Zitto anajua nini anafanya

Kama ni mwanasheria tufafanulie hiyo hukumu ina maana gani kwa Tanzania. Jibu hoja.
 
Nani alikwambia membe sio muislam? Hoja ya udini bado itawatafuna sana na hawawezi kufika mbali.
 
Siyo kweli, soma post zangu za zamani utaelewa kuwa sijali chama bali najali mabadiliko ya kweli. CDM is done, they know it.

Cdm is done ila sio kwa kukosa wapiga kura ama mvuto, hilo uliweke akilini. Wote tunaona chaguzi za kishenzi, kikatili na kihayawani ili kuhakikisha cdm hawatangazwi washindi. Kama ni kufa kwa mantiki hiyo uko sawa, ila sio kwa kukosa mvuto kwa umma.
 
Kama ni mwanasheria tufafanulie hiyo hukumu ina maana gani kwa Tanzania. Jibu hoja.

Ww hujui siasa bali ni mpuuzi fulani uliyeamua kuleta upuuzi wa propaganda za kizee, ndio maana unaongea vitu vinavyochangia ujinga wako kukaa hadharani.
 
Cdm is done ila sio kwa kukosa wapiga kura ama mvuto, hilo uliweke akilini. Wote tunaona chaguzi za kishenzi, kikatili na kihayawani ili kuhakikisha cdm hawatangazwi washindi. Kama ni kufa kwa mantiki hiyo uko sawa, ila sio kwa kukosa mvuto kwa umma.
Nakubaliana nawe kiasi fulani, kifo cha chadema ni kwa sababu ya kimazingira zaidi ya kufa kwa hoja zao. Kwa sasa wamewekwa kwenye wakati mgumu sana.
 
Ww hujui siasa bali ni mpuuzi fulani uliyeamua kuleta upuuzi wa propaganda za kizee, ndio maana unaongea vitu vinavyochangia ujinga wako kukaa hadharani.
Akhsante kwa kutuonyesha busara zako!
 
Unasema "mwaka 2025 Chadema hawatakuwa na mtu mwenye wasifu wa kugombea Urais", hili sijui umelipata wapi?

Usitake uonekane mganga wa kienyeji humu ndani, siku zote siasa ni matukio, na matukio yanatokea kila siku, hata yule unaemuona leo hana mvuto huwezi kujua hiyo 2025 atakuwa wapi, nani alitegemea mwaka 2016 Lissu angekuwa na haiba na mvuto aliokuwa nao leo?

Unasema Magufuli hajali nani atakuwa Rais 2025, myfriend you must be mad, hujielewi kabisa, na wala hueleweki nini ukichoandika, kama Magufuli anamsimamo huo tusingemuona kila siku akihangaika kulazimisha kuipoteza Chadema, analazimisha kuipoteza Chadema ili chama chake kikose mshindani wa kweli, kwani hao unaowapigia debe wewe ni wasanii tu, hakuna jasusi wala nini.

Umempamba sana Zitto kwenye andiko lako, kama ni mahaba yako binafsi au whatever I dont care, kwa kifupi kuweka matumaini yako yote kwa ACT sababu tu wana Membe ni upofu, hiyo kanda ya kusini bado wewe na wenzako hamjaweza kuthibitisha nguvu ya Membe mpaka pale kura zitakapopigwa na matokeo kutoka, vinginevyo andiko lako lote limejaa ndoto tu!.
 
Umeona uje na rundo la matusi ili ujaribu kuficha ukweli, humtishi mtu na mitusi yako, hamna lolote na huyo jasusi wenu, kama alishindwa akiwa ndani ya CCM tena akiwa mgongoni mwa JK ataweza leo akiwa upinzani?!

Katafuteni watoto muwadanganye na lile igizo lenu la jana pale Mlimani City.
 

Nani mpinzani? Mtaje
 

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Membe hana nguvu wala hautakiwi kusubiria uchaguzi. Membe anaikuza ACT
 
Ningekuwa niko kwenye nafasi yako ningewapa hii offer Chadema kabla ya uchaguzi: Tundu Lisu awe mgombea mweza wa Membe na baada ya uchaguzi 60% ya wabunge wa kuteuliwa watachaguliwa kutoka Chadema.
Katiba ya Jamhuri haikubali hili. Membe anatoka upande mmoja wa Muunmgano na Tundu Lissu. Rais akitoka Bara mgombea mwenza lazima atoke visiwani.
 
Act kuwa main opposition party ningumu hata Mbowe akiamua kwenda Act
 
Mtu ambaye hatari zaidi kwa upinzani sio Magufuli, bali ni Zitto mwenyewe.
 
Kete kubwa walivyocheza CCM kwenye Uchaguzi wa mwaka huu

Ni Membe kwenda ACT-Wazalendo

Hii itagawa kura za Wapinzani, na JPM atashinda kama alivyoshinda kwenye Uchaguzi ndani ya Chama baada ya Membe na Lowasa kutofautiana mwaka 2015.

ACT Wazalendo watawataka CHADEMA (kwa kuwa ndio Chama cha upinzani chenye nguvu) waunde nao umoja ili wasimamishe mgombea mmoja wa upinzani wakishawishi kuwa wao ndio wana mgombea presidential material zaidi (Membe)

CHADEMA hawatakubali kwa hoja tatu, moja ni kwamba wameshajaribu kumtumia mercenary Lowasa na ikashindikana na akarudi 'nyumbani', hivyo kurudia makosa yale yale ni insanity, pili wao wana mgombea makini mpinzani halisi (mgombea yoyote kati ya waliochukia fomu) na tatu hawapo tayari kujiweka kama Chama cha pili cha upinzani kwa kukubali Chama kingine ndio kisimamishe mgombea wa Urais na wao waunge mkono (hii hawataisema hadharani).

Pia mwaka 2015 sio zamani sana, hivyo CHADEMA hawajasahau ACT-Wazalendo hawakuwaunga mkono walipomsimamisha Lowasa chini ya UKAWA.

Hapa ndio kila Chama kitachukua njia yake, na ndipo JPM atapita kiulaini sana.

Jamani enhe, hapo kuhusu mambo ya Tume Huru ya Taifa msiniulize kabisaa

 
Ni ndoto tu kama ndoto zingine zilizootwa 2015 . "Wakati " ndiyo una majibu ya kweli, ni suala la wakati tu . Membe atawatia kisomo ACT kama vile Lowasa ilivyokua kwa Chadema .

A TIME WILL TELL US KIKUBWA NI UZIMA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…