SI KWELI Zitto: CHADEMA hawataki wenyewe kushiriki uchaguzi basi waache chokochoko

SI KWELI Zitto: CHADEMA hawataki wenyewe kushiriki uchaguzi basi waache chokochoko

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Wakuu

Ni kweli kauli hii imetolewa Zitto Kabwe "CHADEMA hawataki wenyewe kushiriki uchaguzi basi waache chokochoko"

Zitto Chokochoko Oct 9.jpg
 
Tunachokijua
Zitto Kabwe ni Kiongozi mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo na ni mgombea wa nafasi ya ubunge kupitia jimbo la Kigoma Mjini kuelekea uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25, 2025.

Madai

Kumekuwapo na grafiki yenye utambulisho wa Jambo TV ikisambazwa kupitia mitandao ya kijamii ikiwa na ujumbe unaodai kuwa Mgombea wa ubunge jimbo la Kigoma Mjini kupitia ACT Wazalendo Zitto Kabwe amewataka CHADEMA kuacha chokochoko kwa kuwa ni wao wenyewe ndiyo wamekataa kushiriki uchaguzi.

Uhalisia wa Taarifa hiyo

JamiiCheck imefanya ufuatiliaji wa kina na kujiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.

Kupitia utafutaji kw anjia ya maneno muhimu (keywords search) kama yanavyoonekana kwenye grafiki hiyo, umebaini kutokuwepo kwa chanzo chochote cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo ama kumnukuu kiongozi huyo.

JamiiCheck imepitia pia kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya Zitto Kabwe ikiwemo ule wa X na kujiridhisha kuwa hakuna ujumbe wowote uliochapishwa unaofanania na huo.

Aidha taarifa hiyo inasambazwa na grafiki tu bila taarifa kamili kueleza mahali na wakati ambapo kiongozi huyo aliyazungumza maneno hayo kuhusu CHADEMA kama inavyopaswa kuwa taarifa kamili.

Hata hivyo ufuatiliaji zaidi umejirirdhisha kuwa grafiki hiyo ni ya kughushi na haijatolewa wala kuchapishwa na Jambo TV.
Achana nae chawa huyo, msaka tonge alishapoteza mvuto, amekosa hata akili ndogo ya kujua upepo unaelekea wapi bado anawalamba nyayo watawala, soma alama za nyakati, hii miaka mitano watawala hawatoboi zitto
 
Back
Top Bottom