Zitto Kabwe apendekeza TANESCO wauze hisa(20%) fedha itakayopatikana ilipe madeni, Waziri Makamba atoa maagizo

Tulisema january amepelekwa kwa manufaa ya watu binafsi. Hata juma halijaisha anakuja na mapandekezo ya kuuza hisa za tanesco kutoka serikali eti kulip madeni. Madeni yenyewe mengi ni feki. Shirika la tanesco ni dude kubwa na muhimu kutoa huduma. Ni nani hao watapenda kununua hisa shirika ndio kwanza linaanza kuweza kujiendesha hata faida halipati? Jaribio la kubinafsisha wakati wa mkapa liliishia kwa wajanja kupiga tu hela za umma. Makaburu waliyopewa kuendesha kwa mkataba waliishia kuliibia tu shirika mabilioni.
January asiruhusiwe kufanya chochote kikubwa maana hata uwezo hana. Badala yake hatua kudhibiti wizi na ujanjaujanja wa kulihujumu na kuliibia shirika zitumike.
Msiwe wasahaulifu haraka. Kumbukeni kilichotokea ttcl kwa kisingizio cha kubinafsisha shirika. Watu binafsi kujinufaisha kwa gharama ya umma.
Huyo zitto na january lao moja tu ni watu wapigaji.
 
Ndio maana Makamba akateuliwa, harafu Zitto ndio zumari lao kujidai anapendekeza wakati ni agenda ya kikundi chao akiwemo SHH.Uzen tu Tanesco
Huyo SHH ujue anatokea ngo's. Hawa wengi wamepikwa uliberali na huanguka kirahisi kwenye mitego ya kibeberu. Watuachie tanesco yetu na huyo makamba yafaa atolewe mara moja. Tumeweza kusambaza umeme nchi nzima kutokana na uwepo wa tanesco katika muondo wake. Watatuletea balaa lingine.
 
Tanesco kuuza hisa chini ya utawala wa CCM ni ndoto. Ni kibubu cha CCM.
 
Wazo la kubinafsisha tanesco achilia mbali ttcl ni wazo zuri sana kwa mtu anaethnk po+ . Ni vzur kwakua kwasasa hio unayosema kunatija kuendeshwa chni ya serikali ni Big NO. Hapa tuangalie tuu namna nzuri ya ubinafsishaji, mwekezaji sio lazima atoke nje, pia tuweke mfumo mzur wa kudhibiti wizi, uhujumu wa shirika na mfumo mzur utakao mpa bei nafuu ya units mwananchi.
Wewe unahofu tuu kwa mfumo wa sasa wa uwekezaji kuwa tunaweza kupigwa,, YES tunaweza kuibiwa but best b4 investing tufanye tafiti na uchunguzi kutoka nchi zlizoruhusu mashirika binafsi yalivowekeza Kwenye umeme apa mabarozi wanahusika sana kama watajitambua.
My take: tanesco ibaki mmiliki wa sources of energy na muuzaji wa energy hio kwa mainvestors ambao wao watafanya kazi kubwa upande wa distribution.
Hapa tenda itolewe na pia serikali isimamie vigezo na tija katika kuwanufaisha watumiaji wa mwisho.
 
Mlianza na IPTL, hamkuridhika, mkaja na Richmond hamkuridhika nk. sasa mnataka kuiua kabisa Tanesco. Kumbe ndiyo maana wafanyakazi wa Tanesco wanafanya hayo wanayoyafanya - wanahisi soon tanesco haitakuwepo.
Zitto kumbuka ya NBC, Mwalimu Nyerere alishauri wakaziba masikio - masikini Nyerere, nadhani alikufa akiwa na masikitiko makubwa.
 
Wanasiasa huwa ni wachumia tumbo tu,unaweza kukuta Kuna wafanyabiashara wapo nyuma yao,Wana fanya lobbying hisa za shirika ziuzwe,
Wakati mjadala wa wabunge kutokulipa Kodi na viwango vya Vipato vyao,umepamba moto,Hawa wanasiasa walikaa kimya hakuna aliyejitokeza kusema ni kiasi gani wanavuta,Kabwe,Mdee na wenzie wote walipiga kimya,
 
Mkuu acha ukichaa

Yaani unakaa hapa unadanganya wananchi ATCL ilijenga faida 2020?

Yaani upo hapa unatuletea upumbavu wa lile limfu kudanganya dunia eti ATCL ilileta faida 2020?

Punguza uongo na unafiki na uzandiki
Hivi ATCL haijawahi kutoa gawio!
 
Nimekumbuka kampuni fulani ambayo baada kuinunua mnunuzi alitumia asset zake (kampuni) kukopa hela nyingi benki na hakulipa deni. Baada ya muda srikali ikasema kampuni hii iko kwenye interest kubwa ya serikali, ikaamua kuichukua tena na kulipa madeni yote, Same will be for Tanesco
 
Yajayo yanafurahisha Ok,unaweza ukakuta wajanja wanapita humo humo kwenye hisa,tukija kushtuka tushaumia hata mkiwakamata baadaye wanatoka wanakuwa mashujaa kama Rugemalia.

Hii nchi........ (Kwa sauti ya Mrema).

Mtanikumbuka.
 
Ushauri wangu kwako Mheshimiwa Waziri kwanza kabisa vunja hiyo bodi na ng'oa menejimenti yote na kusuka safu mpya yenye wataalamu wenye weledi usiotia shaka na uzalendo kindakindaki.Bodi goi goi huzaa menejimenti goi goi na uzembe,wizi,uvivu na kiburi kwa watendaji wa chini na kunajisi ufanisi mzima wa Shirika.

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
 
Kumbuka miaka iyo tuliyokuwepo enzi ya ttcl,na leo hii tupo katika teknolojia gani,ndio utaelewa Tanesco bila ya kupata ushindani umeme bado utatusumbua sana
 
Walianza IPTL kama sikosei
Wameanzia mbali mpaka nimesahau!!
Hasara ya Tanesco kwa asilimia kubwa imechangiwa na mikataba mibovu!

Watu wanajuha bwawa la Nyerere likiisha na kuanza kuzalisha Umeme. Halafu mikataba mibovu ikavunjwa na kuwaondoa wafanyakazi wazembe. Tanesco kupata hasara itakuwa historia.

Sifa atapewa Marehemu!!
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…