Zitto Kabwe ni mwenyekiti mstaafu wa chama cha
ACT- Wazalendo aliyehudumu nafasi hiyo kwa muongo mmoja. Zitto alihamia ACT- Wazalendo mwaka 2015. Kupitia tiketi ya CHADEMA Zitto aliwahi kuwa mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini mwaka 2005 mpaka 2015.
Balozi
Humphrey Polepole ni wanasiasa na mwanadiplomasia kutokea nchini Tanzania ambaye amaye amewahi kuhudumu katika nafasi mbalimbali ndani ya chama cha mapinduzi (CCM), mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzani na Balozi wa Tanzania nchini Malawi na baadaye Cuba.
Mnamo mwezi Julai 13, 2025 Polepole, kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagramalichapisha
barua iliyotoa taarifa ya kujiuzulu nafasi ya ubalozi, ambapo kabla ya Taarifa hiyo alikuwa balozi wa Tanzania nchini Cuba. Polepole alisema
"Kwa Imani yangu, kwa hofu ya Mungu niliyonayo, kwa misingi ambayo nikuzwa na kujifunza na kwa itikadi ambayo nimeiamini, imenibidi kufanya uamuzi huu."
Ipo taarifa inayosambazwa katika mtandao wa Facebook ikitumia utambulisho wa grafiki za Millard Ayo, Jambo TV na The Chanzo, kuwa Zitto Kabwe amesema "Polepole ni mnafiki na kuhoji ulikuwa wapi wakati nashughulikiwa 2020?"
Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani hakuna chanzo rasmi kilichoonesha kama kauli hiyo imetolewa na
Zitto.
Vilevile grafiki zilizotumika kusambaza taarifa hiyo (
Jambo TV, Millard Ayo na
The Chanzo) ni za kughushi kwani hazijachapishwa na vyombo hivyo, bali zimetengenezwa na wapotoshaji ili kusambaza taarifa isiyo ya kweli.