Pre GE2025 Zitto ashauri upinzani kuungana kwenye chaguzi kuing’oa CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huyu Dogo muhuni tu. akiwa kwenye kikosi kazi si alisema mama yao atawale mpaka 2030 then ndo atakayekuja baada ya hapo apingwe

Pia Alisha kiri hadharani kuwa hatampinga mama yake

Sasa nani waungane wakati ameisha kuwa na upande tayari

Au maokoto aliyopewa yamemeisha sasa anataka aongezewe
Hawa wanasiasa uchwara wanatumia confuse wananchi
 
Ni ushauri mzuri.
 
Kwa mfumo huu wa uchaguzi kuing'oa CCM haiwezekana ambapo CCM wakati wa uchaguzi huwa wanaenda maporini, wengine wakienda huko huchimba dawa bila kutumwa na serikali
 
Yani huyo takataka dah
 
Huyu mwami ni kibaraka wa Ccm hapaswi kuaminiwa na watu wanaoamini katika mabadiliko, ni kweli kuungana ni jambo jema sana maana umoja ni nguvu ila si kwa kuunganishwa na ZZK
 
Ukiungana na Zitto unakuwa dhaifu, mfano ni wanachama wa CUF Zanzibar walipoamua kuingia ACT, wamekuwa dhaifu sana, harakati zote za Maalim zimekufa.

Pia, kwanini muungano uwepo wakati wa uchaguzi tu, wakati hapa njiani mnapingana tu na wengine kuwa upande wa watesi?!
 
Yaani chadema wanatangaza maandamano hamuwaungi mkono,
Tena Bora mngekuwa mnakaa kimya kabisa badala yake mnatoka hadharani kuyapinga
Wenzenu walikuwa wanafufua upinzani, wanaamsha wanachama

Sahii mnataka kuungana??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…