibu

Zitto huyu anayekomaa na kupambana na JPM ana haja gani ya kuwa ndumilakuwili akakae meza moja na JPM? Ana gain nini?

CDM historia inaandikwa, kilikuwa chama kikubwa
Umeona uje na rundo la matusi ili ujaribu kuficha ukweli, humtishi mtu na mitusi yako, hamna lolote na huyo jasusi wenu, kama alishindwa akiwa ndani ya CCM tena akiwa mgongoni mwa JK ataweza leo akiwa upinzani?!

Katafuteni watoto muwadanganye na lile igizo lenu la jana pale Mlimani City.
 
Umeona uje na rundo la matusi ili ujaribu kuficha ukweli, humtishi mtu na mitusi yako, hamna lolote na huyo jasusi wenu, kama alishindwa akiwa ndani ya CCM tena akiwa mgongoni mwa JK ataweza leo akiwa upinzani?!

Katafuteni watoto muwadanganye na lile igizo lenu la jana pale Mlimani City.

Nani mpinzani? Mtaje
 
Unasema "mwaka 2025 Chadema hawatakuwa na mtu mwenye wasifu wa kugombea Urais", hili sijui umelipata wapi?

Usitake uonekane mganga wa kienyeji humu ndani, siku zote siasa ni matukio, na matukio yanatokea kila siku, hata yule unaemuona leo hana mvuto huwezi kujua hiyo 2025 atakuwa wapi, nani alitegemea mwaka 2016 Lissu angekuwa na haiba na mvuto aliokuwa nao leo?

Unasema Magufuli hajali nani atakuwa Rais 2025, myfriend you must be mad, hujielewi kabisa, na wala hueleweki nini ukichoandika, kama Magufuli anamsimamo huo tusingemuona kila siku akihangaika kulazimisha kuipoteza Chadema, analazimisha kuipoteza Chadema ili chama chake kikose mshindani wa kweli, kwani hao unaowapigia debe wewe ni wasanii tu, hakuna jasusi wala nini.

Umempamba sana Zitto kwenye andiko lako, kama ni mahaba yako binafsi au whatever I dont care, kwa kifupi kuweka matumaini yako yote kwa ACT sababu tu wana Membe ni upofu, hiyo kanda ya kusini bado wewe na wenzako hamjaweza kuthibitisha nguvu ya Membe mpaka pale kura zitakapopigwa na matokeo kutoka, vinginevyo andiko lako lote limejaa ndoto tu!.

😂😂😂 Membe hana nguvu wala hautakiwi kusubiria uchaguzi. Membe anaikuza ACT
 
Ningekuwa niko kwenye nafasi yako ningewapa hii offer Chadema kabla ya uchaguzi: Tundu Lisu awe mgombea mweza wa Membe na baada ya uchaguzi 60% ya wabunge wa kuteuliwa watachaguliwa kutoka Chadema.
Katiba ya Jamhuri haikubali hili. Membe anatoka upande mmoja wa Muunmgano na Tundu Lissu. Rais akitoka Bara mgombea mwenza lazima atoke visiwani.
 
Act kuwa main opposition party ningumu hata Mbowe akiamua kwenda Act
 
Mtu ambaye hatari zaidi kwa upinzani sio Magufuli, bali ni Zitto mwenyewe.
 
Kete kubwa walivyocheza CCM kwenye Uchaguzi wa mwaka huu

Ni Membe kwenda ACT-Wazalendo

Hii itagawa kura za Wapinzani, na JPM atashinda kama alivyoshinda kwenye Uchaguzi ndani ya Chama baada ya Membe na Lowasa kutofautiana mwaka 2015.

