Zitto Kabwe atoa kauli kuhusu chaguzi ijayo ya Kenya

Zitto Kabwe atoa kauli kuhusu chaguzi ijayo ya Kenya

mkuu unasema usipoweza kujikuna inabidi ukunwe na jirani?? kwetu bara mwanaume kukunwa ni dhambi kubwa. sijui huko mchambawima

Mchamba wima na Kajamba nani waachie wenyewe. Ni ipi nzuri kuruhusu wachina wat kutoka mbali kama China kuja kuwekeza umachinga Kariakoo au kuruhisu jirani kuja kuwekeza? Ikiwa una ardhi mzuri ya kufugia ng'ombe na huku wewe unaishi kwa kuvua samaki mtoni ni busara kumwalika jirani aje atumie ardhi ile kwa kufugia ng' ombe ili wewe upate maziwa na samaku wajo wapate chakula kizuri kutokana na kuwepo kwa ng'ombe hao.
 
Kenya-pamoja na kuchinjana na ukabila wao bado wanatupiga bao. We need to shut up!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! and mind our own #$%& business. Hatuna jipya, tutaendelea kushika mkia tu

Mimi nadhani, kuwa kufanya kwao maamuzi ya kikabila wanajirudisha nyuma. Wangekuwa mbali zaidi, na watu wa kawaida, ambao sio hawa mamilionea wanasiasa wangekuwa pia wanafaidika na hizi biashara kubwa tunazoziona.

Umasikini, ukosefu wa fursa na ujinga uliopo kenya ni wa hali ya juu sana kuliko Tanzania, hawa tunawajali?
Au na sie tumeshakuwa na mentality ya kibepari kabisa kuwa - kwa kuwa kuna matajiri, investments, barabara, na vitu vingine muhimu (vilivyowevwa ili investments zikue) basi nchi inaendelea?

Sie tunaweza tusiende kuwa waumini wa kufanya maamuzi ya ukabila, au udini lakini kwa uhakika sasa wenye mali na wanasiasa uchwara wameshikamana. Sie tusio nazo bado hatujashikana tunapelekeshwa. nadhani hili ni baya kuliko hata ukabila
 
Mkuu hapo kwenye nyekundu unaweza kutupa mifano ya uwekezaji ya waingeraza hapa nchini zaidi ya Barclays Bank na Standard Chartered Bank? Just curious to know more.

Ukiachilia mbali hizo benki, wana biashara nyingine mbalimbali hapa Tanzania, kuanzia mashamba na utitiri mwingine wa biashara (kama ilivyo kwa Unilever Tanzania, Brooke Bond Tea) wapangishaji wa majengo, Knight Frank, wana hisa Serengeti Breweries na kadhalika. Maelezo ya Balozi wao hapa Tanzania yanasema hivi:-

"As development partners, Britain has historically been Tanzania's largest donor, and our aid programme is now the largest it has ever been. In the commercial sphere, we remain the biggest investor, with British investors in all areas of the Tanzanian economy, large and small.
Mwaka jana, gazeti la Business Times Tanzania la Tanzania ndili lililotoa takwimu hizo, kwa kushirikiana na Wizara yetu ya Uchumi na Uwekezaji.
Pitia zaidi HAPA na HAPA

Sijajua kwa nini Wachina na Wahindi hawajawa kwenye kundi la wawekezaji wakubwa hapa Tanzania. By the way tusiende zaidi nje ya mada ya Zitto.
 
Back
Top Bottom