Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kiongozi mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema kuwa Operesheni Majimaji inayofanywa na chama hicho inalenga kuwaamsha Watanzania kurejesha thamani ya kura yao, ambayo amesema imeporomoka kwa kiasi kikubwa katika chaguzi tatu zilizopita.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Narunyu, Manispaa ya Lindi, Zitto alisema kuwa kwa sasa kura ya Mtanzania imepoteza heshima na uhalali kwa sababu ya kile alichokiita "kubakwa kwa mchakato wa uchaguzi."
Zitto alikumbusha jinsi ambavyo katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019, wagombea wote wa upinzani walienguliwa bila sababu za msingi, hali iliyopelekea vyama kujiondoa kwenye uchaguzi huku CCM ikiendelea kuongoza mitaa na vijiji pasipo ushindani halali.
Zitto pia alitupia lawama mabadiliko ya kiutaratibu yaliyofanyika kwenye mchakato wa uchaguzi wa mwaka 2020, akidai kuwa vyama vya upinzani viliondolewa kwenye hatua zote muhimu za uchaguzi zikiwemo uchapaji, uwasilishaji, na usambazaji wa karatasi za kura.