Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), amedai kuna upotoshaji kuhusu barua aliyoiandikia uongozi wa Benki ya Dunia (WB) kuhusu mkopo wa Dola za Marekani milioni 500 ambao Tanzania imeomba kwa benki hiyo.
Akiwa mjini Toronto, Canada juzi, Zitto alidai si lengo lake kuzuia misaada nchini ila anafanya hivyo ili kuwalinda watoto wa kike wanaopata ujauzito wakiwa katika masomo kwa kile alichodai kuwapo ubaguzi katika mfumo rasmi wa elimu nchini.
“Kwanza kuna upotoshaji wa suala hili zima kwa sababu nimeandika barua siyo kuzuia misaada ila kuitaka Benki ya Dunia kabla ya kutoa mkopo kwa Serikali ya Tanzania, izingatie kuwa mkopo ule unakwenda kuwabagua watoto wa kike ambao wamepata ujauzito na kuzuiwa kurudi shuleni," alidai.
Wiki iliyopita baada ya kuibuliwa kwa suala hilo bungeni jijini Dodoma, Spika wa Bunge, Job Ndugai, alimtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi, kuchunguza kitendo hicho cha Zitto ili kuona kama kuna jinai au la.
Alisema uchunguzi huo unapaswa kufanyika ili kama kutaonekana kuwapo kwa jinai, mbunge huyo achukuliwe hatua kufuatia hoja binafsi iliyowasilishwa bungeni na Mbunge wa Siha, Dk. Godwin Mollel (CCM), aliyetaka kuchunguzwa kwa jambo hilo.
“Mbunge mwenzetu atakaporudi, labda anaweza akatufafanulia wenzake, Mheshimiwa Zitto Kabwe kuandika barua Word Bank (Benki ya Dunia) kwamba nchi yetu ikose fedha za mkopo ambazo lengo lake ni elimu kwa sababu ya tofauti za sera," Spika Ndugai alisema.
Akijenga hoja yake siku hiyo ili aungwe mkono na wabunge, Dk. Mollel alisema: “Nasimama kwa Kanuni ya 47(1) ili kuomba kuahirisha shughuli za Bunge ili kujadili jambo la dharura. Hapa juzi mwenzetu Zitto ameandika barua kwenye Benki ya Dunia, na alipoandika barua kwenye Benki ya Dunia, alitaka fedha zizuiliwe ambazo zingekuja kusaidia elimu Tanzania.
“Lakini, pesa hizo zingekuja tungejenga shule tano kubwa kwa kila wilaya, tungeweza kuwaweka bwenini watoto zaidi ya 2,000 wa kike ambao mwisho wa siku hata kiwango cha mimba kwa taifa letu kingeshuka sana."
Alisema wabunge waliapa bungeni kwa kutumia Katiba ya Tanzania na katiba hiyo imetaja dhahiri maadui wa taifa ukiwamo umaskini, ujinga na maradhi.
Alisema unapogusa kwenye eneo hilo la elimu ina maana umefuta ujinga, umaskini na maradhi, hivyo akadai Zitto anapaswa kuchukuliwa hatua kwa kuwa amevunja katiba.
Muungwana blog