Zitto Kabwe: ACT - Wazalendo na vyama washirika, Januari 2021 kuitisha Bunge maalum la bajeti kuifuta hii inayopitishwa kesho na CCM

Zitto Kabwe: ACT - Wazalendo na vyama washirika, Januari 2021 kuitisha Bunge maalum la bajeti kuifuta hii inayopitishwa kesho na CCM

The Palm Tree

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Posts
7,951
Reaction score
12,541
Zito Kabwe amesema hili leo wakati akiichambua bajeti ya Magufuli 2020/2021 pamoja na kutoa mwelekeo wa chama chake kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba, 2020.

Amesema kama chama cha ACT - WAZALENDO kitapata ridhaa ya wananchi wa Tanzania kupitia sanduku la kura ktk uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kuunda serikali itakayoshirikisha vyama washirika.

Akaendelea kusema, jambo la kwanza watakalofanya na kwa kuwa serikali chini ya ACT WAZALENDO na vyama washirika watairithi bajeti kuu hii hii inayokwenda kupitishwa na bunge la CCM kesho trh 17/6/2020, basi watakachofanya ni kuitisha Bunge maalumu la bajeti mwezi January, 2021 na kuifumua bajeti yote hii na kuiseti upya ili kuleta uhalisia.

Amesema, watairejesha nchi katika mstari wake isiendelee kuserereka kwenda kwenye uharibifu.

Tazama video yake hapa akizungumza.

 
Yaani wapinzani washike dola? Zitto nishushe njiani!! [emoji23][emoji1787]
 
Ndo sasa anautaka urais. Kweli tuwe makini kuchagua rais.
 
Alieongea ndo huyuhuyu zitto aliesafiri kwenda USA na Ulaya kuchongea watoto wa wajane,wanyonge na yatima wasipate msaada wa kuboresha miundo mbinu Yao ya elimu kisa yeye Mtoto wake anasomea international School? Au Kuna zitto mwingine.

Basi Kama Ni yeye mwambieni kuwa HATA 0.5% YA KURA CHAMA CHAKE HAKITAPATA. na hizi taarifa zimufikie na yule Mgombea urais wa online AKA Mbeligiji.
 
Zito yupo sahii.. Namuelewa sana kwa hili labajeti hewa ndani ya miaka mitano ya Magufuli. Bajeti isio na uhalisia wowote imeumiza sana nchi na watu wake.

Bajeti hewa imeshindwa kuleta ajira mpya nchini kwa miaka5 ya Magufuli. Bajeti hewa imeshindwa kuongeza mshahara watumishi wa umma kwa miaka 5ya Magufuli.

CCM Ilishajifia tupa kule na Bajeti hewa zao.
 
Hayo maneno anamwambia nani? Kama kuna mtu anajijua kuwa anaambiwa yeye basi akapate matibabu haraka kabala hajaanza kuokota chupa majalalani.
 
Zitto hilo bunge ataliitisha akiwa bangwe au gungu?
 
Back
Top Bottom