Hehehehe!! Nimecheka Sana, nimeikuta u-tube. Kweli kabisa wimbo na ngoma ni tamaduni za kirundi. Nimefanya kazi Kambini miaka ya 90 nafahamu tamaduni zao.
Ngoma za kiha kunatofauti kidogo Ila zinaelekeana.
Warundi wameendelea kutukuza Ngoma yao na kuboresha zaidi hivi nyimbo zao na Ngoma zinavutia Sana hasa Kama unafaham lugha za Kiha,kihangaza,kirundi,kinyarwanda,kishubi- na kwa mbaali kisubi(maeneo hayo ni Kigoma na Ngara na pia karagwe na Tabora maeneo ya Mwese.
Kwakua nyimbo zao zinavutia Basi watanzania wa maeneo hayowanaziadopt na kuzicheza
sasa, swala la kua VP ni mrundi au la, hao watu wa maeneo hayo huwezi watofautisha kwa sura,kuzungumza na tamaduni.
Kwa vyeti na makaburi ya Babu zao, makaburi yasizidi matatu kwa umri wa mpango.
Naomba kuishia hapo.