ACT Wazalendo watawataka CHADEMA (kwa kuwa ndio Chama cha upinzani chenye nguvu) waunde nao umoja ili wasimamishe mgombea mmoja wa upinzani wakishawishi kuwa wao ndio wana mgombea presidential material zaidi (Membe)

CHADEMA hawatakubali kwa hoja tatu, moja ni kwamba wameshajaribu kumtumia mercenary Lowasa na ikashindikana na akarudi 'nyumbani', hivyo kurudia makosa yale yale ni insanity, pili wao wana mgombea makini mpinzani halisi (mgombea yoyote kati ya waliochukia fomu) na tatu hawapo tayari kujiweka kama Chama cha pili cha upinzani kwa kukubali Chama kingine ndio kisimamishe mgombea wa Urais na wao waunge mkono (hii hawataisema hadharani).

Pia mwaka 2015 sio zamani sana, hivyo CHADEMA hawajasahau ACT-Wazalendo hawakuwaunga mkono walipomsimamisha Lowasa chini ya UKAWA.

Hapa ndio kila Chama kitachukua njia yake, na ndipo JPM atapita kiulaini sana.

Jamani enhe, hapo kuhusu mambo ya Tume Huru ya Taifa msiniulize kabisaa

ZITTO ANAJUA NINI ANAFANYA.

Mbowe alipompeleka Lowasa Chadema (inasadikika kidikteta) alisema wamebadilisha gia angani. Mbowe alikuwa anaamini Lowasa atashinda uchaguzi, alitegemea kuwa ile mitandao ya Lowasa italinda kura na Chadema kitashika madaraka.Baada ya matokeo ya uchaguzi (inasadikika yalichakachuliwa)CCM wakaweka nia ya kuua upinzani (Chadema) kabla ya 2020. Lowasa akatishiwa kupotezewa hela na mwanafamilia wa karibu akafunguliwa kesi. Lowasa akakubali yaishe akarudi CCM, the rest is history.

Sasa swali la kujiuliza ni kwanini Zitto na ACT warudie yaleyale Chadema waliyafanya? Jibu rahisi ni kuwa Zitto anajua nini anafanya kama ilivyochambuliwa hapo chini:

  • Anajua kuwa Magufuli anashinda urahisi 2020 kwa sababu:
  • Hakuna tume huru
  • Wametayarishwa wakuu wa wilaya na watendaji wengine kuhakikisha hilo linatimia
  • Vitisho vya polisi vimeshaanza
  • na kadhalika, na kadhalika
Sasa kama anajua hawatashinda urahisi kwanini wanamtanguliza Membe na kwa nini alimkaribisha Maalimu ACT?

