Zitto Kabwe anahoji kuhusu Kiwanda cha Sukari, Kampuni ya Mkulazi Holdings

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Mwanasiasa anayeongea kwa Takwimu, Zitto Kabwe kaandika hivi;

Juzi Nimeuliza hapa kuhusu Mradi wa Kiwanda cha Sukari Kampuni ya Mkulazi Holdings ambayo inamilikiwa na Shirika la NSSF na Jeshi la Magereza.

Swali langu rahisi sana, KWANINI Wakala wa Barabara TANROADS ndiye aliyenunua mitambo ya kuzalisha Sukari? KWANINI mitambo haijafika?


Siku tatu zilizopita alihoji;

Mradi wa kuzalisha Sukari tani 250,000 huko Mkulazi Morogoro umekwamia wapi? Tulipaswa kuwa tunajitegemea kwa Sukari sasa. Mradi wa tangu mwaka 2016 unaofadhiliwa na Fedha za NSSF na PSSSF umefikia wapi? Mara ya mwisho kuusikia ni Machi 16, 2021 Waziri Mhagama alipotembelea huko

Kilombero doubles capacity. Bakhresa Bagamoyo Sugar at 80% to completion. Mkulazi Holdings imefikia wapi Mradi wake wa kuzalisha Sukari? Afrika Mashariki ni Soko 1 kupitia Itifaki ya Soko la Pamoja ya Jumuiya. Tukiongeza uzalishaji wa Sukari tutauziana, tutashindana.
 
Zito kwa sasa ana uwezo wa kuongea au kuandika lolote, liwe la faida au hasara kwa taifa he doesn't care, ilimradi yeye mkono wake uende kinywani tu.
Una maanisha nini?
 
Mradi ule ulishindikana, Miwa ile chini iliyolimwa yote nasema yote iliuzwa kiholela na mradi ukafa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…