Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 22,269
- 58,563
Leo nitakuwa uwanjani kuwapa support Taifa Stars. Nitavaa Jezi Rasmi ya Taifa Stars ambayo ni hii. Hakuna Jezi nyengine zaidi ya hii.
Nilizungumza na Waziri Paul Makonda kuhusu huu mjadala wa Jezi na nikwamwambia ni mjadala hauna maana kabisa. Alinipa maelezo yake na nikwambia baadhi ni maelezo mazuri kabisa lakini yanapaswa kujadiliwa mezani na kelele mitaani. Nilizungumza na watu wa sandaland pia na kuwaambia wanapaswa kukaa na Wizara ili kuchukua mawazo yao.
Kutaka NIKE wauze jezi zetu Haina shida, NIKE wanunue rights kutoka Sandaland. Uongozi unataka kutoa empowerment kwa wananchi wako. Kama Sandaland tayari Ana mkataba na TFF.
Halafu tumewapata NIKE hakuna shida. Waziri angemsaidia Mtanzania kuhamisha rights kwa NIKE ambapo Taifa lingefaidika na Mtanzania angefaidika sana. Waziri kutangaza kuwa jezi mbaya inaonyesha kuwa hakai wizarani na hafuatilii kazi zake za uwaziri.
Jezi ambayo tayari Timu ya Taifa inavaa unatangazaje kuwa ni mbaya? Timu inacheza kesho na ipo kwenye ratiba badala ya ku focus kwenye ushindi wa Timu tunahamisha mjadala kwenye jezi. Mchakato wa Jezi ni mrefu, Waziri kulalamika mtaani ni kushindwa uongozi. Narudia Waziri Makonda na kampuni ya sandaland waachane na huu mjadala usio na maana yeyote. Huu ni mjadala wa watu walioshiba.
Ni mjadala unaondoa focus kwa Timu. Mambo yote Waziri anataka yanaweza kuboreshwa kwa kukaa na Sandaland. Waziri amefanya kosa kubwa kuukuza Huu ugomvi usio na maana kabisa. Paul Makonda weka mawe mfukoni tafadhali. Elekeza nguvu kwenye kuboresha tufanye vizuri.
Sandalandtheonlyone achana na mambo ya mahakamani. Kaeni chini na Waziri kupata jawabu. Mkataba wa kuzalisha Jezi ni halali na unapaswa kutekelezwa. Ubora wa jezi ni jambo la kuboresha na sio jambo la kelele za mtaani.
Kuendeleza mjadala Huu ni ku JINX national team. Kama Waziri Makonda anao NIKE awaite waongee na Sandaland kisheria ili kuhamisha rights commercially. Kutaka kutafuta sababu za kipuuzi kumnyanganya mkataba sandaland ni UZWAZWA na UNDEZI wa Hali ya Juu sana.
Unamnyanganya vipi MZAWA mwenye mkataba na kumpa mgeni badala ya kumwunganisha huyo mzawa na Nike? Hizo hazitakuwa akili itakuwa ni Matope yamekaa kichwani tu