  • Zitto plan yake ni kuwa chama kikuu cha upinzani kabla ya 2025. Hili halihitaji ufafanuzi.
  • Anataka kuweka mazingira ya yeye kuwa mgombea wa uraisi kwa niaba ya upinzani 2025. Anajua kuweka jina lake kugombea urahisi sasa hivi alafu ashindwe ni kujichafulia jina. Hayuko tayari kushindwa alafu agombee tena miaka na miaka kwani hiyo haiendani na imani yake ya ukishindwa waachie wengine (rejea ugonvi wake ndani ya chadema). Akigombea tena baada ya kushindwa ataitwa mnafiki.
  • Membe anaweza kumsaidia kupata wabunge maeneo ya kusini. Ikumbukwe CUF ndiyo alikuwa mpinzani mkuu maaneo haya. Kumpata Membe kutapunguza zaidi wafuasi wa CCM maeneo hayo.
  • Ataongeza kipato cha ruzuku kwa kuwa na wabunge wengi bungeni. Pemba na maeneo yote ambapo CUF inanguvu yatageuka kuwa ACT. Hela itamruhusu kufanya shughuli nyingi za chama.
  • Kumweka Membe kunaua jinamizi la hoja ya udini iliyotumika kuikandamiza CUF. CCM walitumia ukanda kuipinga Chadema na udini kuipinga CUF. Kumkaribisha Membe kumeua ndege wawili kwa jiwe moja na hizo hoja zote mbili za CCM zimepotea.
  • Vindication.. pamoja na yote Zitto anayosema hadharani moyoni bado anamachungu na kuondolewa kwake Chadema. Chadema inakufa kifo cha kuchanwa chanwa na wembe mara 1000. Mwaka 2025 chadema hawatakuwa na mtu yeyote mwenye wasifu wa kugombea uraisi, labda Lisu agombee tena au wamweke Halima Mdee. Chadema kupona kisiasa wanahitaji miujiza kwa sasa. Baada ya chadema kusukumwa kwenye kona hawatakuwa na jinsi bali kumpa ushirikiano Zitto atakapotangaza nia 2025 kwani chama chake kitakuwa na nguvu zaidi. Na Zitto alishasema "Zaburi 118:22 jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la msingi", Wote tunashuhudia taratibu anavyotimiza huo usemi.
  • Magufuli hajali nani atakuwa raisi 2025 ila anaogopa kushitakiwa. Hii itaonekana zaidi kwenye matukio yatakayofuata baada ya uchaguzi. Magufuli keshabadili sheria ili imlinde, ila kama tulivyoona Malawi na Zambia, hilo pekee halitoshi. Unahitaji raisi anayekufuata akulinde Nkurunzinza alimweka mtu wake mungu akampenda, Kabila kaweka mtu wake na mpaka sasa wananchi wa congo wanapiga kelele. Magufuli katika kujaribu kujilinda anaweza weka mtu ambaye CCM na Taifa haitakuwa tayari kumpokea na hivyo kumpa Zitto nafasi 2025.
  • Hukumu ya Mahakama ya Africa iliyotolewa siku chache zilizopita inampa nafasi 2025. Hii haikuwa kwenye mahesabu ya Zitto lakini ni kama zawadi ya mungu na ataipokea kwa mikono miwili. Uchaguzi wa 2025 utakuwa ni uchaguzi wa kwanza Tanzania ambapo mshindi wa uraisi anaweza shitakiwa mahakamani. Hili ni pigo kubwa kwa CCM kwa sababu itafuta uhalali wakujipa kuongoza inchi. Kwa Zitto na ACT hii ni nafasi kuitoa jasho CCM. Kwa mgombea yeyote wa uraisi 2025 anajua kuwa ana nafasi ya kudai haki mahakamani.
  • Anapiga mahesabu ya magufuli na CCM kuendelea kuwasomesha namba watanzania. hasira ya wa watanzania 2025 haitapimika kama hali ya hela haitabadilika mifukoni mwa watanzania.
  • Haitaji kura za ukanda wa kaskazini mashariki kushinda uraisi. Ikumbukwe Zitto alikuwa wa kwanza kulalamika ukaskazini ndani ya Chadema. Mpaka sasa chadema mizizi yake mikuu bado ipo kaskazini mashariki. Zitto kashachukua Zanzibar na kusini mashariki. Hesabu zake kwa sasa ni jinsi ya kuipata mikoa ya kati na magharibi kaskazini. Hili atalifanyia kazi miaka mitatu ijayo. Ila kazi anayo kushindana na hoja za flyover, ringroad, SGR, vivuko nakadhalika nakadhalika.
  • Anajua kinyongo kinatoa mtu mwaminifu kwa adui. Ingawaje wengi wanakejeli Membe kuhamia ACT na kusema ni sawa na Lowasa, hasira ya Membe si kufukuzwa chama bali ni kunyimwa nafasi aliyoamini ni ya kwake kugombea uraisi 2015. Ikumbukwe, mkapa na kikwete wote walishikilia mambo ya nje, kichwani kwa Membe kupewa majukumu ya kidiplomasia ni kutayarishwa kuwa raisi. Hivyo basi hakukuwa na mwingine zaidi yake ndani ya CCM aliyekuwa na haki ya kuwa raisi. Uelewa wa Zitto kuwa hicho kinyongo kinampa amani kuwa Membe ni pons mzuri kwenye bigger chess game.
  • Anajua hamuitaji tena Membe baada ya Miezi 6. Membe akishindwa hana haki ya kugombea tena, Membe akishampa wabunge wa kusini hamuitaji tena. Ila thamani ya Membe si hapo tu bali pia ni mahusiano aliyojenga na mataifa ya nje wakati wa kazi zake. Mataifa makubwa ndo watatumika kuweka pressure pale inapohitajika kuilazimisha CCM ibadili muendeleo wa kisiasa Tanzania. Zitto anachohitaji kwa Membe ni kutambulishwa tu kwa walioishika dunia na mengine yatafuatilia.
  • Anajua watanzania kwa sasa wamekata tamaa ya kuiondoa CCM. Hii itathibitishwa na idadi ya watu watakaojitokeza kupiga kura. Dalili zote zilianza kuonekana wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa, watu walikata tamaa. Hakuna sababu ya yeye kuweka jina lake kugombea uraisi wakati anajua watanzania wamekata tamaa.
  • Haitaji kuichafua CCM wapo wengi watakayoyaweka mabaya yake hadharani. Hapa naongelea jinsi gani Lisu atamsafishia njia Zitto. CCM wawe waangalifu sana na jinsi watakavyo deal na Lisu. Dunia nzima inaangalia na Lisu anaweza kuwa Ken Saro-Wiwa wa Tanzania, kitakachomtokea yeye ikawa ndo fimbo iliyovunja mgongo wa ngamia. Hii ni ya kuongelea siku nyingine.
  • Haitaji kusubiri miaka kumi kugombea uraisi. Membe hatashinda uraisi, period. Angeshinda inamaana zitto angehitaji kusubiri miaka 10. Miaka kumi ni mingi sana kwenye siasa anaweza tokea mtu mwingine machachari akaidumaza nyota ya Zitto. Zitto mwenyewe hayuko tayari kusubiri mda mrefu hivyo.
Membe alisema mengi yatatokea kabla ya uchaguzi. Hili la hukumu ya african court imerusha karata nyingine ambayo hatujui hatma yake itakuwaje. Labda wanasheria tufafanulieni hii hukumu inaweza kutumika kubatili matokeo 2020?

