Old Member (Retired)
JF-Expert Member
- Sep 29, 2012
- 3,401
- 1,610
Katika hali ambayo watu wengi hawakutegemea mbunge wa Kigoma Kaskazini Ndugu Zitto Kabwe ameandika wimbo wa Bongo Fleva unaoitwa Wema kwa Ubaya, wimbo huo amemuandikia msanii wa Kigoma (Linex/Sande Mjeda) huku sauti ya Zitto Kabwe ikisikika kidogo mwishoni alipomalizia kwa maneno machache.
Mbali na mambo mengine yaliyopo kwenye wimbo huo lakini pia kuna baadhi ya mashairi ambayo yanaonekana kuelezea hisia za Zitto Kabwe hasa katika kipindi kigumu anachopitia kisiasa.
Miongoni mwa mashairi yanayopatikana kwenye wimbo huo ni pamoja na "Hamninyimi usingizi mnao kesha na kuombea wenzenu wapatwe na mabaya, hamridhiki na mkipatacho shukrani zenu za punda Mungu anawaona......"
Mashairi mengine ni "Nimezaliwa kulipa wema ubaya, sijazaliwa kulipa ubaya kwa ubaya, i know you wish to bring me down but am telling you will never do it....."
Mwisho wa wimbo sauti ya Zitto Kabwe inasikika ikisema "Mungu hamtupi mtu mwenye dhamira ya kweli, hawezi shindwa hawezi kata tamaa"
Dr. MCHUNGUZI HURU (PhD)

Last edited by a moderator: