Zitto Kabwe aandika wimbo wa Bongo Fleva

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,610
Katika hali ambayo watu wengi hawakutegemea mbunge wa Kigoma Kaskazini Ndugu Zitto Kabwe ameandika wimbo wa Bongo Fleva unaoitwa Wema kwa Ubaya, wimbo huo amemuandikia msanii wa Kigoma (Linex/Sande Mjeda) huku sauti ya Zitto Kabwe ikisikika kidogo mwishoni alipomalizia kwa maneno machache.

Mbali na mambo mengine yaliyopo kwenye wimbo huo lakini pia kuna baadhi ya mashairi ambayo yanaonekana kuelezea hisia za Zitto Kabwe hasa katika kipindi kigumu anachopitia kisiasa.

Miongoni mwa mashairi yanayopatikana kwenye wimbo huo ni pamoja na "Hamninyimi usingizi mnao kesha na kuombea wenzenu wapatwe na mabaya, hamridhiki na mkipatacho shukrani zenu za punda Mungu anawaona......"

Mashairi mengine ni "Nimezaliwa kulipa wema ubaya, sijazaliwa kulipa ubaya kwa ubaya, i know you wish to bring me down but am telling you will never do it....."

Mwisho wa wimbo sauti ya Zitto Kabwe inasikika ikisema "Mungu hamtupi mtu mwenye dhamira ya kweli, hawezi shindwa hawezi kata tamaa"

Dr. MCHUNGUZI HURU (PhD)
 
Last edited by a moderator:
Haya Dr Muchunguzi. Hivi ni vihoja tu mengi yatakuja, ngoja tuone kwenye siasa ya 2015...
 
Wanasiasa wengi waliochoka huwa hukimbilia sanaa hasa nyimbo kumalizia..wako wapi walioandika nyimbo..MUDHIHIR,KAPUYA,SEIF KHATIB
 
Daaah wamemnyanyasa mno. Ana haki ya kutoa ya moyoni
 
Duh!! Sipati picha Zzk akikunja mdomo kuimba!! Mi nataka video tu!! Hapa Masanja inabidi akaze buti aisee!!
 
Katika hali ambayo watu wengi hawakutegemea mbunge wa Kigoma Kaskazini Ndugu Zitto Kabwe ameandika wimbo wa Bongo Fleva unaoitwa Wema kwa Ubaya, wimbo huo amemuandikia msanii wa Kigoma (Linex/Sande Mjeda) huku sauti ya Zitto Kabwe ikisikika kidogo mwishoni alipomalizia kwa maneno machache.

Mbali na mambo mengine yaliyopo kwenye wimbo huo lakini pia kuna baadhi ya mashairi ambayo yanaonekana kuelezea hisia za Zitto Kabwe hasa katika kipindi kigumu anachopitia kisiasa.

Miongoni mwa mashairi yanayopatikana kwenye wimbo huo ni pamoja na "Hamninyimi usingizi mnao kesha na kuombea wenzenu wapatwe na mabaya, hamridhiki na mkipatacho shukrani zenu za punda Mungu anawaona......"

Mashairi mengine ni "Nimezaliwa kulipa wema ubaya, sijazaliwa kulipa ubaya kwa ubaya, i know you wish to bring me down but am telling you will never do it....."

Mwisho wa wimbo sauti ya Zitto Kabwe inasikika ikisema "Mungu hamtupi mtu mwenye dhamira ya kweli, hawezi shindwa hawezi kata tamaa"

Dr. MCHUNGUZI HURU (PhD)

Hakuna uhusiano wa uzi na maelezo,jifunze kuandika kwanza ndo urudi humu jamvini
 
Last edited by a moderator:
Miongoni mwa mashairi yanayopatikana kwenye wimbo huo ni pamoja na "Hamninyimi usingizi mnao kesha na kuombea wenzenu wapatwe na mabaya, hamridhiki na mkipatacho shukrani zenu za punda Mungu anawaona......"
Mashairi mengine ni "Nimezaliwa kulipa wema ubaya, sijazaliwa kulipa ubaya kwa ubaya, i know you wish to bring me down but am telling you will never do it....."
Amegeuka kua LADY JAYDEE SIO!
 
Zitto ana vimbwanga mara katoka na Diva mara hii anatunga na anaimba bongofleva.
 
Mbona mistari haina vina wala mizani akaimbe na Kigoma all stars!!

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ha ha ha ngoja aje ney wa mitego si alishamtumia salaam zake kwenye wimbo wa "salaam zao" kuwa huku kwenye bongo fleva hawamtaki kabisa!
 
Anaimba au anawika?
mmh mi sipati picha hata nega haitoki.
Mungu hatamtupa sababu ana dhamira ya kweli kwenye bongo fleva ha ha ha kuanzia kigoma all stars hvyo maneno yetu hayamkatishi tamaa.
te he te he
 
Hahahahaaaa, huu uzi yaani umenichekesha mpaka nikatoa machozi! Ila ni kweli huu wimbo nimeuona na kuusikiliza jana mchana EATV! Kweli mwisho Zitto ameongea. Nitaufuatilia tena ili niusikilize upya nimsikilize jamaa!!
 
Back
Top Bottom