Ushari wangu kwa Zitto, wape Chadema an offer they cant resist before this election. Itakuwa vigumu wao kukuunga mkono baada ya 2020 ukisubiri wadhalilishwe kwanza kwenye uchaguzi. Ningekuwa niko kwenye nafasi yako ningewapa hii offer Chadema kabla ya uchaguzi: Tundu Lisu awe mgombea mweza wa Membe na baada ya uchaguzi 60% ya wabunge wa kuteuliwa watachaguliwa kutoka Chadema. Viongozi wengi wa Chadema na wanaharakati wa kweli wako katika hatari ya kupotea kisiasa. Hawa watakuwa wanajeshi wazuri kwa ACT pale upinzani wa kweli utakapoitikisa CCM 2025. This is a win-win situation, viongozi wazuri wa chadema wataendelea kuwepo bungeni na ACT itaheshimika kaskazini mashariki na ukanda wa kati.

Mwisho nasema msiwakejeli ACT na Zitto wanajua nini wanafanya. Wana chadema jitayarisheni kisaokolojia kumeza matapishi yenu (Zitto) na kuwa chama kikuu cha pili cha upinzani Tanzania. Ila mjue kuwa hakuna adui kwa wanaotaka mabadiliko ya kweli. Kupanda kwa Zitto inaweza kuwa baraka kubwa sana kwa Chadema kama vichwa vilivyotulia vikifanya kazi.
akhsanteni
Puza
 
Ni ndoto tu kama ndoto zingine zilizootwa 2015 . "Wakati " ndiyo una majibu ya kweli, ni suala la wakati tu . Membe atawatia kisomo ACT kama vile Lowasa ilivyokua kwa Chadema .

A TIME WILL TELL US KIKUBWA NI UZIMA
 
Back
Top Bottom